Zijue Sababu Zinazopelekea Mlango Wa Kizazi Kulegea
Mlango wa kizazi kulegea, pia huitwa mlango wa kizazi kutokuwa na uwezo, ni hali ambayo hutokea pale tishu dhaifu za mlango wa kizazi zinaposababisha au kuchangia kujifungua mtoto kabla ya muda wake au kuharibika kwa mimba.
Kabla ya ujauzito, mlango wako wa kizazi, yaani sehemu cha chini ya mji wa mimba ambayo hufunguka kwenye uke kwa kawaida hujifunga na kukaza. Kadiri ujauzito unapoendelea na unajiandaa kujifungua, mlango wa kizazi hupungua polepole, hupungua kwa urefu(effaces) na hufunguka(dilates). Kama una mlango wa kizazi uliolegea, basi mlango wako wa kizazi unaweza kuanza kufunguka muda sio mrefu, na kukufanya ujifungue mapema mno kabla mtoto hajakamilisha miezi yake.
NUKUU: Mlango wa kizazi uliolegea unaweza kuwa vigumu kuupima na kuutibu. Kama mlango wako wa kizazi ukianza kufunguka mapema, au kama una historia ya madhaifu ya kizazi, basi daktari wako anaweza kupendekeza dawa ya kuzuia wakati wa ujauzito, kufanya vipimo vya ultrasound mara kwa mara au njia ambazo hufunga mlango wa kizazi kwa kushona kabisa(cervical cerclage).
Je, Nini Husababisha Mlango Wa Kizazi Kulegea?
Watalaam wa huduma ya afya hawajatambua sababu halisi ya mlango wa kizazi kulegea. Hata hivyo wanajua mambo fulani yanayoweza kukuweka hatarini. Mambo hayo ni kama haya yafuatayo:
- Uharibifu kwenye mlango wako wa kizazi
- Kufanyiwa upasuaji wa mlango wa kizazi hapo awali
- Kuzariwa na mlango wa kizazi usiokuwa na umbo la kawaida
- Mjiwa wa mimba usio na umbo la kawaida
- Utoaji mimba mara kwa mara.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Kama una mlango wa kizazi uliolegea, unaweza usiwe na dalili au ishara zozote wakati wa ujauzito. Baadhi ya wanawake wanakuwa na masumbufu ya kawaida au kutokwa na matone ya damu kwa muda wa siku kadhaa au majuma yanapoanza kati ya majuma 14 au 20 ya ujauzito.
Kwahiyo kuwa makini sana kwa mambo haya yafuatayo:
- Kuhisi msukumo kwenye nyonga
- Maumivu mapya ya mgongo
- Maumivu kwenye tumbo la chini
- Badiriko kwenye ute unaotoka ukeni
- Kutokwa na damu nyepesi ukeni
Je, Madhara Yake Yanakuwaje?
Mlango wa kizazi uliolegea huleta hatari kwenye ujauzito wako, hasa wakati mimba inapoanza kufikisha miezi minne. Hatari hizi ni pamoja na:
- Kujifungua kabla ya muda kuwadia
- Mimba kuharika
Ndugu msomaji katika makala hii naomba niishie hapa, nikaribishe kipindi cha maswali, karibu sana.
Je, Unahitaji Huduma? Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670 au 0712181626.
Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP tukakuunganisha na darasa letu ili upate mafunzo zaidi ya afya.
Karibuni sana!
Comments
Post a Comment