Fahamu Kwanini Ugonjwa Wa PID Husababisha Mimba Kutunga Nje Ya Kizazi

Katika wajawazito 100, mmoja anaweza kuwa na tatizo la kupata mimba nje ya kizazi. Hali hii humaanisha kwamba, yai lililorutubishwa tayari limeshachomekwa  katika tishu nje ya mfuko wa kizazi(uterus) badala ya ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus). Yai hili huendelea kukua ndani ya kiini tete(embryo) ambapo limeshapachikwa. 

NUKUU: Mara nyingi mimba zinazotunga nje ya kizazi huwa haziwezi kukua mpaka mwisho wa ujauzito, na hivyo huweza kuleta hatari kwa afya ya mama hasa pale inapopasuka na kuvujisha damu tumboni mwa mama.

Je, Hali Ya Mimba Kutunga Nje Ya Kizazi Inatokeaje?

Kwa kawaida mbegu ya mwanaume na yai la mwanamke hukutana katika mirija ya uzazi (Fallopian tubes) na hapo ndipo mimba hutungika. Kiinitete husafri polepole kwenda kwenye mji wa uzazi ambako hujipandikiza kwenye ukuta wa uzazi na mimba huanza kukua. Katika ugonjwa huu wa mimba kuwa nje ya kizazi (ectopic pregnancy) mbegu za mwanaume na yai la mwanamke huungana ili  kutengeneza kiinitete. Badala ya kupandikizwa kwenye tumbo la uzazi, kiinitete huenda kujipandikiza sehemu nyingine tofauti na mji wa uzazi. Kinaweza kujipandikiza kwenye mirija ya uzazi, ovari, kwenye shingo ya uzazi na ndani ya tumbo la uzazi(abdominal cavity). Mimba nyingi za nje ya kizazi hujipandikiza kwenye mirija ya uzazi ambapo huwa na hatari ya kupasuka kadri mimba inavyokua.

 

NUKUU: Mara chache sana mimba zinazotunga nje ya kizazi huweza kukua mpaka mwisho, nyingi huishia kupasuka na kuondolewa kwa upasuaji.

Je, Nini Husababisha Mimba Kutunga Nje ya Kizazi?

Zifuatazo ndio baadhi ya sababu zinazochangia kutokea mimba kutunga nje ya kizazi.

  • Umri wa zaidi ya miaka 40 kwa mwanamke
  • Kutoa mimba zaidi ya 3
  • Upasuaji wa mirija ya mirija ya uzazi mara unapokuwa na tatizo
  • Maambukizi ya magonjwa katika via vya uzazi au PID

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Kufuatia wiki kadhaa baada ya kukosa siku zako za hedhi, hutokea dalili zifuatazo:

  • Kuchelewa kuingia katika kipindi cha hedhi
  • Kupata maumivu ya tumbo chini ya kitovu au kiuno, ambayo yanaweza kuwa upande mmoja.
  • Maumivu yanaweza kuja na kuacha, au kuwa makali sana kiasi cha kushindwa kuvumilia.
  • Kutokwa damu ukeni hasa baada ya tendo la ndoa, na mara nyingi inaweza ikatoka kidogo kidogo.
  • Damu inaweza kuwa nyepesi au nzito nyeusi.

Wakati mwingine unaweza usipate dalili zozote, tatizo likagunduliwa wakati wa kipimo cha ultrasound. Kuna baadhi ya watu wanaweza wasipate dalili zozote na mimba kukua nje ya kizazi mpaka wakati wa kujifungua kukaribia.

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa visababishi vya mimba kutunga nje ya kizazi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Comments

Popular posts from this blog

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa