Zifahamu Hatua 4 Za Vidonda Vya Tumbo
Mgonjwa wa vidonda vya tumbo katika hatua ya kwanza asipopata tiba, tindikali nyingi iliyozalishwa tumboni hushuka na kuingia kwenye utumbo mdogo na kuharibu mfumo wa mmeng’enyo au usagaji wa chakula kwa kuwa vimeng’enyo vya utumbo mdogo hushindwa kufanya kazi kwenye mazingira ya tindikali.
NUKUU: Hali hii husababisha kuharibika kwa uteute wa sehemu hii ambao ndiyo ulinzi wa utumbo mdogo na matokeo yake ni mtu kuwa na vidonda tumboni pia kwenye utumbo mdogo yaani (duodenal ulcers). Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (stomach).
Dhana hii sio kweli kwani sehemu inayoathiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama duodenum. Dalili ya mwanzo kabisa ya ugonjwa ni ule uvimbe tuliosema unajitokeza sehemu ya ndani ya tumbo, yaani:
- Tumbo kujaa gesi,
- Kichefuchefu cha mara kwa mara,
- Kiungulia kikali na kutapika kwa baadhi ya wagonjwa.
Hatua Ya Pili:
Hatua ya pili vidonda hujitokeza taratibu sehemu zenye uvimbe na vidonda hivyo huongezeka na kuwa vikubwa. Na katika hatua hii mgonjwa huwa anapatwa dalili zifuatazo:
- Maumivu makali ya tumbo yanayodumu kwa muda mrefu,
- Kujaa gesi,
- Kukosa hamu ya kula,
- Choo kuwa kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu.
NUKUU: Hali hii ya kukosa choo kwa muda mrefu hujulikana kama (chronic dyspepsia) yaani kushindwa kufanyakazi kwa mfumo wa kusaga au kumeng’enya chakula kutokana na tindikali nyingi inayozalishwa tumboni.
Tindikali hiyo huingia kwenye mzunguko wa damu, mgonjwa hujisikia uchovu na kizunguzungu, homa hasa nyakati za jioni na pia mgonjwa hupoteza uzito wa mwili. Katika hatua hii tindikali husababisha magonjwa ya ini na figo kwa kuwa tayari iko katika mfumo mzima wa mwili kupitia mzunguko wa damu.
Hatua Ya Tatu:
Ni kwamba vidonda vikubwa hupasua mishipa midogo ya damu na kusabababisha damu kuvujia tumboni na kubadilisha rangi ya choo cha mgonjwa kuwa ya kahawia.
NUKUU: Damu nyingi ikivujia tumboni mgonjwa hutapika na kuharisha damu, hali hii husababisha mgonjwa kuishiwa damu mara kwa mara, maumivu makali ya tumbo huongezeka, homa, maumivu ya viungo na kukosa hamu ya chakula.
Hatua Ya Nne:
Hatua ya nne ya vidonda vya tumbo ni mtu kukumbwa na saratani ya utumbo na ni hatua ambayo ni ya hatari sana kwa kuwa vidonda hutengeneza tundu katika tumbo au utumbo mdogo na kusababisha kuoza kwa viungo muhimu vya ndani na matokeo yake ni saratani au kansa ya utumbo.
Je, Nini Suluhisho Lake?
James Herbal Clinic tunayo dawa nzuri kabisa yenye uwezo wa kuondoa na kukomesha kabisa vidonda vya tumbo. Unahitaji huduma na ushauri, tupigie: 0768 559 670/0712 181 626.
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment