Fahamu Mambo 3 Yanayopelekea Kuvimba Kwa Shingo Ya Kizazi

Kuvimba kwa shingo ya kizazi kitaalamu tunaita, “Cervicitis”, nayo huwa ni sehemu nyembembe inayokuwa chini mwishoni mwa tumbo la uzazi ambayo hufunguka ndani kwenye uke.

Dalili za kuvimba kwa shingo ya kizazi ni pamoja na kutokwa na damu ya hedhi kwa kujirudia mara mbili ndani ya mwezi mmoja, kuhisi maumivu wakati unaposhiriki tendo la ndoa, na kutokwa na uchafu ukeni. Hata hivyo, pia inawezekana kupatwa na hali ya kuvimba kwa shingo ya kizazi na kushindwa kuona dalili au ishara zozote.




Mara nyingi, kuvimba kwa shingo ya kizazi kunaweza kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa, kama vile pangusa au kisonono. Uvimbe wa shingo ya kizazi unaweza kutokana na magonjwa ya siyo ambukiza pia. Matibabu ya ugonjwa huu huhusika na kutiba uvimbe wa shingo ya kizazi.

Mara nyingi, kuvimba kwa shingo ya kizazi huwa hauonyeshi dalili, na unaweza kujifunza tu ugonjwa baada ya kupata vipimo. Ikiwa kama una dalili, basi zinaweza kuwa pamoja na hizi zifuatazo:

  •  Kutokwa na uchafu mwingi usio wa kawaida ukeni
  • Kuhisi maumivu wakati unapokojoa mara kwa mara
  • Kuhisi maumivu wakati unaposhiriki tendo la ndoa
  •  Kutokwa na damu ya hedhi kujirudia mara mbili ndani ya mwezi mmoja
  • Kutokwa na damu ukeni baada ya kumaliza kushiriki tendo la ndoa

 Je, Nini Visababishi Vyake?

Visababishi vinavyofanya shingo ya kizazi kuvimba ni hivi vifuatavyo:

1.     Maambukizi Ya Magonjwa Ya Zinaa

Mara nyingi, maambukizi ya bakteria au virusi ambayo husababisha shingo ya kizazi kuvimba huambukizwa kupitia ngono. Kuvimba kwa shingo ya kziazi hutokana na maambukizi ya zinaa, ikiwa pamoja na kisonono, pangusa, malengelenge pamoja na mkanda wa jeshi.

2.     Athari Za Mzio

Mzio, au dawa za uzazi wa mpango au kondom, vinaweza kupelekea shingo ya kizazi kuvimba. Athari za bidhaa za wanawake kwa ajili ya usafi, kama vile sabuni zenye kuondoa harufu, pia zinaweza kusababisha kuvimba kwa shingo ya kizazi.

3.     Bakteria Kukua Kwa Kasi

Bakteria wanaokua na kuzaliana kwa wingi ukeni kwa kawaida hupelekea shingo ya kizazi kuvimba.

Je, Nini Vihatarishi?

Uko katika vihatarishi vikubwa vya kuvimba kwa shingo ya kizazi, ikiwa kama:

·        Una tabia ya kushiriki tendo la ndoa bila kinga, kuwa na wapenzi wengi au kushiriki tendo la ndoa na mtu ambaye ana tabia ya kushiriki na wapenzi wengi

·        Ulianza kushiriki tendo la ndoa mapema ukiwa bado mdogo

·        Uliwahi kupatwa na magonjwa ya zinaa. 

Je, Nini Madhara Ya Kuvimba Kwa Shingo Ya Kizazi?

Shingo yako ya kizazi hufanya kazi kama kinga ili kuzuia bakteria na virusi wasiweze kuingia kwenye tumbo la uzazi. Wakati shingo ya kizazi inapoambukizwa, kuna vihatarishi vikubwa kwamba maambukizi watasafiri na kuingia kwenye tumbo la uzazi.

Uvimbe wa shingo ya kizazi ambao husababishwa na kisonono au pangusa unaweza kuenea kwenye ukuta wa tumbo la uzazi na kwenye mirija ya uzazi, na hivyo kusababisha PID, maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke ambayo yanaweza kusababisha matatizo ya uzazi ikiwa kama hayajatibiwa.

Kuvimba kwa shingo ya kizazi pia kunaweza kuongeza vihatarishi vya kupata HIV kutoka kwa mpenzi mwenye maambukizi.

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa zenye uwezo mkubwa wa kuondoa vyanzo vya kuvimba kwa shingo ya kizazi, nazo ni MULTICURE POWDER, PERFECT POWDER na CARD HERB.

Ndugu msomaji, Makala yetu ndio inaishia hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako. Pia unaweza kutuma namba yako ya WhatsAp ili tuweze kukuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.

Je, Unahitaji Huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 570 au 0712 181 620,

Arusha-Mbauda.

Karibu sana!

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa