Jinsi Ya Kuandaa Juisi Ya Kupambana Na Kikohozi Kigumu

Kama ilivyo shira (syrup) halisi, juisi pia husaidia kupambana na kikohozi kigumu na kusafisha njia yote ya upumuaji na kupambana kikohozi.

                                      Pumua Kwa Kina

Juisi ya Pumua Kwa Kina haizuii kukohoa. Jambo zuri ni kwamba, kikohozi kwa ujumla ni kitendo kisicho cha hiari cha ulinzi wa mwili kinachotumika kuondoa makohozi yaliyokusanyika kwenye mirija ya hewa. Kwasababu hiyo, sio vizuri kuzuia kikohozi ila kiruhusu ili njia ya upumuaji isafike mapema iwezekanavyo.

Juisi ya Pumua Kwa Kina haizuii kukohoa, shukrani kwa uwepo wa shimari(fennel) na kitunguu kwani hufanya makohozi kuwa mepesi na hivyo husaidia kuondolewa kwa urahisi. Kwa njia hii kikohozi huwa sio kikali na hivyo huondolewa kwa urahisi mno.

Karoti husaidia kukarabati uteute makamasi unaokuwa kwenye mirija ya hewa na kusaidia kuponya mfumo wa hewa. Asali yenyewe huwa imebeba viini vya protini vinavyoambatana na maambukizi na kusafisha mfumo wa hewa. Kwa njia hii basi, mchanganyiko wa juisi hii husaidia kusafisha njia ya hewa na kuondoa makohozi.

VIUNGO

Ili uweze kuandaa mchanganyiko wa juisi hii ambayo itakuwa dawa nzuri kwako, basi chukua vitu hivi:

  • Tunguu shimari 1
  • Kitunguu maji 1/2
  • Karoti 3
  • Asali kijiko 1 cha mezani

MAANDALIZI

a) Katakata, karoti, kitunguu maji, tunguu shimari, changanya halafu blendi kwenye blenda kwa pamoja.

b) Ongeza asali

MATUMIZI: Tumia juisi yako ikiwa yenye joto la kawaida, usitumie ikiwa ya baridi.

Neno La Faraja: Heri wenye moyo safi maana hao watamuona Mungu. Matayo 5:8.

Rafiki, somo letu linaishia hapa, tunakaribisha kipindi chako cha maswali. Unahitaji ushauri, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Karibu sana!

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa