Jinsi ya Kuondoa Sumu Kwenye Kongosho Lako Kwa Njia Ya Asili Kwa Kutumia Aina Tatu Tu Za Juisi!
Kongosho ina umbo la peasi lakini tambarare, huku likiwa na eneo pana linaloitwa "kichwa," shingo na mwili katikati, na sehemu ya mwisho iliyo nyembembe inaitwa "mkia."
Kongosho ni tezi ndefu yenye urefu wa inchi 6 ambayo iko kwenye tumbo.Tumbo, ini, wengu au bandama, utumbo mwembamba na kibofu cha nyongo ndivyo vinalizunguka kongosho.
Kongosho ina kazi kuu mbili: endocrine na exocrine. Seli za exocrine za kongosho huunda enzymes zinazosaidia kusaga chakula.
Jinsi Ya Kuondoa Sumu Kwenye Kongosho Lako Kwa Kutumia Juisi
Zifuatazo hapo chini ni baadhi ya juisi zenye afya unazoweza kutumia kwa ajili ya kongosho lako:
1. Cauliflower, lettuce na juisi ya karoti
- Tawi la celery.
- Glasi ya juisi ya karoti.
- Kikombe cha cauliflower ya Brussel (iliyo na mvuke).
- Nusu glasi ya maji.
Weka kila kitu kwenye blenda na uchanganye vizuri, kisha uichukue juisi yako, halafu kunywa polepole.
2. Juisi Ya Aloe Vera Na Juisi Ya Artichoke
- 1/2 kikombe cha maji ya moto.
- Artichoke ikiwa imepikwa na kuwa laini
- Juisi ya limao 1/2 kikombe
- Kikombe 1cha juisi ya aloe
Weka vitu vyote kwenye blenda, saga ili upate mchanganyiko, juisi lazima iwe ya vuguvugu na lazima iwe nzito, ambayo ni nzuri kwa kuponya kongosho. Hii inatumiwa wakati wa chakula cha mchana.
3. Juisi Ya Papai Na Mbegu Za Kitani
- Lozi (almond) tatu
- Kipande kikubwa cha papai
- Nusu glasi ya maji.
- Kijiko cha unga wa flaxseed
Hii inatumiwa asubuhi na ni rahisi sana kuiandaa, saga vyote kwenye blenda yako pamoja na nusu glasi ya maji. Inatumiwa kwa kunywa kidogo kidogo kila asubuhi na utaona kwamba italipatia virutubisho kongosho lako na litakuwa na afya.
Rafiki msomaji, ujumbe wa mwisho wa injili unatusisitiza kwamba, “wafundishe watu namna ya kutunza afya, namna ya kuepuka ugonjwa. Hii ni sayansi ya kweli”. Place of Herbs, E. G. White, Ukr. 13.
Neno La Faraja: Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe, usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako, nitakutia nguvu, naamu nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Isaya 41:10.
Je, unahitaji huduma zaidi na ushauri? Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Karibu sana!
Comments
Post a Comment