Kwanini Maambukizi Ya UTI Husababisha Figo Na Mirija Kuharibika?

Maambukizi katika njia ya mkojo (UTI) ni maambukizi katika sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo. Mfumo wa mkojo ni pamoja na figo, mirija inayotoa mkojo kwenye figo (ureter) mkojo, kibofu cha mkojo na mrija wa mkojo(urethra). Maambukizi mengi yanahusisha njia ya chini ya mkojo, yaani kwenye kibofu cha mkojo na mrija wa mkojo(urethra).

Wanawake wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya UTI kuliko wanaume. Kama maambukizi yakijikita sana kwenye kibofu cha mkojo, basi maumivu yanaweza kuwa makali na yenye kuchukiza. Lakini matatizo makubwa ya kiafya yanaweza kutokea ikiwa maambukizi ya UTI yataenea hadi kwenye figo.

Wahudumu wa afya mara nyingi hutibu maambukizi ya mfumo wa mkojo kwa kutumia madawa ya vidonge (antibiotics). Unaweza pia kuchukua hatua za kupunguza uwezekano wa kupata UTI hapo awali.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

UTI sio kila wakati huonyesha dalili. Lakini inapoonyesha dalili, basi mara nyingi huwa kama hizi zifuatazo:

·        hamu kali ya kukojoa isiyoisha

·        kuhisi maumivu makali unapokojoa

·        kukojoa mara kwa mara na kutoa kiasi kidogo cha mkojo

·        mkojo wenye rangi ya ukijivu kwa mbali

·        mkojo kuwa mwekundu au kuwa na rangi kama ya kola, yaani ishara za damu kwenye mkojo

·        mkojo wenye harufu kali

·        kuhisi maumivu ya nyonga kwa wanawake, hasa kuzunguka kwenye eneo la mfupa wa kinena.

Kwa watu wazima, UTI inaweza kupuuzwa au kudhaniwa kama hali zingine.

Aina Za Maambukizi Ya UTI

Kila aina ya UTI inaweza kusababisha dalili maalum zaidi. Dalili hutegemeana na sehemu gani ya njia ya mkojo iliyoathirika.


 Je, Vyanzo Vyake Ni Nini?

UTI hutokea wakati bakteria wanapoingia kwenye njia ya mkojo kupitia mrija wa mkojo na kuanza kuzaliana kwenye kibofu cha mkojo. Mfumo wa mkojo umeundwa kuzuia bakteria. Lakini ulinzi wakati mwingine hushindwa kufanya kazi ya kuzuia. Hilo linapotokea, bakteria wanaweza kukukaa kuzaliana na kukua na kuwa maambukizo kamili katika njia ya mkojo.

UTI ya kawaida hutokea hasa kwa wanawake na huathiri kibofu na mrija wa mkojo.

  • Maambukizi Kwenye Kibofu: Aina hii ya UTI kwa kawaida husababishwa na bakteria aina ya Escherichia coli (E. coli). E. Coli ni aina ya bakteria, kwa kawaida inayopatikana kwenye njia ya utumbo (GI). Lakini wakati mwingine bakteria wengine wanaweza kusababisha.Kufanya ngono pia kunaweza kusababisha maambukizi ya UTI, lakini si lazima mpaka uwe mwenye kupenda ngono sana ndio uweze kupata maambukizi haya. Wanawake wote wako katika hatari ya kuambukizwa UTI kutoka na mfumo wao wa uzazi ulivyo. Kwa upande wa wanawake, mrija wa mkojo huwa uko karibu sana na njia ya haja kubwa. Na ufunguzi wa urethra ni karibu na kibofu. Hii hurahisisha bakteria walio karibu na njia ya haja kubwa kuingia kwenye mrija wa mkojo na kusafiri hadi kwenye kibofu cha mkojo.
  • Maambukizi Kwenye Mrija Wa Mkojo: Aina hii ya UTI inaweza kutokea wakati bakteria wanaokuwa kwenye utumbo kusafiri kutoka kwenye njia ya haja kubwa na kuja kwenye mrija wa mkojo au njia ya mkojo Maambukizi ya kwenye njia au mrija wa mkojo yanaweza pia kusababishwa na  magonjwa ya zinaa. Bakteria hao ni pamoja na, kisonono, pangusa (Chlamydia) na mycoplasma. Hii inaweza kutokea kwa sababu mirija ya mkojo ya wanawake iko karibu na uke.

Je, Madhara Yake Ni Nini?

Unapotibiwa kwa usahihi na kwa ufasaha, maambukizi ya ya kwenye njia ya mkojo husababisha matatizo  mara chache sana. Lakini usipofanya matibabu mapema, basi UTI inaweza kusababisha matatizo makubwa ya afya.

Matatizo ya UTI yanaweza kuwa pamoja na:

  • Maambukizi ya mara kwa mara, ambayo inamaanisha una UTI mbili au zaidi ndani ya miezi sita au mitatu au zaidi ndani ya mwaka mmoja. Wanawake wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya mara kwa mara.
  • Uharibifu wa kudumu wa figo kutokana na maambukizi kwenye figo kwasababu ya UTI ambayo haijatibiwa.
  • Kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo au mtoto anapozaliwa  kabla ya wakati pale UTI inapotokea wakati wa ujauzito.
  • Mrija wa mkojo kuwa mfinyu kwa wanaume  kwa wanaume kutokana na kuwa na maambukizi ya mara kwa mara ya UTI.
  • Kuvimba kwa tezi dume

Je, Nini Suluhisho Lake?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa maambukizi mbalimbali katika njia ya mkojo. Unataka huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626.

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Comments

Popular posts from this blog

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa