Mambo 6 Yanayomfanya Mwanamke Kuhisi Maumivu Ya Tumbo Wakati Wa Hedhi Au Baada Ya Kutoka Hedhini
Wanawake wengi huhisi maumivu ya tumbo kabla
au wanapokuwa hedhini. Lakini inaweza pia mwanamke akahisi maumivu ya tumbo
anapokuwa hedhini. Maumivu haya mara nyingi huwa sio makali sana. Hata hivyo,
ni muhimu kwamba unayafuatilia, hasa ikiwa kama yanakaa kwa muda mrefu. Maumivu
ya tumbo wakati wa hedhi inaweza kuwa ni dalili ya magonjwa mbalimbali.
Endelea kusoma Makala hii ujifunze dalili, visababishi, Pamoja na matibabu ya kukosa hedhi au kutokwa na damu ya hedhi nyingi kwa muda mrefu.
Je, Nini Visababishi Vyake?
Wakati mwingine maumivu ya tumbo baada ya hedhi huwa sio makali mno. Lakini kama una maumivu makali endelevu yanayodumu muda mrefu kuliko mzunguko wako wa hedhi, inaweza kuwa ishara kwamba una magonjwa kwenye tumbo lako la uzazi(uterus).
Hapa nitakuelekeza visababishi vya maumivu ya tumbo unapotoka hedhini:
1. Endometriosis
Endometriosis ni ugonjwa ambao hutoea pale seli zinazofanana na ukuta laini wa mji wa mimba(uterus) zinapoota nje ya mji wa mimba. Ugonjwa huu unaweza kusababisha maumivu makali kabla au wakati wa hedhi au baada ya hedhi.
Maumivu yanaweza
kuambatana na uvimbe Pamoja na maumivu ya nyonga. Maumivu yanaweza kuwa makali
na yanaweza kutokea wakati unaposhiriki tendo la ndoa au unapotoa haja kubwa au
unapokojoa. Maumivu haya endelevu unaweza kuyahisi kiunoni mwako.
Dalili za ugonjwa wa
endometriosis ni Pamoja na:
- Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa
- Maumivu kwenye njia ya haja kubwa wakati unapojisaidia au kukojoa
- Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi au katikati ya hedhi
- Kushindwa kupata ujauzito(ugumba)
- Kuhisi uchovu
- Kuhara au kukosa choo
- Tumbo kuunguruma
- Kuhisi kichefuchefu
- Kuhisi maumivu kabla ya hedhi au wakati wa hedhi au baada ya hedhi huku yakiambatana na maumivu ya kiuno na tumbo la chini.
Adenomyosis ni
ugonjwa unaosababishwa na kuota kwa tishu zisizokuwa za kawaida. Badala ya
kujengeka kwenye ukuta wat umbo la uzazi, hizi tishu huota kwenye ukuta wa
msuli wat umbo la uzazi(uterus). Dalili zake huwa ni Pamoja na:
- Kutokwa na damu nyingi ya hedhi tena kwa muda mrefu
- Kuhisi maumivu makali sana wakati unapokuwa hedhini
- Kuhisi maumivu makali wakati unaposhiriki tendo la ndoa
- Damu kuwa na mabonge unapokuwa hedhini
- Kuhisi maumivu makali maeneo ya tumbo la chini
- Maumivu maeneo ya tumbo la chini au kwenye nyonga
- Kutokwa na uchafu mwingi ukeni wenye harufu na rangi mbaya
- Kutokwa na damu ukeni nisiyo ya kawaida mfano, yenye utelezi
- Kuhisi homa au mafua
- Kuhisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kuhisi vibaya wakati unapoenda haja kubwa.
- Maumivu ya tumbo yenye kuchoma
- Mzunguko wa hedhi kubadirika
- Kutokwa na damu ya hedhi kwa muda mrefu
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara au kushindwa kukojoa
- Kuhisi mgandamizo au maumivu
- Kuhisi kukosa choo
- Kukosa ujauzito(ugumba)
- Mgongo au miguu kuuma.
Kumbuka uvimbe wa fibroid unatibiwa na dawa zetu za asili kwa urahisi mno na unapata ujauzito.
5. Vivimbe Kwenye Vifuko Vya Mayai(Ovarian Cysts)
Vivimbe ambavyo hujengekea ndani ya vifuko vya mayai vinaweza kusababisha kutokwa na damu ya hedhi kidogo na tumbo kuuma sana. Vivimbe vingi kwenye vifuko vya mayai hupotea vyenyewe bila matibabu. Hata hivyo, vivimbe vikubwa kwenye vifuko vya mayai vinaweza kusababisha maumivu ya nyonga kwenye maneo ya tumbo la chini.
Tumbo lako linaweza kujaa, ukahisi kama umeshiba au muda mwingine kuunguruma mara kwa mara na kujamba. Kwahi fika hospitali haraka sana ikiwa kama unahisi maumivu makali ya ghafla au homa au kutapika.
Vivimbe kwenye vifuko vya mayai hutibiwa kwa dawa za asili na kuondoa vyanzo vyake.
6. Mimba Kutunga Nje Ya Kizazi
Mimba kutunga nje ya kizazi hutokea wakati yai lililorutubishwa linapojipachika lenyewe nje ya mji wa mimba.
Dalili za mimba kutunga nje ya kizazi zinaweza kuanza kama mimba ya kawaida kabisa. Hata hivyo, unaweza kuendelea kupata dalili zifuatazo:
- Kutokwa na damu isiyo ya kawaida
- Kuhisi maumivu kwenye tumbo la chini au nyonga
- Maumivu kupita kama kisu kinachoma
- Maumivu begani
NUKUU: Damu nyingi huja kuanza kutoka kama
mrija wa uzazi ukipasuka. Hali hii inaweza kuambatana na damu nyepesi, kukosa
pumuzi na mshituko wa moyo. Unapoona hivyo wahi kupata matibabu haraka.
Hivyo, makala yetu inaishia hapa ndugu msomaji, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.
Comments
Post a Comment