Fahamu Chakula Bora Kwa Uzazi Wa Mwanaume
Kwanza napenda kuwapongeza wale wote ambao huwaandaa vijana wa kiume kuwa wababa bora kwa kuwapa mafunzo stahiki. Ili kiwanda cha mbegu kifanye kazi kwa ubora, kinahitaji mlo wenye virutubisho vya kutosha. Kula mlo wenye afya na kufanya mazoezi ya kutosha kunasaidia kuweka mbegu za kiume katika hali nzuri.
Vipo vyakula muhimu sana ambavyo baba mtarajiwa anapaswa kuvipata. Navyo ni hi vifuatavyo:-
1. Matunda.
2. Mbogamboga.
Mboga lishe ni muhimu sana kwa baba anayehitaji mtoto. Mboga mchanganyiko zisizopungua saba. Mfano, michicha, mnafu, tembele, bamia, majani ya maboga, majani ya kunde, mlenda. zote hizi zipikwe pamoja.
3. Nafaka zote.
Viazi vitamu viliwe sana, mahindi ya kuchemsha na ndevu zake pamoja na muhogo hasa muhogo mbichi.
4. Vyakula vya protini ni muhimu sana. Vyakula hivi visikose angalau mara mbili kwa wiki.
5. Vyakula vya maziwa.
Vyakula hivi ni kama maziwa fresh, mtindi na jibini, kwa sababu vina mafuta ambayo ni muhimu katika kiwanda cha kuzarishia mbegu za mwanaume.
Ni virutubisho gani vinaweza kuboresha uwezo wa kutengeneza ujauzito kwa mama?
1. MADINI YA ZINKI.
Madini haya yana umuhimu sana katika swala zima la uzazi kwa mwanaume. Utafiti umeonyesha kuwa wanaume wengi wenye matatizo ya uzazi hawapati madini ya zinki ya kutosha ili kuweza kuongeza idadi ya mbegu za kiume zilizokomaa. Tumia nafaka kwa wingi.
2. MADINI SELINIAMU.
Utafiti umeonyesha kuwa virutubisho vinaweza kuimarisha kiwanda cha mbegu za baba na hivyo kutatua matatizo ya uzazi, kwa hiyo seliniamu ni muhimu katika kuboresha afya ya mbegu za kiume. Seliniamu hupatikana katika vyakula kama vile karanga, ufuta, samaki, nyama n.k.
3. VITAMIN D
Utafiti unaonyesha kuwa vitamin D inaweza kuwa muhimu kwa kusaidia kasi ya mbegu za kiume kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Vyanzo vya vitamin D ni samaki ya mafuta,nyama nyekundu,ini,viini vya mayai ya kienyeji, siagi na nafaka.
4. ASIDI YA FOLIKI
Kirutubisho hiki kina kazi ya kukomaza mbegu za kiume ili ziwe na afya. Vyanzo vya aside foliki ni mboga za majani kama spinachi,matunda yenye nyuzinyuzi kama machungwa, maharage,mikate, nafaka n.k.
5. ANTIOXIDANTS
Hivi ni virutubisho vipatikanavyo katika vyakula venye vitamin C au E ambavyo husaidia kurekebisha na kulinda seli zilizoathiriwa. Virutubisho hivi hasa hupatikana katika stafeli aina zote, apple na zabibu.
ANGALIZO
Vifuatavyo ni vitu ambavyo
huathiri utendaji kazi wa kiwanda cha mbegu cha baba;
·
Uzito mkubwa.
·
Unywaji wa pombe.
· Ulaji wa chakula cha aina moja.
Kwa ushauri, naomba utume ujumbe au wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda.
Karibu sana!
Comments
Post a Comment