Fahamu Sababu Zinazomfanya Mwanamke Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa?
Viwango vya wanawake vya hamu ya tendo la ndoa hupungua kadiri wanavyozidi kukua. Ni kawaida viwango vya juu na vya chini kutokea pamoja katika mwanzo au mwisho wa mahusiano. Au viwango hivi vinaweza kutokea kwa mabadiliko makubwa ya maisha kama vile ujauzito, kukoma hedhi au ugonjwa. Dawa zingine zinazotumiwa kwa ajili ya kutibu magonjwa fulani zinazoathiri hisia pia zinaweza kusababisha kushuka kwa hamu ya tedno la ndoa kwa mwanamke.
Ikiwa kama hali ya kukosa hamu ya tendo la ndoa
inaendelea au inatoweka tena inarudia, na kusababisha shida zako kibinafsi, basi
ongea na mtaalamu wako wa afya. Unaweza kuwa na ugonjwa unaoweza kutibika
unaoitwa ugonjwa wa kukosa hamu au hisia ya tendo la ndoa.
Je, Dalili Zake Ni Nini?
Na hata kama hamu yako ya tendo la ndoa iko chini
sana kuliko ilivyokuwa hapo awali, bado uhusiano wako unaweza kuwa na nguvu. Nipende
kuema hivi: Hakuna kiwango kinachoweza kufafanua upungufu wa hisia au hamu ya
tendo la ndoa kwa mwanamke. Ni hali inayotofautiana.
Dalili za kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake ni pamoja na:
- Kufurahia kidogo au kutokufurahia kabisa aina yoyote ya shughuli za ngono, ikiwa ni pamoja na kupiga punyeto.
- Ni mara chache tu unaweza kuwa na hamu ya tendo la ndoa au kukosa kabisa.
- Kuwa na huzuni au mawazo sana kutokana na kukosa hamu ya tendo la ndoa,
Je, Vyanzo Vyake Ni Nini?
Hamu ya tendo la ndoa inategemeana na mchanganyiko
wa mambo mengi yanayoathiri urafiki wako na mwenza wako. Sababu hizi ni pamoja
na:
- Ustawi wa kimwili na kihisia.
- Uzoefu
- Imani
- Uhusiano wako sasa
- Mitindo ya maisha,
Ikiwa una changamoto katika mojawapo ya maeneo haya, inaweza kuathiri uwezo wa hamu yako ya tendo la ndoa.
Sababu Za Kimwili
Magonjwa mbalimbali, mabadiliko ya mwili pamoja na madawa
vinaweza kusababisha hisia au hamu ya tendo la ndoa kuwa kidogo, ikiwa, pamoja
na:
- Matatizo Ya Uzazi: Ikiwa unapata maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa, au huwezi kufika kileleni, inaweza kupunguza hisia au hamu yako ya tendo la ndoa.
- Uchovu Wa Mwili: Uchovu unaotokana na kubeba watoto wachanga au wazazi wanaozeeka unaweza kuchangia kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa. Uchovu kutokana na ugonjwa au upasuaji pia unaweza kuwa ni chanzo.
Mabadiliko Ya Homoni
Mabadiliko katika viwango vyako vya homoni yanaweza
kubadilisha hamu yako ya tendo la ndoa. Hii inaweza kutokea wakati:
- Kukoma Hedhi: Kiwango cha homoni ya estrojeni hupungua wakati wa kukoma hedhi. Hii inaweza kukufanya usivutiwe sana kushiriki tendo la ndoa na kusababisha uke mkavu, na kusababisha kushiriki tendo la ndoa huku unahisi maumivu makali au usumbufu. Wanawake wengi bado wanaridhisha wanaposhiriki tendo la ndoa wakati wa kukoma hedhi na baada ya hapo. Lakini wengine wanakosa hamu ya tendo la ndoa kabisa na wanashindwa kuridhisha waume zao wakati wa mabadiliko haya ya homoni.
- Kunyonyesha Au Ujauzito: Homoni hubadirika tu wakati wa ujauzito, na baada ya kupata mtoto na wakati wa kunyonyesha inaweza kupunguza raha wakati unaposhiriki tendo la ndoa. Uchovu na mabadiliko vinaweza kubadiri umbo au sura ya mwili vinaweza kuathiri hamu ya tendo la ndoa. Vivyo hivyo ule msukumo wa ujauzito au mimba inapoingia.
Matatizo Ya Kisaikolojia
Hali yako ya akili inaweza kuathiri hisia zako. Sababu za kisaikolojia za hisia kidogo za tendo la ndoa ni pamoja na:
- Matatizo ya afya ya akili kama vile wasiwasi au msongo wa mawazo
- Msongo wa mawazo unaohusiana na mambo kama vile fedha au kazi
- Muonekano mbaya wa mwili
- Kutokujithamini
Masuala Ya Mahusiano
Kwa watu wengi, hisia zinapokuwa karibu, ni ufunguo wa kuwa karibu na mwenza wako. Kwa hivyo matatizo katika uhusiano wako yanaweza kuwa sababu kuu ya kukosa hisia au hamu ya tedno la ndoa. Mara nyingi, ile hali ya kutokupata raha yoyote unaposhiriki tendo la ndoa, ni matokeo ya masuala yanayoendelea kama vile:
- Kutokuwa na mahusiano mazuri na mwenza wako
- Migogoro au ugomvi ambao haujatulia,
- Mawasiliano duni unapohitaji kushiriki tendo la ndoa,
- Masuala ya uaminifu
- Wasiwasi juu ya uwezo wa mpenzi wako kushiriki tendo la ndoa,
- Kutokuwa na usiri wa kutosha,
Je, Nini Suluhisho Lake Hasa Kwa Wanawake?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri zenye uwezo
mkubwa wa kuondoa vyanzo vya kukosa hisia wakati wa tendo la ndoa, nazo ni
VITAMAKA, FRESH HERB na NEOTONIC.
Nipende kuishia hapa, niwakaribishe katika kipindi cha maswali na maoni yenu, karibuni sana. Pia unaweza kutuma namba yako ya WhatsAp ili tuweze kukuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.
Je, Unahitaji Huduma? Basi, tupigie: 0768 559
670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment