Fahamu Mambo 4 Yanayomfanya Mwanamke Kushindwa Kupata Ujauzito.
Ugumba hufafanuliwa kama kujaribu kupata mimba kwa
kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara, bila kinga kwa angalau mwaka mmoja,
lakini bila mafanikio.
Sababu za ugumba kwa wanawake zinaweza kuwa ngumu
kutambulika. Kuna matibabu mengi, kulingana na vyanzo vya ugumba. Lakini wapo wanandoa
wengi wasio na uwezo wataendelea kupata mtoto bila kufanya matibabu.
Je, Dalili Za Ugumba Zinakuwaje?
Dalili kuu ya ugumba ni kutoweza kupata mimba. Mzunguko wa hedhi ambao ni mrefu sana (siku 35 au zaidi), mfupi sana (chini ya siku 21), vipindi vya hedhi kubadilikabadilika au kukosa hedhi kabisa kunaweza kumaanisha kuwa mayai yako hayapevuki. Kunaweza kusiwe na ishara au dalili zingine.
Je, Ni Muda Gani Mwanamke Anapaswa Kufika Hospitali Kuonana Na Daktari?
Wakati unapoanza kutafuta msaada itategemena na umri
wako:
- Hadi kufikia umri wa miaka 35, madaktari wengi wanapendekeza ujaribu kupata mimba kwa angalau mwaka mmoja kabla ya kupima au matibabu.
- Ikiwa uko kati ya miaka 35 na 40, jadili matatizo yako na daktari wako baada ya miezi sita ya kufanya vipimo.
- Ikiwa una umri wa zaidi ya miaka 40, daktari wako anaweza kupendekeza vipimo au matibabu mara moja.
Daktari wako pia anaweza kutaka kuanza vipimo au kutibu mara moja ikiwa wewe au mwenzi wako mnafahamu matatizo ya uzazi, au kama una historia ya hedhi isiyo ya kawaida au yenye maumivu makali yenye uchungu, ugonjwa wa PID, kuharibika kwa mimba mara kwa mara, matibabu ya saratani au endometriosis.
Je, Sababu Ni Nini?
Ili ujauzito utokee, kila hatua ya mchakato wa uzazi wa mwanamke inapaswa kutokea kwa usahihi. Hatua katika mchakato huu ni:
- Moja ya mirija miwili hutoa yai lililokomaa
- Yai huchukuliwa na mrija wa uzazi
- Manii au mbegu huogelea hadi kwenye mlango wa kizazi, hupita kwenye mfuko wa uzazi na kuelekea kwenye mrija wa uzazi kufikia yai kwa ajili ya kulirutubisha.
- Yai lililorutubishwa husafiri chini ya mrija wa uzazi hadi kwenye mfuko wa uzazi (uterus).
- Yai lililorutubishwa hujipachika (implants) ndani ya mfuko wa uzazi (uterus) na kukua.
Mfumo Wa Uzazi Wa Mwanamke
Vifuko vya mayai (Ovaries), mirija ya uzazi, mfuko wa uzazi (uterus), mlango wa uzazi na uke, pia huitwa mfereji wa uke, ndio huunda mfumo wa uzazi wa mwanamke.
Urutubishaji Na Upachikaji Wa Yai
Wakati wa urutubishaji, mbegu za mwanamue na yai huungana kwenye moja ya mirija ya uzazi na kuunda kiini. Kisha kiini husafiri ndani ya mrija wa uzazi ambapo hubadilika na kuwa seli. Mara tu seli hii inapofika kwenye tumbo la uzazi(uterus), huchimba kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi (uterus) mchakato unaoitwa upachikaji.
Katika wanawake, mambo kadhaa yanaweza kuvuruga mchakato huu kwa hatua yoyote. Ugumba wa wanawake husababishwa na moja au zaidi ya sababu zilizo hapa chini.
Matatizo Ya Yai Kushindwa Kupevuka
Kutokupevuka kwa mayai mara kwa mara au kutokupevuka kabisa kwa yai husababisha visa vingi vya ugumba. Matatizo katika udhibiti wa homoni za uzazi katika tezi ya hypothalamus au pituitary au matatizo katika vifuko vya mayai (ovaries) inaweza kusababisha matatizo ya upevushaji.
Ugonjwa wa mvurugiko wa homoni (homornal imbalance) husababisha kutofautiana kwa homoni, ambayo huathiri upevushaji wa mayai. Mvurugiko wa homoni inahusishwa na kunenepa kupita kiasi, kuota nywele au vinyweleo vingi usoni au mwilini, na kutokwa chunusi usoni. Ni chanzo cha ugumba kwa mwanamke.
Homoni mbili zinazozalishwa na tezi
ya pituitary huwajibika katika kuchochea upevushaji wa mayai kila mwezi - homoni
ya kuchochea follicle (FSH) na homoni ya luteinizing (LH). Msongo wa mawazo wa kimwili
au wa kihisia kupita kiasi, uzito wa mwili wa juu sana au wa chini sana, au kunenepa
sana au kukonda sana hivi karibuni kunaweza kuvuruga uzalishwaji wa homoni hizi
na kuathiri upevushaji wa mayai. Vipindi vya hedhi kubadirikabadilika au kukosa
hedhi kabisa ni ishara za kawaida.
- Mayai Kushindwa Kukomaa
Pia huitwa kushindwa kwa yai
kupevuka kabla ya wakati, hii kwa kawaida husababishwa na majibu ya kingamwili
au kwa kukosa mayai mapema kwenye kifuko cha mayai (ovary). Kifuko cha mayai
(Ovary) hakitoi mayai tena, na kinapunguza uzalishaji wa homoni ya estrojeni
kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 40.
- Kiwango Kikubwa Cha Homoni Ya Prolactin
Tezi ya pituitari inaweza kusababisha uzalishaji wa ziada wa homoni ya prolactini (hyperprolactinemia), ambayo hupunguza uzalishaji wa homoni ya estrojeni na inaweza kusababisha ugumba. Hii inaweza pia kusababishwa na madawa unayotumia kwa magonjwa mengine.
Kuharibika Kwa Mirija Ya Uzazi
Mirija ya uzazi iliyoharibika au kuziba huzuia manii kufika kwenye yai au kuzuia njia ya yai lililorutubishwa kuingia kwenye tumbo la uzazi (uterus). Sababu za kuharibika au kuziba kwa mirija ya uzazi zinaweza kuwa kama hizi zifuatazo:
- Ugonjwa wa PID, ambao ni maambukizi kwenye mfuko wa uzazi (uterus) na mirija ya uzazi kutokana na pangusa (chlamydia), kisonono au magonjwa mengine ya zinaa.
- Upasuaji wa awali katika tumbo au fupanyonga, ikiwa ni pamoja na upasuaji wa mimba iliyotunga nje ya kizazi, ambapo yai lililorutubishwa hupandikizwa na kukua mahali pengine mbali na tumbo la uzazi (uterus), mara nyingi huwa ni kwenye mirija ya uzazi.
Endometriosis
Endometriosis hutokea wakati tishu ambazo kwa kawaida huota kwenye tumbo la uzazi hujipachika na kuota katika maeneo mengine. Uotaji wa tishu hizi za ziada kuondolewa kwake kwa njia ya upasuaji, kunaweza kusababisha makovu, ambayo yanaweza kuziba mirija ya uzazi na kuzuia yai na mbegu za mwanaume visiungane.
Endometriosis pia inaweza kuharibu kujipachika kwa yai lililorutubishwa. Hali hiyo pia inaonekana kuathiri uzazi kwa njia zisizo za moja kwa moja, kama vile uharibifu wa manii au yai.
Matatizo Kwenye Tumbo La Uzazi Au Shingo Ya Kizazi
Sababu kadhaa kwenye tumbo la uzazi (uterus) au shingo ya kizazi (cervix) zinaweza kuingilia kujipachika kwa yai au kuongeza hatari ya kuharibika kwa mimba:
· Uvimbe wa fibroid au myomas ni kawaida kwenye tumbo la uzazi (uterus). Baadhi vivimbe hivi vinaweza kuziba mirija ya uzazi au kuingilia kujipachika kwa yai, hivyo kuathiri uwezo wa mwanamke kupata ujauzito. Hata hivyo, wanawake wengi ambao wana uvimbe wa fibroid huwa wajawazito.
· Matatizo ya tumbo la uzazi yaliyopo tangu kuzaliwa, kama vile tumbo la uzazi lenye umbo lisilo la kawaida, linaweza kusababisha matatizo ya kutokupata ujauzito.
· Njia ya mlango wa kizazi kuwa finyu, kunaweza kusababishwa na ulemavu wa kurithi au kuharibika kwa kizazi.
· Wakati mwingine shingo ya kizazi haiwezi kuzarisha kiwango kizuri cha ute ili kuruhusu mbegu za mwanaume kupita kwenye shingo ya kizazi hadi kwenye tumbo la uzazi (uterus).
Je, Nini Suluhisho Lake?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa zenye
uwezo mkubwa wa kutengeneza kizazi na kukupa uwezo wa kupata mimba.
Makala yetu inaishia hapa, nipende kukaribisha kipindi cha maswali na maoni yako, karibu sana.
Je, Unahitaji huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626.
Arusha Mbauda.
Comments
Post a Comment