Je, Nini Kinachomfanya Mwanamke Kukosa Hedhi Mwezi 1-2 Na Kuendelea?
Hii ni hali ya mwanamke ambaye amepevuka na kukomaa maumbile yake ya uzazi lakini anashindwa kupata hedhi au anaweza kupitiliza siku zake za hedhi.
Kwa ufupi tatizo hili limekua likiwakumba na kuwaletea usumbufu wa kisaikolojia wanawake wengi wakidhani kwamba wamepata ujauzito nk, kumbe sivyo. Hata hivyo tatizo hili la kukosa hedhi linaweza kutokea awali au baadae kabisa maishani mwako.
NUKUU: Kuna aina mbili za tatizo hili la kukosa hedhi (amenorrhea), nazo zipo kama ifuatavyo;
1. Primary Amenorrhea:
Hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke au msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo ambapo hali hii huweza kuendana na kutopata mabadiliko ya kimaumbile yanayoambatana na kuvunja ungo kama vile kuota nywele sehemu za siri(yaani mavuzi), kuota matiti, nk, ila bado hapati siku zake.
2. Secondary Amenorrhea:
Hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito wala hanyonyeshi na ambaye hajakoma hedhi na wala hatumii dawa za uzazi wa mpango ambapo awali alikua akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama kwa muda huenda ni miezi au mwaka mzima hapati hedhi mpaka sasa.
Je, Jinsi Gani Mwanamke Hupata Hedhi?
Kwa kawaida ili mwanamke apate hedhi katika mzunguko ulio sawa ni lazima tezi ya hypothalamus na pituitary pamoja na kiwanda cha mayai(ovaries) viwe vinafanya kazi kwa ushirkiano wa pamoja bila kupishana.
Je, Vyanzo Vya Tatizo Hili Ni Nini?
Vyanzo vya tatizo hili vyaweza kuwekwa katika makundi makuu matatu ambayo ni:
- Yale yanayohusisha matatizo katika mfumo wa homoni,
- Yale yanayohusisha matatizo katika tezi ya pituitary, mfumo wa uzazi na
- Yale yanayohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke.
Visababishi hivyo huwa ni matatizo katika tezi za hypothalamus ambapo matatizo haya husababisha mambo haya yafuatayo:
- Uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitari,
- Upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi,
- Uzito mdogo kuliko kawaida.
- Tezi ya pituitari kushindwa kufanya kazi vizuri baada ya seli zake kufa, hii ni iwapo mama kama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua
- Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu (wataalamu wanaita prolactinemia). Proclatin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha, hivyo hali ya kuwa na proclatin nyingi katika damu husababisha kukosa hedhi.
- Kuwa na msongo wa mawazo ni hatari
- Kuziba kwa utando unaozunguka uke (yaani hymen), hivyo kukosekana tundu la kupitishia damu (yaani imperforate hymen),
- Mazoezi makali ya mwili na ulaji mdogo wa chakula, tabia hii hushusha homoni ambayo inahusika na kuweka siku zako katika hali nzuri yaani hufanya leptin kuwa katika kiwango cha chini sana hivyo ni hatari.
- Ugonjwa wa kurithi wa galactosemia unaoambatana na kuwa na kiwango kidogo cha sukari aina ya Galactose katika damu,
- Baadhi ya magonjwa ya viungo vya uzazi yamekua yakiambatana na kusimama kwa hedhi mfano wa magonjwa hayo ni uvimbe katika mirija ya uzazi, nk.
- Kukoma kwa hedhi: Hii ni hali ambayo hutokea kipindi cha miaka 42-55 homoni zinazohusika na kupata hedhi huwa kwenye kiwango cha chini sana kiasi kwamba haziwezi kufanya kazi sawasawa kama mwanzo.
Je, Dalili Za Tatizo Hili Zinakuwaje?
Mwanamke kuwa na vinyweleo vingi na kuota ndevu inamaanisha na kuashiria kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni za kiume mwilini mwake. Dalili zinazokuwepo ni kama ifuatavyo;
- Kuongezeka uzito kupita kiasi
- Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito wala hanyonyeshi
- Mwanamke kuwa na mhemko kuliko kawaida
- Uke kuwa mkavu
- Kutokwa jasho sana wakati wa usiku
- Kutokupata hedhi katika mpangilio
- Mabadiliko katika kupata usingizi, vinaweza kuashiria kuwepo kwa tatizo katika (ovaries).
Je, Nini Madhara Yake Ikiwa Tatizo Hili Likichelewa Kutibiwa?
Tatizo hili lisipotibiwa mapema na likaendelea kuwa sugu kwa muda mrefu, basi madhara yake huwa kama ifuatavyo:
- Matiti husinyaa na kupata hedhi bila mpangilio.
- Husababisha matatizo ya kutopata usingizi.
- Mwanamke kuchelewa kukoma hedhi(menopause) huwa ni hali mbaya, kwani husababisha baadaye ugonjwa wa saratani ya matiti kwa kiasi kikubwa.
- Mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwasababu ya kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi na uke kuwa mkavu.
James Herbal Clinic tuna dawa za asili zenye uwezo wa kuondoa vyanzo vya matatizo haya, ukitaka huduma tupigie kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Comments
Post a Comment