Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo
Figo ni viungo vidogo vinavyofanana na maharage ambavyo vina jukumu la kufanya baadhi ya kazi muhimu zaidi mwilini mwako. Kwa mfano, figo zinawajibika katika uzalishaji wa homoni muhimu; huondoa uchafu kwa njia ya mkojo, huchuja damu, na hutengeneza uwiano sawa wa majimaji na madini.
Ugonjwa wa figo au uharibifu wake hupelekea figo kushindwa
kufanya kazi yoyote kati ya hizi, ambazo inaweza kusababisha uharibifu ndani ya
mwili wa mwanadamu. Kuna sababu mbalimbali za hatari zinazoongeza uwezekano wa
kupata ugonjwa wa figo, kwa mfano shinikizo la juu la damu linapokuwa kubwa kupita
kiasi(presha ya kupanda) pamoja na kisukari kisichodhibitiwa. Sababu zingine za
kawaida za magonjwa ya figo ni pamoja na ugonjwa wa moyo, maambukizi ya VVU,
ulevi na homa ya ini(hepatitis C).
Mara tu figo zinapoharibiwa na kupoteza uwezo wake
wa kufanya kazi, maji mengi, madini na vitu vibaya huanza kujikusanya na
kulundikana kwenye mkondo wa damu.Walakini, unaweza kuzuia uharibifu zaidi na
kuongeza uwezo wa figo yako kufanya kazi kwa kutengeneza lishe bora ambayo ina
vyakula vinavyofaa kwa ajili ya figo ambavyo husaidia kupunguza mkusanyiko wa
taka, madini na maji. Pamoja na kuondoa vitu vyote vya chakula vinavyodhuru
figo.
Je, Kuna Uhusiano Gani Kati Ya Uharibifu Wa Figo Na Chakula?
Mapendekezo ya lishe na vizuizi kwa kawaida
hutegemea na hutofautiana kulingana na hatua ya ugonjwa wa figo au kiwango cha
uharibifu uliotokea. Wagonjwa ambao wanateseka na dalili za awali za ugonjwa
sugu wa figo hupewa mapendekezo na vizuizi tofauti vya lishe ikilinganishwa na
wagonjwa walio katika hatua ya mwisho ya uharibifu wa figo au figo
zinaposhindwa kufanya kazi.
Vyakula Vya Kuepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo Kushindwa Kufanya Kazi.
Wagonjwa ambao wanakabiliwa na dalili za hatua za
mwisho za figo kushindwa kufanya kazi(kidney failure) wanatibiwa kwa kuondolewa
mkusanyiko wa maji na vitu vibaya, nao watapewa mapendekezo tofauti ya chakula.
Wagonjwa wengi wanaougua dalili za hatua ya mwisho au kushindwa kwa figo kushindwa
kufanya kazi za hatua ya mwisho hawana chaguo ila hufuata mlo unaoendana na
figo na kuepuka vyakula vinavyohatarisha kutengeneza mrundikano wa kemikali
hatarishi au virutubishi katika mkondo wa damu.
Miongoni mwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa sugu ya figo, figo zao hushindwa kuondoa madini ya fosforasi, potasiamu na sodiamu kama ipasavyo kutoka kwenye mkondo wa damu. Kwa hiyo, madini haya huwaweka katika hatari ya viwango vya juu vya damu. Lishe bora ya figo inahusu ulaji wa vyakula na vinywaji ambavyo vitahakikisha ulaji wako wa sodiamu na potasiamu hauzidi miligramu 2000 kwa siku, wakati matumizi yako ya fosforasi hayawezi kuongeza zaidi ya miligramu 1000 kwa siku.
Figo ambazo tayari zimekwisha kuharibika huwa na ugumu wa kuchuja taka zinazozalishwa wakati protini inapotengenezwa. Kwa hiyo, wagonjwa wanaosumbuliwa na dalili za hatua ya 1-4 ya ugonjwa sugu wa figo wanatakiwa kupunguza matumizi yao ya protini. Walakini, wagonjwa ambao wanachukua matibabu kwa njia ya kutolewa majimaji na taka, wanaougua kushindwa kwa figo kufanya kazi katika hatua ya mwisho wanahitaji kuongezea matumizi ya protini.
Hapa, angalia Hapa Aina 8 Ya Vyakula Ambavyo Lazima Uviondoe Kwenye Milo Yako:
1. Kola za rangi nyeusi
Soda zenye wingi wa sukari na zenye ladha bandia hujazwa kalori na sukari nyingi, na pia hutiwa vikolezo mbalimbali vyenye madhara tena vyenye wingi wa fosforasi, hasa kola zenye rangi nyeusi.
Watengenezaji wengi wa vyakula hutumia fosforasi
kusindika bidhaa za chakula na vinywaji, haswa kuboresha ladha yake, kuongeza muda
wa kudumu na kupunguza kubadilika rangi. Utafiti unaonyesha kuwa fosforasi bandia
iliyoongezwa huonekana kufyonzwa kwa haraka zaidi na mwili ikilinganishwa na
fosforasi inayotumiwa kupitia nyama ya wanyama, mimea au vyanzo vingine vya
asili.
Viambata vya fosforasi bandia huwa na muundo tofauti kuliko fosforasi ya asili, na kwa hivyo, haizuiwi na protini. Kwa kweli, viungio hivi hugunduliwa kuwapo kama aina ya chumvi, ambayo huingizwa kwa urahisi ndani ya njia ya utumbo. Fosforasi iliyoongezwa kiholela mara nyingi imeorodheshwa kwenye orodha ya viambato vya bidhaa; hata hivyo, kanuni hazilazimishi watengenezaji wa chakula kubainisha kiasi kamili cha fosforasi ya ziada inayoongezwa kwenye bidhaa zao.
2. Parachichi
Parachichi ni vyakula bora zaidi vya lishe ambavyo vinaonekana kuwa na faida kubwa na ya muhimu kwa sababu ya viwango hivi vya viuasumu(antioxidant) vya kupambana na magonjwa, nyuzinyuzi na mafuta ya kuponya ugonjwa wa moyo. Hata hivyo, pamoja na kuwa chakula kikuu cha afya, lakini bado ni bidhaa hatari kwa watu wanaopambana na magonjwa ya figo.
Hii ni kwa sababu ya mkusanyiko mkubwa wa madini ya potasiamu
katika parachichi. Kwa mfano, gramu 150 za parachichi hubeba miligramu 727 za madini
ya potasiamu, ambayo ni mara mbili ya potasiamu iliyopo kwenye ndizi yenye ukubwa wa wastani.
Hebu fikiria, kikombe kimoja cha parachichi kinaweza kukupa zaidi ya asilimia 37% ya kuzuia mg 2000 kila siku. Kwa hivyo, unashauriwa sana kuondoa parachichi na bidhaa zinazotokana na parachichi unapoandaa milo yako ili kuepukana na potasiam.
3. Vyakula Vya Kwenye Kopo
Vyakula vya makopo, ikiwa ni pamoja na maharagwe, matunda, mboga mboga, michuzi na supu, kwa kawaida huletwa nyumbani kwa sababu ya urahisi usiopingika na uwezo wake wa kumudu. Watu wengi ambao kwa kawaida hununua vyakula hivi vya makopo hawafahamu viwango vya juu vya kutisha vya sodiamu inayoingia kwenye vyakula hivi.
Kiasi kikubwa cha chumvi huongezwa kwa aina za
chakula cha makopo kama kihifadhi ili kuongeza ladha na kuongeza muda wa bidhaa.
Kwa sababu ya msongamano mkubwa wa sodiamu katika vyakula vingi vya makopo,
inashauriwa sana kwamba wagonjwa walio na uharibifu wa figo waepuke kabisa, au
wapunguze sehemu kubwa ya matumizi yao ikiwa ni lazima waongeze kwenye mlo wao.
Mara nyingi huwa ni uamuzi bora zaidi kuchagua aina za vyakula vya kopo ambavyo vina sodiamu kidogo au vilivyotiwa lebo inayoonyesha kuwa kuwa "hakuna chumvi". Unaweza pia kupunguza msongamano wa sodiamu kwa asilimia 30-80% kwa kuosha tu na kumwaga vyakula vya kopo. Mbinu hii inafanya kazi vyema na maharagwe ya kopo.
4. Mkate Wa Ngano Isiyokobolewa
Mkate wa ngano isiyokobolewa kwa kiasi kikubwa huchaguliwa kuwa bora zaidi kwa chakula bora kabisa, na mikate ya unga mweupe uliokobolewa, na kusindikwa hudharauliwa kutokana na ukosefu wa virutubisho muhimu. Walakini, unapokuwa na ugonjwa au uharibifu wa figo, inaweza kuwa changamoto kuchagua aina sahihi ya mkate ambayo haitaongeza dalili za ugonjwa wako.
Hata mkate wa ngano isiyokobolewa (brown bread) ni chaguo bora zaidi kwa sababu ya mkusanyiko wake mwingi wa nyuzinyuzi(fiber), lakini wagonjwa walio na uharibifu wa figo wanashauriwa kuchagua mkate mweupe badala ya aina za nafaka. Unaona, mkate wa ngano isiyokobolewa (brown bread) huwa una mkusanyiko mkubwa wa potasiamu na fosforasi, na kadiri mkusanyiko wa pumba na nafaka unavyozidi kuwa mkubwa, ndivyo mkusanyiko wake wa virutubisho hivi viwili(potasiam na fosforasi) unavyoongezeka.
Kwa mfano, gramu 30 za mkate wa ngano isiyokobolewa zitaupa
mwili wako mg 69 za potasiamu na takribani mg 57 za fosforasi. Kwa upande
mwingine, kipande kimoja cha mkate mweupe kitakupatia tu miligramu 28 za
potasiamu na fosforasi. Kumbuka tu kwamba mikate mingi iliyochakatwa na bidhaa
za mkate zilizowekwa kwenye vifurushi, iwe ngano ni isiyokobolewa, nyeupe au
kahawia, pia huwa na viwango vya juu sana vya sodiamu.
Inapendekezwa sana kuchagua mikate yako baada ya kulinganisha na kuchunguza lebo ya aina kadhaa ya lishe. Hakikisha umechagua aina ambayo ina sodiamu kidogo, na ni muhimu pia kupunguza matumizi ya mikate kwa kadri iwezekanavyo.
5. Mchele Wa Kahawia
Mchele wa kahawia ni sawa sawa tu na mkate wa ngano isiyokobolewa (brown bread) na bidhaa nyinginezo, kwani pia mchele wa kahawia ni nafaka nzima na hivyo basi, una msongamano mkubwa wa potasiamu na fosforasi ikilinganishwa na mchele mweupe. Kwa mfano, kikombe kimoja cha wali wa kahawia uliopikwa kitakupatia mg 154 ya potasiamu na mg 150 ya fosforasi. Kwa upande mwingine, kikombe kimoja cha mchele mweupe uliopikwa kitakupatia tu miligramu 54 za potasiamu na miligramu 69 za fosforasi.
Unaweza kuongeza wali wa kahawia kwenye mlo wako
wakati unapokuwa na tatizo la figo ili mradi tu uweze kudhibiti ukubwa wa
sehemu yako na kula mara kwa mara kwa kulinganisha uwiano sawa na vyakula
vingine vyenye fosforasi na potasiamu kidogo. Inapendekezwa sana kuchagua
nafaka zenye fosforasi kidongo, kama vile Bulgar, nafaka zinazofanana na ngano
(Buckwheat), na shayiri ni njia mbadala salama zaidi za lishe bora ya figo.
6. Ndizi
Ndizi ni maarufu kwa kuwa na wingi wa potasiamu.
Ingawa kwa kawaida huwa ina viwango kidogo vya sodiamu, ndizi moja yenye ukubwa
wa wastani itakupa miligramu 422 za potasiamu kwa njia ya kutisha. Kama una
tabia ya kutumia zaidi ya ndizi mbili kwa siku, inaweza kuwa vigumu sana
kudumisha matumizi yako ya kila siku ya potasiamu chini ya mg 2000.
Ikiwa unapenda kula matunda katika ukanda wa tropiki,
kumbuka kwamba karibia aina zote zimejaa viwango vya juu vya potasiamu. Walakini,
mananasi yana mkusanyiko mdogo wa
potasiamu ikilinganishwa na matunda mengine ya yanayo kuwa katika ukanda wa tropiki.
7. Bidhaa Za Maziwa
Bidhaa za maziwa ni sehemu muhimu ya lishe yenye afya na yenye uwiano sawa kwa sababu huwa ina wingi wa virutubisho vingi na vitamini kadhaa. Hata hivyo, bidhaa za maziwa pia zina wingi wa potasiamu, fosforasi na protini nyingi, ambayo huwafanya kuwa kiungo cha hatari kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na figo.
Wakia (ounces)
8 za maziwa hutoa miligramu 222 za fosforasi na miligramu 349 za potasiamu
kwa njia ya kutisha. Ulaji wa mara kwa mara wa bidhaa kadhaa za maziwa pamoja
na vyakula vingine vyenye fosforasi nyingi zinaweza kuwa hatari kwa afya ya mifupa
kwa wagonjwa walio na magonjwa ya figo. Hii inakuja kwa mshangao kidogo kwa
sababu maudhui ya kalsiamu katika bidhaa za maziwa, hasa maziwa mgando,
inashauriwa sana kuimarisha misuli na muundo wa mfupa.
Utafiti unaonyesha kuwa wakati figo zinapougua au zikiwa zinakabiliwa na uharibifu, matumizi ya kupita kiasi ya fosforasi yatasababisha mkusanyiko wa fosforasi ndani ya mkondo wa damu. Hii itasababisha muundo wa mifupa kuwa dhaifu na myembamba kupita kiasi kadiri muda unavyopita, ambayo itakuweka kwenye hatari kubwa ya kuteseka, kuteguka au kuvunjika kwa mfupa.
Bidhaa za maziwa pia huwa na protini nyingi, kwa
mfano, wakia (ounces) 8 za maziwa yote huwa na wingi wa takribani gramu 8 za
protini. Wagonjwa walio na ugonjwa wa figo wanapaswa kuchukua hatua za
kupunguza matumizi yao ya maziwa ili kuzuia mrundikano mwingi wa taka za
protini kwenye mkondo wa damu.
Badala ya maziwa, unaweza kuchagua mbadala salama zaidi ambao una wingi wa viwango vya chini zaidi vya protini, fosforasi na potasiamu ikilinganishwa na maziwa ya ng'ombe na bidhaa za maziwa. Kwa mfano, maziwa ya mchele na maziwa ya almond ni mbadala mzuri wa maziwa ya ng’ombe kwa wagonjwa wa figo.
8. Machungwa Na Juisi Ya Machungwa
Hata hivyo, chungwa
na juisi fresh ya chungwa iliyokamuliwa ni chanzo mojawapo cha wingi nwa
vitamin C, ladha yake ya citric pia huwa ina kiwango kikubwa cha potasiamu.
Chungwa moja kubwa linaweza kukupa miligramu 333 za potasiamu. Lakini juisi ya
machungwa huwa na mkusanyiko mkubwa zaidi, kwa mfano, wakia(ounces) 8 za juisi
ya machungwa zitaupa mwili wako miligramu 473 za potasiamu.
Zingatia sana wingi hatari huu wa potasiamu, ni bora kuepuka machungwa na juisi ya machungwa, na ikiwezekana, yaondoe kabisa kwenye mlo wako, na badala yake chagua aina nzuri za matunda zenye potasiam kidogo kama vile apple, Crannberry, na Zabibu.
9. Nyama
Kuna utafiti mwingi unaoanzisha uhusiano wa moja kwa moja kati ya ulaji wa nyama iliyosindikwa, na sababu za hatari za magonjwa sugu. Nyama zilizosindikwa huchukuliwa kuwa moja ya vyakula vikuu vya lishe kwa sababu huhifadhi viwango vya juu vya kutisha.
Kimsingi, ni nyama zilizowekwa kwenye makopo,
zilizobanikwa, au zilizotiwa chumvi, kwa mfano sausage, bacon, pepperoni, jerky
na kitimoto. Nyama iliyosindikwa huwa imejaa chumvi nyingi hatari, ambayo
huongezwa ili kuboresha ladha yake na kuhifadhi ladha iweze kudumu kwa muda
mrefu. Zaidi ya hayo, nyama hizi pia hubeba msongamano mkubwa wa protini, na
ikiwa daktari wako amekushauri upunguze matumizi yako ya protini, ulaji wa
nyama zilizosindikwa huwa hazifai tena kwako.
Ikiwa mlo wako ni wa nyama nyingi kupita kiasi, basi
utapata changamoto kubwa ya kuwa na wingi wa sodiamu chini ya miligramu 2000,
pamoja na kudhibiti kama ipasavyo matumizi yako ya protini.
Pia fungua hapa: Zijue Sababu Za Ugonjwa Sugu Wa Figo, Dalili Zake, Madhara Yake Na Tiba Zake
Makala yetu inaishia hapa mpendwa msomaji, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.
Unahitaji Huduma? Basi, tupigie kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu Sana!
Comments
Post a Comment