Yafahamu Madhara Ya Magonjwa Ya Zinaa Pale Yanapokaa Muda Mrefu Bila Kutibiwa.
Wasichana wengi wanaojihusisha na maswala ya ngono katika umri mdogo wanakabiliwa na ongezeko la uwezekano wa kupata saratani ya shingo ya kizazi (cervical cancer). Shingo ya kizazi ambayo haijakomaa inapokutana na misukosuko ya ngono mingi hudhoofika na kupoteza nguvu za kukabiliana na mashambulizi ya virus vya Human Papilloma – (HPV) ambao husababisha saratani hiyo mapema au baadaye sana.
Virusi hawa huambukiza kwa njia ya kujamiiana na mwanaume hata kama atakuwa amevaa
kondomu wakati wa kufanya tendo la ndoa na msichana. Saratani hii ni tatizo kubwa
la kiafya linaloongoza kwa vifo vya wanawake wengi duniani leo.
Ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kwa kawaida
huwapata wanawake wengi ambao huanza kujamiiana huku wakiwa katika umri mdogo,
miaka michache baada ya kuvunja ungo wao.
NUKUU: Wasichana na wanawake wenye wapenzi wengi, au wenye wapenzi wakiume ambao wana mtandao mkubwa wa wapenzi wengine wengi, huwa katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya virusi wanaosababisha ugonjwa wa saratani ya shingoyakizazi. Kwa bahati mbaya sana wasichana wengi hupata maambukizi ya virusi hawa kwa kufanya ngono kwa mara ya kwanza, hata kama ni mara mojatu.Tatizo jingine kuhusiana na maambukizi ya virusi hawa ni kwamba, msichana anaweza kuishi na virusi hawa bila habari kwa miaka 10 hadi 15 hivi ndipo madhara yake yanapojitokeza kwa uwazi.
Tatizo jingine linalowakabili wasichana wadogo wanaoendekeza ngono ni ugumba wakati watakapohitaji kuzaa. Magonjwa mengi ya ngono hushambulia mirija ya uzazi na kusababisha mirija hiyo kuziba. Mirija ya uzazi inapoziba, hushindwa kupitisha mayai kwa ajili ya kutunga mimba pale msichana atakapohitaji kupata watoto hapo baadaye.
Magonjwa ya ngono kwa wasichana pia husababisha
maumivu makali na kuugua hasa pale tumbo la chini linaposhambuliwa. Msichana hupata
ugonjwa wa mwana mimba yaani uambukizo katika mji wa mimba na wakati mwingine katika
njia ya mkojo yaani UTI. Hii pia huambatana
na maumivu makali wakati wa kukojoa.
Magonjwa mengine katika kundi hili la magonjwa
mengi mbalimbali, husababisha madhara makubwa na ya muda mrefu. Kaswende inaweza
kusababisha ugonjwa wa moyo na akili hasa pale msichana anapochelewa kupata matibabu
sahihi. Magonjwa haya pia yanaweza kukaa mwilini kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili
huku ya kiendelea kudhuru afya ya msichana.
Je, Jinsi Gani Mwanamke Au Mwanaume Anaweza Kujikinga Na MagonjwaYaZinaa?
Tabia ya kuchangia nguo za kuvaa au taulo za kujifutia maji baada ya kuoga pia ikiepukwa, inasaidia kwa kiasi kikubwa katika kinga ya magonjwa haya. Magonjwa kama kaswende, kisonono, upele na mengine yanaweza kuambukizwa kwa urahisi kupitia njia hii ya kuchangia nguo, mavazi ya aina nyingine au matandiko.
NUKUU: Njia nyingine ya muhimu ni ile ya kuepuka vishawishi kutoka kwa wavulana na wanaume wasiojiheshimu. Vishawishi vya pesa, simu za mkononi, lifti za magari, toyo, vyakula kama viazi vya kukaanga maarufu kama chips na nyama ya kuku, mara nyingi hutumika kuwanasa wasichana wengi hasa wale wenye tama mbaya ya vitu na wenye uroho wa vyakula. Wengi husahau umuhimu wa maisha na masomo na huangalia vishawishi kama mafanikio, badala ya mitego yenye hatari kwa afya zao na maendeleo yao ya baadaye.
Kumbuka kuwa mazoea mabaya ya kisitawishwa ni vigumu sana kuyaacha. Jitihada kubwa sana zinahitajika ili kuepuka mtego huu wa kufanya mapenzi ya ngono katika umri mdogo. Jitahidi kwa kadri ya uwezo na nguvu zako zote za kimwili, kiroho na kiakili kupambana na hisia hasi kuelekea ngono hata kama ni vigumu, kwani huo ndio uamuzi sahihi nas alama.
Jaza mawazo na hisia njema katika akili yako kila siku na kuepuka jambo lolote linalo kupeleka katika mtego wa kuwazia mapenzi ya mahaba na ngono.Tamaa ya ngono inaweza kutawaliwa kwa mafanikio, kwani Mungu ameweka uwezo mkubwa ndani ya akili za wasichana ili waweze kujitawala. Na ushahidi wa jambo hili ni mwingi sana katika jamii za mataifa mbalimbali katika historia.
Epuka hadithi na liwaya za mahaba, magazeti ya udaku yanayo sifia ngono, vipindi vya luninga (Televisheni) vinavyo pamba mambo ya mapenzi na ngono kiufundi ili kuwavutia vijana. Epuka mitandao ya wavuti, facebook, Youtube pamoja na CD za video zinazoonyesha picha za ngono na miziki inayochochea mapenzi na ngono. Nipende kuwashauri dada zangu, wadogo zangu wa kike na watoto wetu kuwa ni jambo la busara pia kuwaepuka marafiki pamoja na vijana warika lako wasio kuwa na maadili mema.
NUKUU: Wasichana wengi huondoa hofu na kujidanganya kuwa wanaweza kuonyeshana mapenzi na wavulana wadogo wanaokaribiana umri na wao kwa kukumbatiana, kubusiana, kunyonyana ndimi na kushikana shikana sehemu za siri bila kufanya ngono. Hilo ni jambo la hatari, ni mbegu nzuri ambayo baada ya muda mfupi itazaa matunda ya ngono hatarishi. Nawasihi sana wasichana muwe makini na vijana wanaume wenye umri mdogo. Vijana wengi wa kiume wamekosa maadili haijalishi wapo vyuoni au mitaani.
Matendo hayo huamusha na kuchochea kwa nguvu sana hisia, tamaa mbaya na hamu kali ya ngono kwa wasichana na wavulana ambayo itawasumbua sana na baada ya muda mfupi sana watatumbukia ghafla katika mtego wa ngono hatarishi. Kanuni ya usalama ni kuepuka kucheza chezan a mambo yahatari. Epuka kucheza cheza na bunduki yenye magazine iliyojaa risasi, kwani ni rahisi kufyatuka na kusababisha maafa makubwa.
Hivyo basi msomaji, makala yetu inaishia hapa, nakaribisha kipindi cha maswali na maoni yako, karibu sana.
Je, Nini Suluhisho Lake?
Ikiwa kama una maambukizi ya magonjwa ya zinaa, basi James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa ya zinaa. Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626.
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment