Mambo 6 Yanayosababisha Kiungulia Kikali

Ugonjwa wa kujaa kwa asidi tumboni ni hali ya kawaida, ambapo asidi hutoka tumboni na  kuvujia kwenye koo la chakula(umio).

Kawaida asidi hutokea kama matokeo ya kikazio cha msuli kinachokuwa chini ya koo la chakula kinapodhoofika.

Ugonjwa huu husababisha dalili kama vile kiungulia pamoja na radha mbaya nyuma ya kinywa. Inaweza ikawa kero ya hapa na pale kwa baadhi ya watu, lakini kwa wengine inaweza kuwa tatizo kubwa la maisha yote.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Ugonjwa wa asidi tumboni unaweza kuleta masumbufu makubwa mno, na dalili zake huwa kama hizi zifuatazo:

·        Kiungulia (hali unayohisi kama kuungua moto kifuani ambayo mara nyingi hutokea baada ya kula). Mbubujiko wa asidi (ambapo asidi ya tumboni hurudi nyuma mpaka kinywani mwako na kusababisha radha mbaya yenye uchungu). 

  • Kupumua hewa mbaya
  • Kuhisi au kuugua
  • Kuhisi maumivu unapomeza au kushindwa kumeza
  • Kuvimbiwa au tumbo kufura.
  • Koo la chakula kuvimba

Je, Vyanzo Vyake Ni Nini?

Ugonjwa wa kujaa kwa asidi tumboni ni hali ya kawaida, ambapo asidi hutoka tumboni na  kuvujia kwenye umio (koo la chakula). 

Kwa kawaida, kikazio hiki cha msuli hufunguka ili kuruhusu chakula kiingie tumboni na hujifunga ili kuzuia asidi tumboni isivuje na kurudi kwenye koo la chakula.

Je, Ni Nani Aliye Katika Hatari Zaidi Ya Ugonjwa Wa Asidi Kwenye Koo La Chakula?

Mambo yafuatayo yanaweza kuongeza hatari yako ya kupata asidi kwenye koo la chakula:

  • Kuwa mnene kupita kiasi au kitambi: hii inaweza kuongeza shinikizo kwenye tumbo lako na kudhoofisha misuli chini ya koo la chakula.
  • kula kiwango kikubwa cha vyakula vyenye mafuta mengi: tumbo huchukua muda mrefu kuondoa asidi ya tumbo baada ya kumeng'enya chakula chenye mafuta mengi na asidi ya ziada inaweza kuvujia  kwenye koo la chakula. 
  • uvutaji sigara, unywaji pombe, kahawa, ulaji wa ugali wa sembe, au vyakula vilivyokobolewa: hivi vinaweza kudhoofisha msuli wa chini ya koo la chakula.
  • Ujauzito: mabadiliko ya muda katika viwango vya homoni na kuongezeka kwa shinikizo kwenye tumbo lako wakati wa ujauzito kunaweza kusababisha asidi kububujika na kurudi kwenye koo la chakula.
  • Madawa fulani ya vidonge: baadhi ya dawa zinaweza kusababisha mbubujiko wa asidi kurudi kwenye koo la chakula au kufanya dalili kuwa mbaya zaidi, ikiwa ni pamoja na vizuizi vya njia ya kalsiamu (hutumika kutibu shinikizo la damu), nitrates (hutumika kutibu angina),
  • Msongo wa mawazo, nk.

Je, Nini Suluhisho Lake?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa mbubujiko wa asidi tumboni. Ukitaka kupata huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626. Pia unaweza kutuma namba yako ya whatsAp tukakuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.

Arusha-Mbauda,

Karibu Sana!

Comments

Popular posts from this blog

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa