Fahamu Dalili 5 Za Ugonjwa Wa PID
Dalili za ugonjwa wa PID ni rahisi kuupata mara tu unapofanya uchunguzi wa vipimo. Zuia matatizo makubwa ya kiafya na kushindwa kupata ujauzito (ugumba) kwa kushauriana na daktari wako wa magonjwa ya wanawake mara tu unapotambua dalili hizo za PID.
Ugonjwa wa PID ni neno linalotumika kuelezea
maambukizi ya viungo vyako vya uzazi yanayosababishwa na muwasho wa bakteria.
PID ni maambukizi ya kawaida, ambayo yanazidi kuwapata wanawake kwa kiwango
kikubwa sana.
Maambukizi katika viungo vya uzazi (PID) yakiachwa bila kutibiwa, yanaweza kusababisha matatizo makubwa ya uzazi—kwa hakika na ndiyo sababu kuu ya ugumba kwa wanawake. PID inaweza kuwa ni matokeo ya matatizo yatokanayo na magonjwa kadhaa ya zinaa, hivyo tafuta matibabu mara tu unapoona mojawapo ya dalili zifuatazo za ugonjwa wa PID:
1. Maumivu Ya Nyonga Au Tumbo La Chini
Wakati viungo vyako vya uzazi vinakabiliwa na bakteria zinazoletwa na ugonjwa wa zinaa, uvimbe hutokea ambayo unaweza kusababisha maumivu makali. Maumivu fulani ya sehemu ya chini ya tumbo ni ya kawaida wakati wa mzunguko wako wa hedhi, lakini maumivu yanayosababishwa na PID ni makali zaidi na yanaonekana zaidi kuliko kuumwa kwa kawaida wakati wa hedhi.
Ikiwa unapata maumivu makali ya
tumbo la chini au nyonga, wasiliana na daktari wako wa uzazi mara moja hasa
ikiwa hauko kwenye kipindi chako cha hedhi.
2. Kutokwa Na Uchafu Ukeni Wenye Harufu Mbaya
Kiasi kidogo cha uteute mweupe ukeni ni wa kawaida mno, lakini ikiwa unaona uchafu mwingi wenye harufu isiyo ya kawaida, inaweza kuwa ni dalili ya ugonjwa wa PID. Huenda usipate maumivu ya nyonga kama maambukizi bado hayajafika kwenye tumbo lako la uzazi uterus yako kupitia kwenye shingo ya yako ya kizazi.
Kuzifahamu dalili za ugonjwa wa PID
kabla haujafika kwenye viungo vyako vya uzazi ndiyo njia bora ya kuzuia ugumba
wa kudumu. Ikiwa unaona uchafu mwingi unatoka ukeni huku ukiambatana na harufu
mbaya, basi wasiliana na daktari wako wa uzazi.
3. Maumivu Wakati Unapokojoa
Kuhisi maumivu wakati unapokojoa mara nyingi huwa ni dalili ya UTI au maambukizi kwenye kibofu cha mkojo. Hali hii ikiachwa bila kutibiwa, maambukizi ya kwenye njia ya mkojo au kibofu cha mkojo yanaweza kuwa mabaya zaidi na yanaweza kusafiri hadi kwenye tumbo la uzazi (uterus) au vifuko vya mayai(ovaries), na kusababisha ugonjwa wa PID. Ikiwa unakabiliwa na maumivu wakati wa kukojoa, daktari wako wa uzazi anaweza kupima mkojo wako ili kuona maambukizi. Hakikisha unawasiliana na daktari wako anayehusiana na maambukizi haya.
Maumivu makali wakati wa kukojoa ni
dalili ya kawaida ya PID, na huenda ikahitaji kutibiwa kwa dawa za asili zenye
nguvu zaidi.
4. Homa Kali Zaidi
Homa kali zaidi ya digrii 101 ni ishara kwamba mwili wako unapigana na maambukizi. Ikiwa homa yako hudumu zaidi ya siku chache, basi muone daktari wako ili kutathmini dalili zako. Homa kali haiashirii PID kila wakati. Hata hivyo, ikiwa homa kali inaambatana na maumivu ya nyonga au kutokwa na uchafu ukeni, ni ishara kubwa kwamba unakabiliwa na dalili za ugonjwa wa PID.
Tafadhali kumbuka kuwa homa yoyote
ambayo hudumu zaidi ya siku mbili inahitaji tahadhari ya haraka kutoka kwa
mtaalamu wa matibabu.
5. Maumivu Makali Wakati Unaposhiriki Tendo La Ndoa
Ikiwa unapata maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa, inaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa PID. Inawezekana pia kuwa ukawa na maambukizi ya UTI au fangasi ukeni, au eneo hilo limechubuliwa na mambo ya ngono ya mara kwa mara au ya nguvu. Maambukizi yanaweza kusababisha ugonjwa wa PID ikiwa haujatibiwa.
Ikiwa unapata ugonjwa wa PID mapema, unaweza kutibiwa kwa mzunguko rahisi kabisa wa dawa za asili(antibiotics). Usiruhusu dalili zako zitokeze bila kufanyiwa vipimo, au ugonjwa wako wa PID usikufanye ukawa mgumba na kusababisha matatizo ya kiafya ya muda mrefu. Unapogundua mojawapo ya dalili hizi za kawaida za PID, fika hospitali haraka iwezekanavyo.
Hivyo basi, makala yetu inaishia hapa. Nipende kukaribisha kipindi cha maswali na maoni yako.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tunazo dawa za asili zenye uwezo mkubwa wa antibiotic. Hivyo unaweza kuwasiliana nasi. Pia unaweza kutuma namba yako ya WhatsAp tukakuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.
Je, Unahitaji Huduma?
Tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment