Je, Nini Humafanya Mwanamke Kuhisi Ujauzito Wakati Hana?
Mimba kwa kawaida huwa ni wakati wa kusisimua kwa mzazi mtarajiwa. Lakini mara nyingi mimba haiishii kwa mtoto anayetarijiwa. Kwa upande mwingine, wanawake huamini kuwa wana mimba, ili kutambua tu kuwa dalili zao hazikusababishwa tu na ujauzito, bali na kitu kingine kabisa.
NUKUU: Mimba ya uongo, kitaalamu tunaita, “Pseudocyesis” ni imani unayokuwa nayo kwamba unatarajia kupata mtoto wakati hakubeba mimba ya mtoto kabisa. Watu wenye mimba ya uongo wana dalili nyingi za ujauzito, japokuwa sio zote, lakini anakuwa na matarajio kabisa ya mtoto tumboni, na wanakuwa na dalili kama hizi:
- Uzito wa mwili kuongezeka
- Kuhisi kichefuchefu
- Mgongo kuuma
Je, Nini Husababisha Tatizo Hili?
Japokuwa visababishi vyake halisi bado havijafahamika, lakini madaktari wanadhania kuwa mambo ya kisaikolojia yanaweza kuufanya mwili kuhisi kwamba una mimba.
Mwanamke anapojihisi kuwa ana hamu ya kuwa na mimba, hali ambayo inaweza kusababishwa na mambo kama haya:
- Ugumba
- Mimba kurudia kutoka
- Kukaribia ukomo wa hedhi
- Au nia ya kuolewa
NUKUU: Basi, miili yao wanawake hawa inaweza kutoa ishara fulani za ujauzito kama vile tumbo kuwa kubwa, matiti kuwa makubwa, au hata kuhisi mtoto anacheza tumboni. Ubongo wa mwanamke baadaye hutafsiri vibaya ishara hizo kama mimba, na husababisha kuachiwa kwa vichocheo au homoni kama vile estrogen na prolactin ambazo hupelekea kuonekana dalili za mimba kwa uhalisi wake kabisa.
Je, Dalili Za Mimba Ya Uongo Zinakuwaje?
Wanawake wenye mimba ya uongo huwa wana dalili nyingi mno kama nilivyoseama hapo awali, na zinakuwa kama zile tu za mjamzito, nazo huwa kama hizi zifuatazo:
- Kutokupata hedhi
- Tumbo kuwa kubwa
- Matiti kujaa, mabadiriko kwenye chuchu, na kutoa maziwa
- Kichefuchefu na kutapika
- Uzito wa mwili kuongezeka
NUKUU: Dalili hizi zinaweza kukaa kwa muda wa wiki chache, kwa miezi 9, au hata miaka kadhaa. Asilimia kidogo kabisa ya wagonjwa wenye ujauzito wa uongo watakuja kwa daktari hospitali wakijihisi kama wana uchungu wa kujifungua mtoto.
Je, Mimba Ya Uongo Inapimwaje?
Ili kubaini kuwa kama mwanamke ana mimba ya uongo, daktari kwa kwaida hutofautisha dalili zao, hufanya vipimo kwenye nyonga na ultrasound, kipimo kile kile kinachotumiwa kuhisi na kugundua mtoto asiyezaliwa wakati wa mimba ya kawaida.
NUKUU: Katika tatizo la ujauzito wa uongo, hakuna mtoto atakayeonekana kwenye kipimo cha ultrasound, na hakutakuwa na mapigo yoyote ya moyo. Wakati mwingine, hata hivyo, atatafuta badhi ya mabadiriko ya mwili yanayotokea wakati wa ujauzito, kama vile mfuko wa uzazi kukua, na mara nyingi shingo ya kizazi. Kipimo cha mimba kupitia mkojo mara nyingi hakitaonyesha kitu katika tatizo hili.
Je, Mimba Ya Uongo Inatibiwa Vipi?
Wanawake wanapoamini kuwa ni wajawazito, hasa kwa kipindi cha miezi kadhaa, inaweza kusikitisha sana kwao kujifunza kwamba wao sio wajawazito. Madaktari huhitaji kutoa habari, na kuwawezesha kisaikolojia, ikiwa pamoja na tiba, ili kumsaidia mgonjwa mwenye tatizo la mimba ya uongo aweze kupona kutoka kwenye hali ya kukata tamaa kwao.
Nashukuru sana mpendwa msomaji, naomba niishie hapa katika makala hii, nikaribishe tu kipindi cha maswali na maoni.
Je, Unahitaji ushauri? Tupigie kwa namba hizi: 0768 559 670/0712181626.
James Herbal Clinic pia tuna darasa endelevu katika Group la WHATSAP, hivyo unaweza kutuma namba yako ili uweze kunganishwa na darasa zuri la afya.
Karibuni sana!
Comments
Post a Comment