Fahamu Chanzo Cha Kuvimba Kwa Tezi Ya Pituitari (Prolactinoma) Kwenye Ubongo.
Prolactinoma ni hali ya uvimbe inaojitokeza kwenye tezi ya pituitary inayokuwa kwenye ubongo wako pale inapozarisha homoni nyingi zaidi kuliko kawaida za prolactin. Chanzo kikubwa ni kupungua kwa viwango vya homoni au vichochezi vya uzazi ambazo ni estrogen inayokuwa kwa mwanamke na testosterone inayokuwa kwa mwanaume.
NUKUU: Madaktari mara nyingi hujitahidi wanatibu tatizo hili kwa dawa ili kurejesha kiwango cha homoni yako ya prolactin kuwa katika hali yake ya kawaida.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Kunaweza kusiwe na dalili au ishara pale kunapotokea uvimbe huo. Hata hivyo, dalili zinaweza kutokea kutokana na wingi wa homoni ya prolactin kwenye damu(hyperprolactinemia) au kutokana na presha kwenye tishu zinazouzunguka uvimbe huo mkubwa wa tezi ya pituitary. Kwakuwa homoni ya prolactin iliyoongezeka inaweza kuharibu mfumo wa uzazi wa mwanamke(hypogonadism), hivyo basi, baadhi ya dalili za prolactinoma hujitokeza sana kwa wanawake kuliko wanaume.
Prolactinoma kwa wanawake huonyesha dalili kama zifuatazo:
- Vipindi vya hedhi kubadirika au kutokupata hedhi kabisa
- Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa kutokana na hali ya ukavu ukeni
- Kutokwa na chunusi nyingi usoni au nywele nyingi maeneo hayo.
- Kutokwa na uchafu kwenye matiti wenye muonekano kama maziwa hata kama huna ujauzito au hunyonyeshi.
Tukiangalia tena kwa wanaume tatizo hili la prolactinoma linapojitokeza, huonyesha dalili kama zifuatazo:
- Kupungukiwa nguvu za kiume
- Nywele za usoni kupungua
- Matiti kuwa makubwa kama ya mwanamke (gynecomastia)
Katika jinsia zote mbili, uvimbe wa tezi ya prolactin unaweza kusababisha mambo yafuatayo;
- Mifupa kuwa laini
- Kupungua kwa uzarishaji wa mwingine wa homoni ya tezi ya pituitary
- Kukosa hisia za tendo la ndoa
- Kichwa kuuma
- Macho kutokuona vizuri
- Ugumba
NUKUU: Hivyo basi, wanawake hupata dalili mapema kuliko wanaume, huku vivimbe vikiwa vidogo sana, hasa wanapoanza kuona ishara za kutopata hedhi au vipindi vya hedhi kubadiri badirika. Wanaume wao huona dalili baadaye pale uvimbe unapokuwa mkubwa na kusababisha kichwa kugonga au kuwa na matatizo ya macho.
Je, Nini Husababisha Tatizo Hili?
Prolactinoma ni mojawapo ya uvimbe ambao huendelea kukua kwenye tezi ya pituitary. Chanzo cha uvimbe huu haujafahamiki.
Tezi ya pituitary huwa ni ndogo tu yenye umbo kama punje ya harage, inayokuwa ndani ya ubongo wako. Mbali na umbo lake kuwa dogo, lakini tezi hii hushughulika karibia na kila sehemu ya mwili wako. Homoni zake husaidia kurekebisha kazi muhimu kama vile mwili kukua, kuunguza mafuta, shinikizo la damu pamoja na uzazi.
Je, Vihatarishi Vyake Vinakuwaje?
Hali hii mara nyingi hujitokeza kwa wanawake wenye umri wa miaka 20 na 34, lakini inaweza kujitokeza katika jinsia zote mbili katika umri wowote. Tatizo hili huwa ni nadra sana kuonekana kwa watoto.
NUKUU: Ikiwa kama una tatizo la prolactin na unahitaji kuwa mjamzito au tayari ni mjamzito, basi nakushauri ufike hospitali kumuona daktari. Vipimo na matibabu vitakuwa vya muhimu sana kwako.
Je, Madhara Yake Ni Nini?
Madhara ya ugonjwa huu yanaweza kuwa pamoja na haya yafuatayo:
- Kupoteza Uwezo Wa Kuona: Tezi hii ikiachwa bila kutibiwa, inaweza kuongezeka ukubwa inaweza kuongezeka na kuwa kubwa sana na hivyo kukandamiza neva za macho.
- Tezi Ya Pituitari Kushindwa Kufanya Kazi: Kuwa na uvimbe mkubwa zaidi kwenye tezi, kunaweza kusababisha kutofanya kazi kwa homoni nyingine zinazodhibitiwa na tezi ya pituitari, na kusababisha tezi ya pituitari kushindwa kufanya kazi vizuri, upungufu wa adrenali na upungufu wa homoni ya ukuaji.
- Mifupa Kuwa Laini: Prolactini nyingi zinaweza kupunguza uzalishaji wa homoni za estrojeni na testosterone, na kusababisha kupungua kwa uwezo wa mifupa na kusababisha hatari ya mifupa kuvunjika kwa urahisi kabisa.
- Matatizo Ya Ujauzito: Wakati wa ujauzito wa kawaida, uzalishaji wa homoni estrojeni huongezeka. Ikiwa wewe ni mjamzito na una una uvimbe wa tezi ya pituitari (prolactinoma) kubwa, viwango hivi vya juu vya estrojeni vinaweza kusababisha kuota vivimbe kwenye kizazi kama vile fibroid na kuendelea vikubwa na kuonyesha ishara au dalili zinazohusiana, kama vile maumivu ya kichwa na mabadiliko katika kuona.
Ikiwa una prolactinoma na unataka kuwa mjamzito au tayari kuwa ni mjamzito, basi zungumza na daktari wako. Matibabu na ufuatiliaji wa vipimo yanaweza kuhitajika.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tunazo dawa za asili nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa tatizo hili. Ikiwa kama unahitaji huduma, basi tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibuni Sana!
Comments
Post a Comment