Fahamu Madhara Ya Vinywaji Baridi (Soda)
Huenda huburudisha, hata hivyo, havikati kiu wala kuchangia afya!
Kile kiitwacho eti vinywaji baridi, soda, au maji ya limau vimetengenezwa kwa sukari zilizosafishwa kama vile shira ya nafaka (yenye fraktozi nyingi), kuwekwa rangi, kuziduliwa, na gesi ya kaboni.
Matumizi sugu ni chanzo cha matokeo yasiyopendeza miongoni mwao, yafuatayo yanajitokeza zaidi ni:
- ugonjwa wa Kisukari
- unene kupita kiasi
- maradhi ya figo, hasa unapotumia vinywaji vya baridi vya Kola
- mifupa kuwa laini kutokana na kupungua kwa madini ya kalsiamu
Utafiti wa Framingham kuhusu mifupa kuwa laini
ulionyesha kwamba wanawake wanaotumia kinywaji kimoja cha Kola kwa siku, hata
kama hakina kafeini au bila sukari, wana asili 5% chini ya uzito wa madini
unaotakiwa kwenye mifupa kuliko wanawake wanaotumia kidogo zaidi ya kinywaji
kimoja cha kola kwa mwezi. Asidi ya fosforasi katika vinywaji ndio inayohusika
hasa kwa madhara yake ya kupunguza kalisi.
James Herbal Clinic tunazidi kutoa ushauri kwako ndugu msoaji kupunguza matumizi ya vinywaji baridi na ikiwezekana achana navyo kabisa ili kulinda afya ya mwili wako.
Neno La Kufariji: Usiingie katika njia ya waovu, wala usitembee katika njia ya wabaya. Jiepushe nayo, usipitie karibu nayo, igeukie mbali ukaende zako. Mithali 4: 14, 15.
Unahitaji huduma? Basi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment