Fahamu Jinsi Ya Kuondoa Sumu Mwilini Mwako Kwa Kutumia Vyakula Tu!

Kuna nadharia inayokubarika katika jamii ya kufikiri kwamba magonjwa mengi huchangiwa na uwezo wa sumu nyingi mwilini, zitokazo nje ya mwili (uchafu wa mazingira, matumizi ya tumbaku, pombe na vinjwaji vingine, viwatilifu, kemikali za usafi, nk), na kutoka ndani ya miili yetu (mabaki ya umeng’enyaji wa chakula, kama vile tindikali ya uriki na urea, vinavyoongezeka kutegemeana na wingi wa protini inayoliwa, sumu zizalishwazo na uvimbe, nk).

Kwa bahati nzuri miili yetu ina mirija kwa ajili ya kutoa sumu mwilini, ukianza na ini, na figo ambavyo huondoa mwilini vitu vingi visivyohitajika. Hata hivyo kukiwa na ziada ya sumu katika damu, mfumo wa kawaida wa kusafisha mwili huzidiwa.

Juisi kama ile isafishayo na nyinginezo huwa na mchanganyiko mzuri kwa kuedneleza usafishaji wa sumu mwilini yumkini na kusababisha magonjwa.

 

VIUNGO

Kwa Milo Mitatu Ya Milimita 250

  • karoti 5 za wastani
  • tufaa 2 za wastani, usizimenye na zisiwe za kukuzwa kwa madawa
  • vikonyo 4 vya figili
  • limao 1 la wastani, lisiwe la kukuzwa kwa madawa

 

MAANDALIZI


  1. Chakata viambata vyote kwenye kikamulio au blenda
  2. Ondoa sehemu ya ganda la limao kwani linaongeza ladha kali.

Neno La Faraja: Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu….1 Wakorinto 6:19.


Ubarikiwe sana ndugu msomaji, makala yetu inaishia hapa, tunakaribisha kipindi cha maswali na maoni yako.

 

Je, unahitaji huduma zaidi? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/ 0712 181 626.

Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa