Mitindo Mibaya Ya Maisha Yaweza Kuwa Chanzo Cha Matatizo Kwenye Mfumo Wa Uzazi Wa Mwanamke

Uchaguzi wa mitindo mibaya ya Maisha inaweza kuathiri uwezo wa mwanamke kupata ujauzito. Fikiria baadhi ya hatua rahisi ikiwa unatarajia kupata mimba.

Kama unatarajia kupata ujauzito, unaweza kujiuliza kuhusu kizazi chako na jinsi gani unaweza kukiboresha. Kuna baadhi ya mambo yanayoweza kuwa nje ya uwezo wako, kama vile masuala ya matibabu yanayoathiri uwezo wa kubeba mimba. Lakini uchaguzi wako wa mtindo wa Maisha unaweza kuwa na athari kwenye uzazi wako pia.

NUKUU: Hapa kuna kile unachohitaji kukifahamu ili kulinda na kuimalisha kizazi chako. Hebu fuatilia Makala hii vizuri.

Je, Kizazi Cha Mwanamke Ni Nini?

Kizazi cha mwanamke ni uwezo wa mwanamke kubeba mimba na kupata mtoto. Wewe Pamoja na mwenzi wako lazima mjiulize kuhusu kizazi chenu ikiwa kama mumejaribu mara kwa mara kupata mimba, bila kutumia kinga wakati mnapofanya tendo la ndoa angalau kwa mwaka mmoja au miezi sita hivi endapo kama una umri Zaidi ya miaka 35, lakini bila mafanikio.

Je, Nini Husababisha Matatizo Ya Uzazi Kwa Mwanamke?

Masuala mbalimbali ya matibabu yanaweza kuchangia matatizo ya uzazi kwa mwanamke, nayo ni kama haya yafuatayo:

  • Matatizo ya kizazi kama vile, uvimbe wa fibroid au vivimbe kwenye vifuko vya mayai
  • Matatizo yay ai kutokupevua, hali ambayo huathiri uwezo wa kuachiliwa yai kutoka kwenye vifuko vya mayai. Hii ni Pamoja na matatizo ya homoni imbalansi nk.
  • Kuziba kwa mirija ya uzazi, hali ambayo mara nyingi husababishwa na PID,
  • Vivimbe vingi nje ya ukuta wa mfuko wa uzazi(endometriosis)
  • Kukosa hedhi ukiwa bado na umri mdogo, nk

Umri pia nao huchangia. Kuchelewa kupata mimba kunaweza kupunguza uwezo wa kupata ujauzito. Kupungua kwa kiwango na ubora wa mayai yako kulingana na umri wako husababisha kuwa vigumu sana kupata ujauzito.

Je, Ufanye Nini Ili Kuimarisha Kizazi Chako?

Uchaguzi wa maisha ya afya  unaweza kukukusaidia kuimarisha uwezo wa tumbo lako la uzazi. Chukua hatua juu ya mambo haya:

  • Tengeneza uzito wako uwe mzuri
  • Epukana kabisa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa
  • Ondoa maambukizi katika via vya uzazi(PID)
  • Epuka kazi za usiku, kama ikiwezekana. Kufanya kazi mara kwa mara zamu ya usiku kunaweza kukuweka katika hatari kubwa ya ugumba au utasa, pengine kwa kuathiri uzarishwaji wa homoni. Kama unafanya kazi zamu ya usiku, jaribu kupata usingizi wa kutosha pale unapata muda wa kupumzika

NUKUU: Ili hali msongo wa mawazo hautakuzuia kupata ujauzito, basi zingatia sana kupunguza mfadhaiko na ufanye mazoezi ya afya ya kukabiliana na hali kama vile mbinu za kupumzika, wakati unapojaribu kupata ujauzito.

Ndugu msomaji naomba niishie hapa katika makala yetu leo, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATsAP ili uunganishwe na darasa letu uweze kupata elimu ya afya kila siku.

Je, Unahitaji Huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670 au 0712181626,

Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!


Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa