Mambo 4 Yanayosababisha Kutokwa Na Uchafu Ukeni Wenye Rangi Ya Kahawia
Hauko kwenye kipindi chako cha hedhi, lakini unaona rangi kidogo kwenye chupi yako. Je, hiyo ni damu ya hedhi? Je, ni uchafu ukeni? Je, ni uchafu pamoja na damu?
Je, Kutokwa Na Uchafu Wa Kahawia Ni Kawaida?
Wakati damu inapochanganyikana na ute ute ukeni,
matokeo yake ni kutokwa uchafu wenye rangi ya kahawia. Wakati mwingine, hii ni
ishara tu kwamba kipindi chako kimefika mwisho.
"Uchafu wa kahawia wa kawaida hutokea mwishoni mwa mzunguko wako wa hedhi," "Kunaposalia damu kidogo nyuma wakati kipindi cha hedhi kinapoelekea kukoma, mara nyingi mwili huivundisha na bakteria na hivyo hushindwa kutoka." Wakati mwingine, ingawa, baadhi ya uchafu huo huonekana nje ukeni mwako au kwenye nguo yako ya ndani, inapoelekea mwisho wa kipindi chako cha hedhi, au hata siku moja au mbili baada ya kumaliza.
Lakini kuna sababu zingine zinazopelekea kutokwa na damu yenye rangi ya kahawia, nazo ni pamoja na:
- Mabadiliko Yanayohusiana Na Kukoma Kwa Hedhi
Unapokuwa katika umri wa kukoma hedhi, kupungua kwa homoni ya estrojeni kunaweza kusababisha kuta za uke wako kuwa nyembamba tena ndogo, hali inayojulikana kama uke kuwa mkavu. Mishipa yako ya damu husinyaa, na unaweza kupatwa na hali ya kutokwa na damu ukeni.
Ikiwa umeshakoma hedhi au unakaribia kukoma hedhi na unaanza kutokwa na uchafu wa kahawia, basi fika katika kituo cha afya, muone daktari wa wanawake juu ya matatizo ya uzazi atakusaidia kuhakikisha kuwa ni uchafu unaotoka ukeni. "Kwa wagonjwa waliokoma hedhi, tunataka kila mara kuhakikisha kuwa damu haitoki kwenye tumbo la uzazi, jambo ambalo linaweza kuashiria masuala mengine.
2. Baktria Ukeni
Maambukizi haya ya kawaida kwa kawaida huambatana na kutokwa na uteute wenye rangi ya kijivu, lakini kwa watu wengine, unaweza kuonekana kuwa wenye rangi ya kahawia, haswa baada ya kukauka kwenye nguo ya ndani.
Kutokwa na uchafu kutokana na
bakteria ukeni, husababishwa na mvurugiko wa bakteria ukeni, na kwa kawaida
huonekana zaidi pale unapokaribia kuingia hedhi au baada ya kumaliza kushiriki
tendo la ndao. Karibia kila mara ute ute au uchafu huu huambatana na harufu mbaya
kama shombo la samaki, kiashiria muhimu kwamba kuna bakteria huko chini.
"Pale bakteria wanaosababisha
bakteria ukeni wanapochanganyikana na damu, au shahawa, huanza kushamiri, hali
ambayo husababisha watoe harufu. Kama unahisi kuwa una tatizo hili, wahi fika
hospitali kafanye vipimo ili uanze kutibu haraka ugonjwa huu.
3. Malengelenge(Trichomoniasis)
Damu inayokuwa kwenye mchanganyiko wa uchafu unaootoka ukeni inaweza pia kuwa matokeo ya maambukizi ya malengelenge (trichomoniasis), yaani maambukizi ya zinaa yanayosababishwa na vimelea hai kwenye uke wako na/au mrija wa mkojo. Kama vile mkwaruzo kwenye ngozi yako unavyoweza kukufanya utokwe na damu kidogo, vivyo hivyo, pia, vimelea hivi vinaweza kuzidisha mikwaruzo kwenye mfumo wa uzazi wako.
"Kuna muwasho ambao hutokea ndani yake, na wakati mwingine kuwashwa huko husababisha matone ya damu. Wakati mwingine uchafu huo unapotoka nje, huwa ni wenye rangi ya kahawia.
Maambukizi ya malengelenge (trichomoniasis)
pia yanaweza kusababisha kutokwa na uchafu wenye rangi nyeupe, njano au ukijani
ambao ni mwepesi au wenye mapovu, tena wenye harufu mbaya. Fika hospitali
haraka sana ukafanye vipimo na pia matibabu.
4. Matone Ya Damu
Hata tone moja la damu linapotoka kwenye shingo ya uzazi au mfuko wa uzazi linaweza kuchanganyikana na uteute ukeni ili kutengeneza uchafu wenye rangi ya kahawia. Na ingawa inaonekana ya kutisha, isikutishe hofu kubwa kwasababu inatibika.
"Shingo ya kizazi huwa ni dhaifu sana, na wakati mwingine inaweza kutoa damu kidogo kidogo. "Matone ya damu damu yanaweza kutoka hata kabla ya kuingia hedhini, ni kawaida kwa wanawake wenye umri mdogo kupata hedhi hivi karibuni. Lakini inaweza kutokea kwa mtu yeyote.
Katika hali nyingine, damu isiyo ya kawaida inaweza kuashiria tatizo la afya, hivyo ikiwa huanza kutokea mara kwa mara (na hasa ikiwa inaambatana na maumivu), ni wakati wa kwenda hospitali au kituo cha afya kwenda kupima kizazi chako.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri zenye uwezo
mkubwa wa kuondoa tatizo la kutokwa na damu au uchafu wenye rangi ya kahawia,
nazo ni PERFECT POWDER, CARD HERB na MULTICURE POWDER.
Ndugu msomaji naomba niishie hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako. Pia unaweza kutuma namba yako ya whatsAp ili tuweze kukuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.
Unahitaji Huduma? Tupigie: 0768 559 670/0712181626,
Arusha-Mbauda,
Karibuni sana!
Comments
Post a Comment