Fahamu Dalili Za Maambukizi Ya Zinaa Aina Ya Malengelenge(Trichomoniasis) Kwa Mwanume Na Mwanamke.
Malengelenge au Trichomoniasis ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya ngono kama magonjwa mengine ya zinaa. Maambukizi ya ugonjwa huu yanaweza kutokea hata kwa mtu asiyekuwa na dalili za maambukizi ya ugonjwa huu. Wanawake hupata maambukizi ya ugonjwa wa Malengelenge kutoka kwa wanaume, na wanaume pia huupata kutoka kwa wanawake walioambukizwa. Matumizi yako ndo huzuia maambukizi, lakini sio salama sana japo yanasisitizwa kila mara.
NUKUU: Umbile la vimelea vyaTrichomonas vaginalis ni sawa na chembe chembe moja ya damu nyeupe kwa upana, ingawa wakati mwingine ukubwa unaweza kutofautiana kulingana na mazingira. Kuwepo kwa umbile kama mikono kwa nje kwenye kimelea hicho inayojulikana kama flagellum, husaidia vimelea hivi kuingia kwenye tishu za mrija wa kupitisha mkojo pamoja na tupu ya mwanamke na hivyo kuharibu seli aina ya epithelium na kusababisha vidonda katika tishu hizo. Hii ndiyo sababu, watu wanaopata ugonjwa huu huwa kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa Ukimwi (HIV) na magonjwa mengineyo ya zinaa.
Je, Mgonjwa Huwa Ana Dalili Gani?
Watu wengi wenye ugonjwa huu huwa hawaonyeshi dalili. Lakini dalili zinapotokea, nazo kwa kawaida huwa kama ifuatavyo;
1. Kwa Wanawake
· Mwasho ama kuhisi kuwa kama moto sehemu za siri
· Mashavu ya uke kuwa mekundu
· Kutokwa na uchafu wa njano wenye harufu mbaya
· Kutokwa na damu sehemu ya uke
· Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa mara kwa mara
· Maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa
· Maumivu ya tumbo
NUKUU: Mwanamke anaweza pia kuona dalili hizo hapo juu kuwa mbaya zaidi baada ya kutoka hedhini, pia dalili hizo zinaweza kuchanganyikana na maambukizi ya fangasi.
Hivyo
napenda kuwasihi sana kina mama kuwa makini waendapo kupata vipimo ili kubaini ugonjwa
wa fangasi na wa malengelenge, kwani unaweza kuambiwa una fangasi kumbe ni maambukizi
ya malengelenge au unaweza kuambiwa una malengelenge, kumbe ni maambukizi ya fangasi.
Kwa upande wa mwanamke, ugonjwa huu huathiri shingo ya kizazi (cervix), mrija wa mkojo, tupu ya mwanamke, kibofu cha mkojo na tezi zinazojulikana kama Bartholin glands, nk.
1. Kwa Wanaume
Mara nyingi wanaume huwa wanaonyesha dalili, nazo huwa kama ifuatavyo:
· Kutokwa na uchafu kwenye uume
· Maumivu makali wakati wa kukojoa
· Muwasho ndani ya uume
·
Kuhisi
hali ya kuwaka moto baada ya kufika kileleni baada ya tendo la ndoa.
NUKUU: Kwa wanaume vimelea hivi vya Trichomonas vaginalis hupatikana katika sehemu za siri za mwanaume, sehemu ya nje ya mrija wa kupitisha mkojo (anterior urethra), kwenye tezi dume, kwenye mirija ya kuhifadhi na kutoa mbegu za kiume (epididymis) na hata kwenye mbegu zenyewe.
Je, Nini MadharaYa Ugonjwa Huu?
Ugonjwa huu usipotibiwa mapema na ukawa sugu, husambaa na kuingia kwenye via vya uzazi kuanzia mlango wa uzazi (cervix), mfuko wa uzazi(uterus), mirija ya uzazi (fallopian tube), na vifuko vyama yai(ovaries) na kuwa ugonjwa unaoitwa “PID”. Tatizo hili huwaongezea wanawake hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi, lakini pia kwa upande wa wanaume huwaongezea hatari ya kupata saratani ya tezi dume.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James & Ferdinand Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya maambukizi ya ugonjwa wa Trichomoniasis au malengelenge, pande zote mbili kwa mwanaume na mwanamke pia.
Hivyo makala yetu inaishia hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako. Pia unaweza kutuma namba yako ya WhatsAp tukakuungan isha na darasa letu la masomo ya afya.
Je, Unahitaji huduma? Basi tupigie; 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment