Fahamu Mambo 5 Yanayosababisha Vidonda Vya Tumbo

Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcers) ni ugonjwa unaompata mtu ambapo kunatokea vijitundu au michubuko katika kuta za ndani za viungo vya mfumo wa uyeyushaji chakula. Michubuko hiyo huweza kutokea katika eneo la mfuko wa chakula (stomach) au duodenum au katika eneo la koo. Inakadiriwa kuwa asilimia 5 hadi 10 ya watu hupatwa na ugonjwa huu angalau mara moja katika maisha yao. Huu ni ugonjwa ambao unaweza kumrudia mtu baada ya kupona endapo chanzo chake hakikudhibitiwa. Ndio maana Yesu alipomtibu yule mgonjwa akamwambia yule mgonjwa, “Enenda lakini usitende dhambi tena…”. 

NUKUU: Kama ugonjwa huu utamrudia mgonjwa , mtu huyu atakuwa amejiweka kwenye hatari kubwa ya kupata madhara makubwa zaidi kama kutokwa na damu au kutokea tundu kubwa katika kuta za mfuko wa tumbo.

 Je, Nini Husababisha Vidonda Vya Tumbo?

Chanzo kikubwa cha ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori). Bakteria hawa huenezwa kwa kula chakula au kunywa maji machafu. Katika mwili wa binadamu bakteria hawa wapo katika mate na katika ute unaotanda juu ya kuta za utumbo mwembamba(duodenum) na mfuko wa tumbo la chakula.

NUKUU: Bakteria hao wa H pylori hutengeneza enzyme (urease) ambayo hupunguza makali ya tindikali katika tumbo. Tatizo hilo likitokea, tumbo hutengeneza tindikali zaidi na hii ndiyo husababisha michubuko katika kuta za tumbo na duodenum. Bakteria hawa pia hudhoofisha kinga ya tumbo na kusababisha maumivu mbalimbali kwa muhusika.

1. Madawa 

Inaonyesha kuwa matumizi ya madawa hasa ya vidonge ya muda mrefu husababisha vidonda vya tumbo. Dawa nyingi ambazo huweza kusababisha vidonda vya tumbo ni zile za kupunguza maumivu ya kichwa na maumivu mengine madogo madogo. Dawa hizo ni kama aspirin, diclofenac, naproxen, ibuprofen n.k. Dawa hizi hupunguza uwezo wa tumbo wa kutengeneza utando wa ute wa kulikinga tumbo hivyo kulifanya liweze kuliwa kirahisi zaidi na tindikali.

NUKUU: Dawa hizi pia hupunguza mtiririko wa damu kuelekea kwenye eneo la tumbo hivyo kupunguza uwezo wa tumbo wa kukarabati seli zilizoharibika.

2. Pombe Na Tumbaku:

 

Watu wanaokunywa pombe na wale ambao wanatumia tumbaku wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo.

 

3. Msongo Wa Mawazo: 

 

Haijabainishwa moja kawa moja kwamba msongo wa mawazo unaweza kusababisha vidonda vya tumbo, bali mtu mwenye vidonda vya tumbo atakuwa na hali mbaya zaidi pale atakapokuwa na msongo wa mawazo.

 

4. Njaa

 

Kushinda njaa kwa muda mrefu bila kula ama kutopangilia muda wa kula kumekuwa chanzo kikubwa cha watu wengi kupatwa na janga la vidonda vya tumbo. Watu wengi wanaokuwa busy sana tukianzia mashuleni hasa wanafunzi wa vyuo, na wafanya biashara wanaokuwa masokoni na sehemu mbalimbali inaonyesha kuwa hili ndo limekuwa janga kwao.

 

5. Matumizi Ya Vyakula Na Vinywaji

 

Inatambulika kuwa mazoea ya vyakula kama vile mkate mweupe, chapati, mandazi, na vyakula vyote vilivyokobolewa kama vile ugali wa sembe, nk, soda, juisi za viwandani, chips, ni moja ya visababishi vya janga hili la vidonda vya tumbo katika jamii leo.



Unaweza kuona hapo juu baadhi ya vyakula na vinywaji ambavyo ndio visababishi vya ugonjwa wa vodonda vya tumbo. 



Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

1. Maumivu Ya Tumbo 

Dalili ya kwanza kabisa ya ugonjwa huu ni maumivu ya tumbo ambayo yanaongezeka pale tindikali inapogusa eneo lililoathirika. Maumivu haya yanaweza kutokea sehemu yoyote kuanzia eneo la kitovuni hadi kwenye mifupa ya mabega na yanaweza kuchukua muda mfupi au kuendelea kwa saa chache. 

NUKUU: Maumivu husikika zaidi wakati tumbo ni tupu na huwa makali zaidi nyakati za usiku. Maumivu hupungua kwa muda mfupi baada ya kula chakula. Mgonjwa anaweza kupata nafuu kwa siku au wiki chache halafu maumivu hurudi tena.

2. Kutapika 

 

Dalili nyingine ya tatizo la vidonda vya tumbo ni kujisikia kutapika au kutapika baada ya kupata chakula.


3. Kukonda


Mtu mwenye vidonda vya tumbo hukosa hamu ya kula chakula na hukonda.

Dalili za ugonjwa huu  huweza kuwa mbaya zaidi kama vile kutapika damu, kutoa haja kubwa yenye rangi nyeusi au iliyochanganyikana na damu nyeusi na kusikia kichefuchefu.


Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa matatizo haya, kama unataka huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

 

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa