Fahamu Madhara Ya Ugonjwa Wa Saratani Ya Tezi Dume
Saratani ya tezi dume ni saratani inayotokea kwenye tezi dume. Tezi dume ni tezi ndogo yenye umbo la jozi (walnut) kwa wanaume ambayo hutengeneza uteute wa manii ambao hurutubisha na kusafirisha mbegu za kiume.
Saratani ya tezi dume ni moja ya aina ya saratani ya
kawaida. Saratani nyingi za tezi dume hukua polepole na hufungamanishwa kwenye
tezi ya dume, ambapo haziwezi kusababisha madhara makubwa. Hata hivyo, ingawa
aina fulani za saratani ya tezi dume hukua polepole na huenda zikahitaji
matibabu kidogo au hata kutopata matibabu yoyote, aina nyingine huwa ni mbaya
na zinaweza kuenea haraka mwili mzima.
Saratani ya tezi dume ambayo hugunduliwa mapema wakati bado ikiwa kwenye tezi dume, ina nafasi nzuri zaidi ya matibabu )yenye matumani na mafanikio.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Saratani ya tezi dume inaweza isionyeshe dalili au
ishara katika hatua zake za awali.
Saratani ya tezi dume ambayo imeendelea zaidi inaweza
kusababisha dalili na ishara kama vile:
- kusumbuka kukojoa
- kupungua nguvu ya kusukuma mkojo kwenye mrija wa mkojo
- damu kwenye mkojo
- damu kwenye shahawa
- maumivu kwenye mifupa
- uzito wa mwili kupungua
- nguvu za kiume kupungua
Je, Nini Vyanzo Vyake?
Haijulikani ni nini husababisha saratani ya tezi dume.
Madaktari wanajua kwamba saratani ya tezi dume huanza
wakati seli za tezi dume zinapoendelea kuwa na mabadiliko kwenye vinasaba. Vinasaba
(DNA) vya seli vina maelekezo ambayo
huiambia seli nini cha kufanya. Mabadiliko huiambia seli kukua na kugawanyika
haraka zaidi kuliko seli za kawaida. Seli zisizo za kawaida zinaendelea kuishi,
huku seli zingine zinakufa.
Mkusanyiko wa seli zisizokuwa za kawaida huunda uvimbe unaoweza kukua na kuvamia tishu zilizo karibu. Baada ya muda, baadhi ya seli zisizo za kawaida zinaweza kutengana na kuenea (metastasize) hadi sehemu nyingine za mwili.
Je, Nini Madhara Ya Tezi Dume?
Madhara ya saratani ya tezi dume na matibabu yake ni pamoja na:
- Saratani Ambayo huenea(metastasizes): Saratani ya tezi dume inaweza kuenea kwenye viungo vya karibu, kama vile kibofu cha mkojo, au kusafiri kupitia mfumo wako wa damu au mfumo wa limfu hadi kwenye mifupa yako au viungo vingine. Saratani ya tezi dume inayosambaa hadi kwenye mifupa inaweza kusababisha maumivu na kuvunjika kwa mifupa kwa urahisi. Pindi saratani ya tezi dume inapoenea katika maeneo mengine ya mwili, bado inaweza kuitikia au kukubali matibabu na inaweza kudhibitiwa, lakini kuna uwezekano wa kuponywa.
- Kushindwa Kujizuia: Saratani ya tezi dume na matibabu yake yanaweza kusababisha kutoweza kuzuia au kudhibiti mkojo. Matibabu ya kutoweza kujizuia kukojoa yanategemea aina ya saratani uliyonayo, jinsi ilivyo mbaya kiasi gani na uwezekano wa kuboreka kwa muda.
- Upungufu Wa Nguvu Za Kiume: Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kutokana na saratani ya tezi dume au matibabu yake ya muda mrefu hasa pale unapotumia madawa ya vidonge, ikiwa ni pamoja na upasuaji, na mionzi. Dawa za asili pamoja na vyakula vya asili vilivyoandaliwa kwa ajili ya ugonjwa huu, vinaweza kutibu na kuondoa ugonjwa huu.
Napenda kuishia hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako. Pia unaweza kutuma namba yako ya WhatsAp tukakuunganisha katika darasa letu.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic
tunayo dawa nzuri ya asili yenye uwezo mkubwa wa kuondoa ugonjwa wa saratani ya
tezi dume bila kutumia upasuaji.
Je, Unahitaji Huduma?
Basi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu Sana!
Comments
Post a Comment