Vyakula 6 Vilivyosindikwa Vitakavyokuua Polepole
Watu wengi siku hizi wamekuwa wakisikia kuhusu hatari za vyakula vilivyosindikwa na " vyakula vya kukaanga chap chap", ikiwa ni pamoja na hatari za vitambi, ugonjwa wa moyo na kisukari.
Hata hivyo, hata katika ulimwengu wa vyakula vilivyosindikwa, bado kuna baadhi ya vyakula ambavyo vina mafuta mengi na kalori ambazo zinapaswa kuepukwa kabisa.
Ifuatayo ni mifano kumi ya vyakula hivi visivyofaa kabisa kutumiwa kama chakula:
1. Burger
Katika kundi hili Burgerinaonekana kupendwa sana na watu hasa wanapotoka out siku za weekend au sikukuu. Lakini wengi hawajui kuwa huwa wanajiharibu wenyewe maana ina wingi wa mafuta na kalori nyingi.
Kwa kuwa inamfanya mlaji kuridhika kwamba ni chakula cha anasa, basi ina uwezo mkubwa wa kuongeza mafuta kugandamana kwenye kuta za mishipa ya damu, kuongeza shinikizo la damu na kuongeza hatari ya uharibifu wa moyo.
2. Pizza
Pizza ni chakula chenye mafuta mengi, nacho kinapendwa na watu wengi kwani hukitumia kama chakula cha starehe hasa wanapokuwa out vile vile siku za weekend au kwenye sikukuu. Pizza ina ukoko mzito ambao huongeza wanga zaidi na kuruhusu kiasi kikubwa cha mafuta.
3. Vyakula Vya Kigeni
Watu hufika mahotelini hasa beach wakiwa wawili mtu na mpenzi wake au wanaweza kuwa baba na watoto, na hivyo hupata sehemu ya kukaa na kuagiza vyakula vya kigeni, navyo huwa ni kama vile nyama ya kopo, maharage ya kopo, nk. Maharage na Vikolezo ni mojawapo ya vyakula vya kigeni vibaya zaidi vinavyopendwa kuliwa na watu wengi leo kama ulimbukeni fulani hivi, huku vikiwa vimejaa mafuta mengi na wingi wa sodiamu. Kundi hili la chakula ni baya sana kwani ndio chanzo cha magonjwa makubwa.
4. Vyakula Vya Kufungua Kinywa (Breakfast Foods)
Chapati, mikate myeupe na blue band, maandazi, Biscuit ni mojawapo ya njia mbaya zaidi za kuanzia siku. Ni aina mbaya sana kwa sababu aina hii inapotumiwa kwa wingi kila siku, husababisha magonjwa makubwa ikiwa pamoja na kudhoofisha ubongo.
5. Vyakula Vilivyowekwa Kwenye Makopo
Peaches wenyewe, kuwa matunda, inapaswa kuwa sahani yenye afya. Walakini, wakati viwanda vya vyakula vinapopakia vyakula kwenye kopo huku vikiwa vimetiwa sukari nyingi, basi virutubishi vya kawaida hutoweka na hatimaye bidha hujaa kalori kwa wingi zisizo za lazima. Ni hatari sana kuwa na mazoea ya kula vyakula vya kwenye makopo.
6. Vinywaji
Vinywaji vingi hasa vinavyotengenezwa viwandani bila shaka vinakuwa na vikolezo vingi vibaya kwani rangi na radha vyote huwa ni vya bandia. Mungu hataki vitu bandia anataka vitu halisi yaani vya asili. Epuka sana matumizi ya vinywaji hivi.
Ukweli ni kwamba ni vyema ukatumia vyakula vya asili kwa ajili ya kuandaa juisi au kinywaji chako kuliko kutumia vinywaji vya viwandani. Pia itakusaidia kuepuka gharama na matokeo mabaya kama vile magonjwa, nk.
Ubarikiwe sana rafiki msomaji, nikukaribishe kwa maswali yako na maoni yako.
Unahitaji ushauri au huduma, basi nipigie: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment