Mambo 5 Yanayosababisha Chango La Uzazi Kwa mwanamke.

Wanawake wenye tatizo la chango huwa wana mikazo ya tumbo la uzazi isiyo ya kawaida kutokana na mvurugiko wa kemikali mwilini. Kwa mfano, kemikali ya tezi ya prostaglandin hudhibiti mikazo ya tumbo la uzazi. Kwahiyo, utaona mwanamke anapokuwa hedhi au anapokaribia hedhi tumbo hukaza na kuuma kabisa.

NUKUU: Chango linaweza kusababishwa na maradhi mengine hasa endometriosis. Haya ni maradhi ambayo tishu za ndani ya ukuta wat umbo la kizazi hubadirika na kuota nje ya tumbo la uzazi. Endometriosis mara nyingi husababisha damu kuvuja kwa ndani, maambukizi Pamoja na maumivu makali ya nyonga.

Visababishi vingine vya chango ni Pamoja na:

  • Ugonjwa wa PID
  • Uvimbe wa fibroid
  • Mimba kutunga nje ya kizazi
  • Maambukizi
  • Mvurugiko wa hedhi, nk

Je, Dalili Zake Zikoje?

Zifuatazo ni dalili za chango. Hata hivyo, kila mtu anaweza akapata dalili tofauti.  Dalili zake zinaweza kuwa Pamoja na:

  • Tumbo la chini kukaza na kuuma
  • Maumivu makali tumbo la chini
  • Kiuno kuuma
  • Maumivu ambayo hupenya na kushuka mguuni
  • Kuhisi kichefuchefu
  • Kutapika
  • Kuharisha
  • Mwili kuchoka
  • Kukosa pumuzi
  • Kichwa kugonga, nk.

Dalili za chango zinaweza kuonekana kama dalili zingine au matatizo ya magonjwa. Mara nyingi unapoona hivi, jaribu kufika hospitali mapema ili upate vipimo.

Je, Viharatishi Vya Chango Ni Nini?

Mwanamke yeyote anapoendelea kuwa na chango, wanawake wengine wanaweza kujiongezea vihatarishi vya ugonjwa:

  • Wanawake wanaovuta sigara
  • Wanawake wanakunywa pombe
  • Wanawake wenye uzito mkubwa
  • Wanawake walioanza kuona hedhi kabla ya kufikisha umri wa miaka 11
  • Wanawake ambao hawajawahi kupata mimba

Je, Chango Linapimwa Kwa Njia Gani?

Ili kupima chango, daktari anapaswa abainishe historia ya ugonjwa wako na kuweza kufanya vipimo kamili vya ugonjwa wako. Vipimo vingine vinaweza kuwa Pamoja na:

1. Ultrasound

Kipimo hiki hutumia mawimbi ya sauit ya masafa marefu ili kutengeneza picha ya viungo vya ndani.

2. MRI(Magneti Resonance Imaging)

Kipimo hiki hutumia sumaku kubwa, masafa ya radio, na kumpyuta ili kutengeneza muonekano mzuri wa picha za viungo vya ndani ya mwili.

3. Laparoscopy 

Njia hii ndogo hutumia laparoscope. Huu huwa ni mrija mwembamba wenye lenzi na mwanga. Huingizwa baada ya kuchanwa kidogo kwenye ukuta wat umbo la chini. Kwa kutumia kipimo hiki ili kutazama ndani ya nyonga na eneo la tumbo la chini, daktari mara nyingi anaweza kutambua vivimbe visivyo vya kawaida.

4.  Hysteroscopy

Hiki ni kipimo cha kuona kwa macho kupitia njia ya mlango au shingo ya kizazi ndani ya tumbo la uzazi. Hutumia kifaa cha kuangalizia(hysteroscope) ambacho huzamishwa ndani ukeni.  

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa zenye uwezo wa kuondoa vyanzo vya chango la uzazi kwa mwanamke. Je, unahitaji huduma, basi tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa