Fahamu Tofauti Kati Ya Uvimbe Wa Fibroid (Uterine Fibroid) Na Uvimbe Maji(Ovarian Cyst)
Vivimbe hivi vinaweza kuonekana kuwa vya kawaida, hata kwa mtu ambaye hajapatwa na matatizo haya, lakini vivimbe maji (cysts) na vivimbe kwenye kizazi (fibroids) vina sifa tofauti sana. Vivimbe vya Fibroid huota kwenye tumbo au mfuko wa uzazi wakati vivimbe maji (ovarian cysts) hukua kwenye vifuko vya mayai(ovaries). Muundo wa vivimbe hivi pia hutofautiana: uvimbe maji huwa ni vifuko vilivyojaa majimaji ambavyo hukua nje ya vifuko vya mayai (ovaries), wakati vivimbe vya fibroid huwa ni tishu zinazoota na kukua ndani au nje ya ukuta wa mfuko wa uzazi(uterus).
Wanawake wengi hupatwa na uvimbe maji kwenye ovari na uvimbe wa fibroid kwenye kizazi kwa wakati mmoja katika maisha yao. Wanawake wengi wanaweza kushindwa kutambua kwamba wana uvimbe maji(ovarian cyst) au uvimbe wa fibroid kwenye matumbo yao ya uzazi, isipokuwa tu pale wanapohisi dalili au kufanya vipimo vya Ultrasound kwa kupiga picha ili kubaini kama ni uvimbe wa fibroid kwenye kizazi au uvimbe maji kwenye vifuko vya mayai. Vivimbe hivi unaweza kuviona kuwa ni vya kawaida sana na kwamba vinaweza visiathiri afya yako, lakini kumbe vinaweza kusababisha madhara makubwa ambayo yanahitaji matibabu yenye gharama kubwa hapo baadaye.
Je, Nini Husababisha Uvimbe Wa Fibroid?
Vyanzo vyake kwa kawaida huwa ni vingi kidogo, navyo huwa kama hivi ifuatavyo hapa;
⦁ Mwanamke kufikisha umri wa miaka 28-33 bila kupata ujauzito
⦁ Ugumba wa muda mrefu
⦁ Matumizi ya pedi zisizokuwa na uthibitisho wa madaktari.
⦁ Kutoa mimba
⦁ Mapungufu ya lishe mwilini, nk.
⦁ Kutoshiriki tendo la ndoa muda mrefu(yaani dada ama mama anapofikia umri wa miaka 25-30 bila kushiriki tendo la ndoa)
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Uvimbe katika kizazi cha mwanamke ukiwa mdogo unaweza usiwe na dalili zozote, na dalili hutegemea sehemu ulipo kwenye mfuko wa uzazi na pia ukubwa wake. Hata hivyo dalili za ugonjwa huu huwa kama ifuatavyo:
⦁ Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi
⦁ Kupata hedhi mara mbili kwa mwezi.
⦁ Maumivu makali wakati wa hedhi.
⦁ Maumivu ya tumbo chini ya kitovu,
⦁ Hedhi zisizokuwa na mpangilio
⦁ Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
⦁ Kutotunga mimba au kuharibika kwa mimba
⦁ Kukosa choo ama tumbo kujaa gesi na kumfanya muhusika kuwa anajamba jamba mara kwa mara.
⦁ Maumivu makali wakati wa hedhi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma uvimbe huo.
⦁ Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya ama usiokuwa na harufu lakini mwingi.
Je, Madhara Yake Ni Nini?
Uvimbe wa fibroid unapozidi kuwa mkubwa husababisha damu kupungua mwilini, mzunguko wa hedhi kubadirika, kukosa hedhi au kutokwa na damu kwa mfululizo au kutokwa na majimaji ukeni yenye harufu, tumbo kuwa kubwa kama mjamzito, kushindwa kupata mimba au kupata mimba halafu inatoka.
Je, Nini Husababisha Vivimbe Maji(Ovarian Cysts)
Kwa kawaida visababishi vya vivimbe hivi huwa ni vingi mno navyo hutofautiana kama hivi ifuatavyo:
⦁ Kufanya tendo la ndoa mwanamke akiwa hedhini,
⦁ Kupungua kwa homoni ya estrogen
⦁ Kuziba kwa mirija ya uzazi ambayo husababisha mkusanyiko wa majimaji
⦁ Vimelea vya muda mrefu kama vile fangasi, nk.
⦁ Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, pangusa, malengelenge au PID, nk.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Kwa kawaida dalili za vivimbe katika vifuko vya mayai humfanya mwanamke kusumbuka sana kuja kuvitambua, navyo huwa kama ifuatavyo:
⦁ Tumbo kuunguruma au kuvimba
⦁ Maumivu katika nyonga kabla au wakati wa hedhi
⦁ Maumivu makali mara mwanamke anapokutana na mumewe
⦁ Maumivu ya kiuno au misuli ya mapaja.
⦁ Matiti kuuma
⦁ Kuhisi kichefuchefu na kutapika.
Je, Nini Madhara Yake?
Tatizo hili lisipotibiwa husababisha mwanamke mfumo wa homoni kubadiri, kukosa hedhi au vipindi vya hedhi kuruka au kushindwa kupata ujauzito na kuwa mgumba daima.
Je, Nini Suluhisho Lake?
James Herbal Clinic tunazo dawa za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo haya ya uvimbe.
Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment