Dalili 4 Za Uvimbe Kwenye mashavu Ya Uke.

Na ieleweke kwamba, tezi za Bartholin huwa ziko kila upande katika sehemu ya uwazi wa uke. Tezi hizi huwa zina kazi ya kutengeneza uteute ambao husaidia kulainisha uke.

Wakati mwingine sehemu za uwazi zinazokuwa kwenye tezi hizi huziba, na kusababisha uteute au majimaji kukusanyikana kwenye tezi. Matokeo yake utaona uvimbe usiokuwa na maumivu ambao kitaalamu unaitwa, “Bartholin’cyst”. Kama uteute au majimaji yanayokuwa kwenye uvimbe huo yatakuwa na maambukizi, basi kutazidi kukusanyikana tena usaha unaokuwa umezungukwa na tishu zilizovimba.

NUKUU: Hali ya mkusanyiko wa usaha huwa ni ya kawaida. Lakini matibabu ya tatizo hili hutegemeana na ukubwa wa uvimbe wenyewe, jinsi uvimbe unavyokuwa na maumivu na endapo kama uvimbe una maambukizi.           

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Ikiwa kama utakuwa na uvimbe mdogo juu ya tatizo hili, unaweza ukashindwa kuutambua vizuri. Lakini kama uvimbe utazidi kuwa mkubwa, utaanza kuhisi kitu kama bonge fulani karibu na mlango wa uke. Ingawa uvimbe mara nyingi huwa hauna maumivu, basi unaweza ukawa mgumu. Madhara kama rangi ya kahawia hivi kwenye uvimbe yanaweza kujitokeza kwa siku kadhaa. Kama uvimbe utakuwa na maambukizi, basi utaanza kuona dalili zifuatazo:

  • Bonge sehemu za uwazi wa uke gumu lenye maumivu
  • Kutojisikia raha hasa wakati unapokuwa unatembea au wakati unakaa
  • Kuhisi maumivu makali wakati unapofanya tendo la ndoa
  • Kuhisi homa

NUKUU: Uvimbe huu sehemu ya uke mara nyingi hujitokeza sehemu moja tu ya mlango wa uke. Uonapo hali kama hii tafadhali napenda kukushauri ufike hospitali mapema ili kuweza kupata vipimo.

Je, Uvimbe Huu Husababishwa Na Nini?

Inaonekana kwamba, wataalamu wanaamini kuwa chanzo cha uvimbe huu huwa ni mkusanyiko wa uteute au majimaji kwenye tezi ya Bartholin. Uteute unaweza kukusanyika wakati njia ya uwazi ya tezi inapoziba kutokana na maambukizi au ajari.

Uvimbe huu unaweza ukaathirika na ukajaa usaha. Baadhi ya bakteria wanaweza kusababisha maambukizi, hasa Escherichia coli(E.coli), pamoja na bakteria ambao husababisha maambukizi ya zinaa kama vile kisonono(Gonorrhea) pamoja na pangusa(Chlamydia).

NUKUU: Uvimbe huu au mkusanyiko wa usaha unaweza ukajirudia tena na utahitaji matibabu. Yafaa sana mwanamke kufanya usafi sehemu zake za uke, au kutumia kondom wakati anapokutana na mpenzi wake ili kuzuia maambukizi ya bakteria wabaya.

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya uvimbe katika mfumo wa uzazi wa mwanamke.

Hivyo basi, huu ndio mwisho wa makala yetu, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako. Pia unaweza kutuma namba yako ya WhatsAp ili tuweze kukuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.

Je, unahitaji huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda.

Karibu sana!

 

Comments

Popular posts from this blog

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa