Fahamu Juisi Ya Kutumia Ili Kukomesha Uvutaji Sigara

Juisi zenye vitamini ni msaada mkubwa katika kukomesha uvutaji sigara na kuboresha afya yako hasa katika mfumo wako wa hewa.


                                Kuacha Kuvuta Sigara

Ili kuacha kuvuta sigara, mwili huwa unahitaji vitu; maji na baadhi ya vitamini;

  • Maji ili kuondoa sumu ya nikotini. Nikotini ndio alkaloid kuu kwenye tumbaku ambayo inaweza kuondolewa au “kusafishwa” kwa maji, tofauti na dawa zingine ambazo ini hushindwa kuziondoa.
  • Vitamini C hubadirisha athari za nikotini iliyobakia mwilini. Vitamini C ndio topozi (antidote) kuu kwa nikotini.
  • Vitamini A, hutumika kukarabati seli za uteute makamasi(mucus) unaokuwa kwenye njia ya upumuaji iliyoharibiwa na moshi wa sigara.
  • Vitamini B, hutumika kukinga wasiwasi na kusaidia kujenga utashi wa kuacha kuvuta sigara.

Juisi ya kuacha kuvuta sigara humpatia mvutaji viambata vyote katika uwiano unaotakiwa kumsaidia mvutaji wa zamani: Vitamini C kwenye ndimu, vitamini A kwenye karori, na vitamini B kwenye kiini cha ngano. Pamoja na hayo, ndimu zina faida zinazofanana na zile za bazoka za nikotini za kuondoa hamu ya kutaka kuvuta, kulingana na utafiti uliofanyika katika chuo kikuu cha Srinakharnwirot Thailand. 

VIUNGO

Unataka kuchanganya viungo hivi unatakiwa kufanya kama hivi ifuatavyo:

  • Ndimu au limao 2
  • Karoti 4
  • Viini vya ngano kijiko 1 cha mezani
  • Majani ya mnanaa

MAANDALIZI

a) Menya hizo ndimu (ondoa maganda ya kutosha ili kuepuka ladha yake kali)

b) Andaa limao na karoti kwenye blenda

c) Ongeza kiini cha ngano, koroga mpaka vichanganyike

d) Ongeza majani ya mnanaa.

MATUMIZI

Jitahidi kunywa hadi bilauri 3 kwa siku za juisi za mchanganyiko wa matunda hayo. Hii itakufanya kuwa rahisi kwa mvutaji sigara kuacha kuvuta kwa kadiri unavyotumia mchanganyiko huu.

Neno La Faraja: Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Rafiki msomaji, makala yetu inaishia hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.

Kama unahitaji huduma nyingine zaidi, basi tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!





Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa