Fahamu Madhara Ya Maambukizi Kwenye Figo Zako
Maambukizi ya figo ni aina ya maambukizi ya mfumo wa mkojo ambayo kwa kawaida hutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo zako. Bakteria ndio chanzo cha ugonjwa huu. Dalili ni pamoja na homa, shida ya kukojoa, maumivu ya kiuno na maumivu wakati wa kukojoa. Maambukizi ya figo yanatibiwa kwa madawa ya antibiotic.
Je, Maambukizi(Pyelonephritis )Ya Figo Ni Nini?
Maambukizi kwenye figo(pyelonephritis) huwa ni aina ya maambukizi katika mfumo wa mkojo (UTI). Bakteria husababisha maambukizi haya pale wanapohama kutoka sehemu nyingine ya mwili wako, kama vile kibofu cha mkojo, mpaka kwenye figo yako moja au zote mbili.
Maambukizi ya figo yanaweza kuwa makubwa kuliko UTI inayokuwa maeneo ya chini. Muone mhudumu wa afya ikiwa una dalili za maambukizi ya figo.
Je, Unawezaje Kutofautisha Kati Ya Maambukizi Ya Figo Na UTI?
Maambukizi ya figo ni aina ya maambukizi yanayokuwa kwenye mfumo wa mkojo (UTI). Lakini watu wanaposema "UTI," mara nyingi wanamaanisha maambukizi yanayokuwa kwenye njia ya chini ya mkojo, au maambukizi ya yanayokuwa kwenye kibofu cha mkojo au kwenye mrija wa mkojo. Maambukizi ya UTI katika maeneo ya chini na maambukizi ya figo yanaweza kuwa na dalili zinazofanana, lakini maambukizi ya figo yana uwezekano mkubwa wa kukufanya ujisikie mgonjwa ghafla, kukupa homa au kusababisha maumivu kwenye kiuno chako au mbavu.
Je, Dalili Zake Ni Nini?
Kwa kawaida dalili za maambukizi ya figo ni pamoja
na:
- homa
- baridi
- maumivu kiunoni au pembeni mwa kiuno
- maumivu wakati unapokojoa
- mkojo wenye damu au wenye rangi ya kijivu ambao unaweza kuwa na harufu mbaya
- kuhisi kukojoa mara kwa mara
Je, Nini Visababishi Vyake?
Maambukizi ya bakteria ndio sababu ya kawaida ya
maambukizi kwenye figo. Virusi vinaweza kusababisha, pia, lakini ni nadra kwa
watu wenye afya. Baadhi ya aina za bakteria zinazosababisha maambukizi kwenye
figo ni pamoja na:
- E. coli
- Proteus mirabilis
- Enterobacter.
- Staphylococcus.
Je, Unapataje Maambukizi Kwenye Figo
Figo zako hukufanya ukojoe ili uondoe taka mwilini. Mkojo hupita kwenye mirija (ureters) hadi kwenye kibofu cha mkojo (mfuko unaoshikilia mkojo wako hadi utakapoenda chooni). Kutoka hapo, hushuka kupitia mrija mwingine (urethra) ili utoke mwilini mwako. Hii kwa kawaida husafisha bakteria yoyote au vijidudu vingine.
Wakati mwingine, bakteria wanaweza kupanda juu ndani ya mwili wako na kuambukiza sehemu za njia yako ya mkojo, ikiwa ni pamoja na mrija wa mkojo, kibofu cha mkojo(cystitis) au njia ya mkojo. Kutoka hapo, bakteria wanaweza kuhamia kwenye figo moja au zote mbili, na kusababisha maambukizi ya figo. Bakteria wanaoingia kwenye damu yako kutoka sehemu nyingine ya mwili wako pia wanaweza kuambukiza figo zako.
Je, Ni Mambo Gani Hatarishi Yanayotokana Na Maambukizi Ya Figo?
Vihatarishi
vya maambukizi ya figo ni pamoja na:
- Vizuizi: Kitu chochote kinachokuzuia kutoa mkojo nje ya njia yako ya mkojo kinaweza kuruhusu bakteria kukua na kuzariana na kurudi kwenye figo zako. Hii ni pamoja na mawe kwenye figo, tezi dume kuvimba, mfuko wa uzazi kuchomoza. Mgandamizo kwenye kibofu chako cha mkojo wakati wa ujauzito pia inaweza kuongeza hatari kwako.
- Mkojo Kurudi Nyuma: Hii ni hali ambapo kukojoa huenda kwa njia isiyo sahihi na kurudi nyuma kutoka kwenye kibofu chako.
- Hali zinazokuweka katika hatari zaidi ya kuambukizwa. Hizi ni pamoja na kisukari, VVU na pale unapotumia madawa ya kinga.
- Jinsia: Wanawake wao kwa kawaida huwa wana njia fupi ya mkojo na ndio maana huwa rahisi mno kuambukizwa na bacteria.
Je, Madhara Yake Ni Nini?
Wakati mwingine, maambukizi ya
figo yanaweza kusababisha matatizo ya kutishia maisha, hasa kwa watu walio na
mfumo dhaifu wa kinga au masuala mengine ya msingi ya afya. Hizi ni pamoja na:
- Bakteria kuanza kuharibu sehemu za figo zako na kuunda gesi. Ni kawaida zaidi kwa watu walio na ugonjwa wa kisukari.
- Tishu za figo kuharibika na hivyo kupunguza utendaji kazi wa figo zako.
Je, Nini Suluhisho Lake?
James Herbal Clinic tumekuandalia
dawa nzuri kabisa zenye uwezo mkubwa wa kuondoa maambukizi kwenye figo.
Unahitaji huduma? Basi wasiliana
nasi kwa namba hizi: 0768 559 670 au 0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment