Chai Bora Ya Kujitengenezea Nyumbani Mwenyewe Kwa Ajili Ya Tatizo La Miguu Kuvimba (Edema).

Unatafuta moja ya chai bora zaidi ya kuzuia maji kukusanyikana mwilini na kuufanya mwilini kuvimba (edema)?  Makala hii itashughulikia swala hili. Parsley hutumiwa katika kutengeneza aina mbalimbali za chakula,  lakini pia ina idadi ya faida za matibabu. Ina wingi wa Vitamini K, vitamini C, vitamini B, na vitamini A, pamoja na madini kama vile potasiamu na chuma, yapo kwa wingi katika mimea hii ya mboga za majani. Kwahiyo ni chakula kizuri pia ni dawa bora kabisa.

Inasaidia katika kudhibiti uzito wa muda mrefu, kudhibiti sukari kwenye damu, na kuzuia matokeo ya ugonjwa wa kisukari kwenye ini.

Pia, parsley imeonyeshwa kuwa ina uwezo wa kutulinda na magonjwa mbalimbali, ikiwamo pumu, saratani ya utumbo, kisukari, na mafuta kujaa kwenye mishipa ya damu, pamoja na kuimarisha mfumo wetu wa kinga, kupambana uvimbe katika miili yetu, kulinda mishipa ya damu, na kupunguza hatari ya saratani.

Hata hivyo ni dawa bora ya asili katika kutibu miguu iliyovimba. Hivyo, ni tiba nzuri sana ambayo imeokoa maisha ya watu waliokuwa wanaelekea katika kupoteza uhai wao kwani hupunguza mrundikano wa maji mwilini kwa haraka zaidi.

Uvimbe kwenye miguu ni matokeo kukusanyika kwa maji mwilini (edema), na kwa kawaida husababishwa kwa sababu ya ujauzito.

Kwa kuongezea, uvimbe waweza pia kusababishwa na matumizi mabaya ya madawa fulani, chango la uzazi, maisha ya kukaa sana, na ulaji wa vyakula vilivyosindikwa au vya chumvi nyingi. Parsley ni dawa ya asili yenye nguvu sana, ambayo imekuwa ikitumika miaka mingi iliyopita, na ni dawa bora zaidi katika dawa za asili ambazo tunaweza kutumia.

Jinsi Ya Kuandaa

Chukua sufuria weka jikoni, weka maji halafu yamshe kabisa yatokote, kisha epua, halafu mimina kwenye kikombe kikombe, ongeza 1/4 ya majani safi ya parsley (yaliyokatwakatwa). Loweka, yaache yakae dakika 5 hadi 7, chuja, kisha kunywa. Unaweza kutumia mara 2 kwa siku kila siku mpaka hali ya kuvimba miguu itoweke.

Inafaa sana kwa mama wajawazito na kwa wengine wote wanaopatwa na hali ya miguu kuvimba kutokana na mkusanyiko wa maji mwilini.

Neno La Faraja: Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote. Zaburi 103:3.

Rafiki msomaji, makala yetu inaishia hapa, nikukaribishe kwa maswali na maoni yako.

Unahitaji huduma au suluhisho, basi tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

 

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa