Madhara 8 Yatokanayo Na Kuchelewa Kula Usiku.
Kula usiku sana kuna madhara mengi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uzito na kuoza kwa meno, kwa sababu hii, unapaswa kudhibiti tamaa ya kula vitafunwa usiku.
Watu wengi wamekuwa na tabia ya kutokupika chakula jioni majumbani mwao, hivyo, wameona kuwa ni rahisi sana kula chipsi mayai, viazi vya kukaangwa, juisi, soda, mkate au biskuti. Lakini usiku ndio mtu anapopaswa kula mapema na kutumia mlo mdogo tu.
Lakini watu wengi hutumia siku hiyo kula chakula kidogo wakati wa kifungua kinywa (mlo wa asubuhi) au chakula cha mchana na kula vitafunio mchana (kama vile mikate, chapati, maandazi, keki na soda, nk), na inapofika jioni pia, napo wanakula mlo mkubwa lakini ukiwa na vyakula zaidi ya ina mbili, mfano; chipsi mayai, mishikaki, chipsi kuku na kachumbali, na bado anashushia juisi au soda.
Baadhi yetu tunahitaji kula chakula kikubwa wakati wa mchana, na kisha kuandaa mapema mlo wa jioni kabla jua halijazama.
Lakini sayansi imegundua idadi ya athari mbaya za vitafunio vya usiku wa manane, kulingana na ripoti hiyo, iliyochapishwa na Reader's Digest, na Alissa Schaff.
1. Madhara Kwenye Tumbo La Chakula
Kuchelewa kula au kula chakula chenye mafuta mengi husababisha kuingulia, maumivu makali ambayo wakati mwingine huambatana na uchungu au ladha kali ya asidi mdomoni. Kiungulia husababisha asidi kuvuja na kuingia kwenye koo la chakula au umio.
Mtu mmoja kati ya watano anaweza kupata hali hii na kuwa mbaya zaidi inapokuwa tatizo la tumbo kujaa gesi ambayo inaweza kusababisha baada ya muda fulani matatizo mbalimbali makubwa ya afya.
2. Unahifadhi Mafuta Mengi
Katika uchunguzi wa watu wazima 31 walio na uzito mkubwa na unene uliopitiliza, watafiti waligundua kuwa wale waliokuwa na mazoea ya kula chakula cha jioni mida ya usiku sana kuanzia saa tano hadi sita, walikutwa na tatizo la uzito mkubwa mno wa mwili na mafuta mengi mwilini kuliko wale waliokuwa wakila chakula hicho mapema.
3. Shinikizo La Juu La Damu (High Blood Pressure)
Kulingana na utafiti, inaonyesha kwamba kula usiku sana kunaweza kuongeza tatizo la shinikizo la juu la damu, haswa kwa wale ambao tayari wana shinikizo la damu.
Watafiti hao walifuatilia hali ya afya ya watu 700 wenye shinikizo la damu na kubaini kuwa waliokula saa mbili kabla ya kulala walikuwa na shinikizo la damu usiku ikilinganishwa na wale ambao hawakula chochote kabla ya kulala.
Ulaji wa usiku wa manane huongeza shinikizo la damu hasa chakula linapokuwa na chumvi nyingi, kwa sababu sodiamu ndicho kipengele kinachotia wasiwasi linapokuja suala la shinikizo la damu. Mtu anapochelewa kula chakula, yeye hukosa usingizi, hivyo basi hupata homoni nyingi za mafadhaiko kama vile adrenaline, ambayo huongeza shinikizo la damu.
4. Kukosa Usingizi
Usingizi usio na utulivu na unaoonekana kwa vipindi ni mojawapo ya madhara yanayokera kutokana na tabia ya kula usiku sana.Vyakula vyenye kafeini kama vile kahawa na chokoleti nyeusi vinaweza kuongeza hali ya kupata usingizi, huku vitafunwa vyenye wingi wa sukari au mafuta huuongezea mwili shughuli wakati wa kupumuzika. Kwa wale wanaougua kiungulia, mateso yao yanaweza kuongezeka maradufu, na kufanya usingizi wao kuwa mgumu zaidi na kudhoofisha umakini wao wakati wa siku inayofuata.
5. Kula Kwa Ulafi Mara Kwa Mara
Watu wengi wanapendelea kutazama chips za viazi au biskuti wanapotazama vyakula wanavyovitamani hushindwa kujizuia. Lakini mtaalamu wa lishe Top Dix anapendekeza kubadilisha vyakula hivi na kuchagua vyakula vyenye afya kama vile matunda, mboga za majani, nk.
6. Huharibu Meno Na Kukufanya Kushindwa Kutabasamu
Mwandishi alisema kuwa kula vitafunio usiku baada ya kumaliza hushindwa kusafisha meno. Kulingana na Chama cha Madaktari wa Meno cha Marekani, kinasema kwamba, kula vyakula vya vyenye kunata kwenye meno, kama vile matunda yaliyokaushwa au peremende, kunaweza kuharibu meno, kwa sababu vyakula hivyo hunata kwenye meno.
7. Kuharibu Mfumo Wa Usagaji Chakula
Kwa hivyo, unapolazimisha mwili wako kumeng’enya chakula, huku mfumo wenyewe ukionyesha muda umeenda, uko katika hatari ya kuharibu utendaji kazi wa mwili. Wakati wa usiku, mwili hutoa homoni ya melatonin, ambayo huchangamsha usingizi, lakini “wanasayansi wanaamini kwamba kula baada ya kuzarishwa kwa homoni hiyo kunaweza kuharibu mwili wako, jambo ambalo linaweza kusababisha kuongezeka kwa uzito.”
8. Mwili Kuongezeka Uzito
"Tukianza kula vitafunio, kunaweza kusiwe na ukomo tena katika kula vyakula vingine tunavyoweza kula. "Uzito kupita kiasi au kupungua kunahusiana na jumla ya idadi ya kalori tunayotumia kwa siku, wakati unaweza kula katika masaa ya kwanza ya usiku, lakini lazima uwe na uhakika kwamba utaacha kula kwa wakati fulani kwa sababu hiyo ni njia nzuri.
Rafiki msomaji, makala yetu inaishia hapa, nakaribisha kipindi cha maswali na maoni kutoka kwako.
Unahitaji katika huduma, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment