FAHAMU MAMBO 5 YANAYOSABABISHA MAUMIVU MAKALI YA TUMBO WAKATI WA UJAUZITO

Maumivu ya tumbo (tumbo la chini) ni kawaida katika ujauzito. Kwa kawaida huwa sio mambo ya kukufanya uwe na wasiwasi sana, lakini wakati mwingine inaweza kuwa ishara ya jambo zito zaidi ambalo linahitaji kuangaliwa kwa umakini.

Huenda ikawa sio kitu cha kukutia wasiwasi ikiwa maumivu ni kidogo na yanaondoka unapobadilisha eneo, au unapopumzika au unapokojoa. Lakini ikiwa una maumivu ya tumbo na una wasiwasi, mpigie mkunga wako au fika hospitali haraka kwa ajili ya kupata huduma.

Fika hospitalini haraka au kwenye kituo cha afya ikiwa kama:

  • Unatokwa na damu nyingi au matone
  • Tumbo linakaza sana
  • Unatokwa na uchafu ukeni usio wa kawaida kabisa
  •  Kiungo kinauma
  • Unahisi maumivu wakati unapokojoa

·        Maumivu ni makali sana na wala hayatoweki baada ya kuwa umepumuzika baada ya dakika 30-60

Chochote kati ya dalili hizi inaweza kuwa ni kitu ambacho kinahitaji kuchunguzwa au kutibiwa haraka.


Pata dawa

 Je, Sababu Ya Maumivu Makali Ya Tumbo Ni Nini?

Baadhi ya magonjwa ambayo yanaweza kusababisha maumivu makali ya tumbo yanahitaji kuchunguzwa haraka.

  1. Mimba Kutunga Nje Ya Kizazi (Ectopic pregnancy)

Huu ndio wakati yai lililorutubishwa huy)jishikisha nje ya tumbo la uzazi, kwa mfano kwenye mrija wa uzazi. Mimba haiwezi kuishi na inahitaji kuondolewa kwa dawa au upasuaji.

Kwa kawaida dalili huonekana kati ya wiki 4 au 12 za ujauzito na zinaweza kuwa kama hizi zifuatazo:

  • maumivu ya tumbo na kutokwa na damu
  • maumivu katika ncha za bega
  • usumbufu wakati wa kukojoa  

1.     2. Mimba Kuharibika Au Kuporomoka

Maumivu ya kubana na kutokwa na damu kabla ya wiki 24 za ujauzito wakati mwingine inaweza kuwa ishara ya kuharibika kwa mimba au tishio la kuharibika kwa mimba (unapotokwa damu lakini kwa kawaida ujauzito unaendelea).

1.     3. Shinikizo La Juu La Damu Wakati Wa Ujauzito

Maumivu chini ya mbavu ni ya kawaida katika ujauzito wa baadaye kutokana na mtoto anayekua na mfuko wa kizazi unapokandamiza chini chini ya mbavu.

Lakini kama maumivu haya ni mabaya au ya kudumu, hasa upande wa kulia, inaweza kuwa ishara ya shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito (pre-eclampsia) ambayo huwapata baadhi ya wajawazito. Kawaida huanza baada ya wiki 20 tu au baada ya mtoto kuzaliwa.

Dalili zingine za presha ya kupanda au shinikizo la damu wakati wa ujauzito ni kama hizi zifuatazo:

  •  Maumivu makali ya kichwa
  • Matatizo ya kutokuona
  • Miguu, uso na mikono kuvimba

 Utahitaji kufuatiliwa hospitalini.

Iwapo una mimba ya chini ya wiki 37 na unakuwa na maumivu ya mara kwa mara kwenye nyonga au kubana, mpigie mkunga wako.

Hii inaweza kuwa ishara ya leba kabla ya wakati, na utahitaji kufuatiliwa hospitalini.

1.     4. Kondo Kupasuka

Huu ndio wakati kondo linapoanza kutoka kwenye ukuta wa tumbo la uzazi, kwa kawaida husababisha kutokwa na damu na maumivu makali ya mara kwa mara ambayo hayaji na kuondoka kama maumivu ya kubana.

Wakati mwingine ni dharura kwa sababu ina maana kwamba kondo la nyuma linaweza kukosa kumudu mtoto wako ipasavyo.

Unapaswa kwenda hospitali ili wewe na mtoto wako mchunguzwe.

1.     5. Maambukizi Katika Njia Ya Mkojo (UTI)

UTI ni ya kawaida wakati wa ujauzito na inaweza kutibiwa kwa urahisi. Inaweza kusababisha maumivu ya tumbo na wakati mwingine, lakini si mara zote, maumivu wakati wa kukojoa, nk.

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya tumbo kuuma, nazo ni REDEEMER, CARD HERB na FRESH HERB.


Asante sana rafiki mpendwa unayefuatilia makala hii. Naomba niishie hapa nikaribishe kipindi cha maswali na maoni.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WhatsAp ili uweze kujiunga katika darasa letu la mafunzo juu ya afya.

Je, Unahitaji huduma? Basi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626.

Arusha-Mbauda.

Karibu sana!

 


Comments

Popular posts from this blog

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa