Haya Ndio Baadhi Ya Aina Ya Magonjwa Ya Kibofu Cha Nyongo
Je, Unazifahamu Kazi Za Kibofu Cha Nyongo?
Kibofu cha nyongo kina urefu wa inchi 4, na ni kiungo chenye umbo la peasi. Kiungo hiki kiko chini ya ini sehemu ya juu ya tumbo lako.
Kibofu hiki huhifadhi nyongo, mchanganyiko wa majimaji, mafuta, pamoja na lehemu (cholesterol). Nyongo husaidia kuyeyusha mafuta yanayokuwa kwenye chakula chenye mafuta pale kinapoingia tumboni mwako.
NUKUU: Kibofu cha nyongo hutoa nyongo na kuiingiza kwenye utumbo mwembamba. Hali huruhusu vitamini za mafuta mumunyifu (fat-soluble vitamins) pamoja na virutubishi kuweza kunyonywa kwa urahisi na kuingizwa kwenye mkondo wa damu.
Je, Dalili Za Matatizo Ya Kibofu Cha Nyongo Zinakuwaje?
Matatizo ya kibofu cha nyongo huwa yanakuwa na dalili zenye kufanana. Dalili hizi huwa kama ifuatavyo;
1. Maumivu
Dalili ya kwanza kabisa ya kibofu cha nyongo huwa ni maumivu. Maumivu haya kwa kawaida hujitokeza katikati pembeni mwa tumbo lako kuelekea juu. Yanaweza kuwa maumivu ya kawaida au ya kwenda na kurudi, au yanaweza kuwa makali kabisa tena ya mfululizo. Baadaye maumivu yanaweza kuanza kupenya katika maeneo mengine ya mwili, hasa mgongoni pamoja na kifuani.
2. Kichefuchefu
Kichefuchefu na kutapika huwa ni dalili za kawaida za matatizo yote ya kibofu cha nyongo. Hata hivyo, ni ugonjwa sugu tu wa kibofu cha nyongo ndio unaweza kusababisha matatizo ya uyeyushaji chakula tumboni, kama vile tumbo kujaa gesi na kuongezeka kwa tindikali.
3. Homa Au Baridi
Baridi au homa isiyoelezeka inaweza kuashiria kwamba wewe una maambukizi. Ikiwa kama una maambukizi, basi unahitaji tiba kabla hajawa mbaya zaidi na kuwa hatari. Maambukizi yanaweza kuwa tishio katika maisha yako kama yakienea katika sehemu zingine za mwili wako.
4. Hali Sugu Ya Kuhara
Kwenda choo mara nne kwa siku kwa muda wa miezi mitatu yaweza kuwa ishara ya ugonjwa sugu wa kibofu cha nyongo.
5. Homa Ya Manjano
Ngozi inapokuwa ya kawahawia, au ya njano, yaweza kuwa ishara ya mawe kwenye mrija wa nyongo. Mrija wa nyongo ni njia ambayo hutoka kwenye kibofu cha nyongo kuelekea kwenye utumbo mwembamba. Tutajifunza baadaye pia juu ya tatizo hili.
6. Choo Au Mkojo Sio Wa Kawaida
Choo chepesi au mkojo wa kijivu huwa ni ishara tosha za kuonyesha kuwa mrija wa nyongo umeziba. Tutajifunza baadaye pia juu ya tatizo hili.
Magonjwa Mabaya Ya Kibofu Cha Nyongo
Ugonjwa wowote ambao huathiri kibofu chako cha nyongo huonekana kuwa ni ugonjwa wa kibofu cha nyongo. Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa ya kibofu cha nyongo.
1. Uvimbe Wa Kibofu Cha Nyongo: Uvimbe wa kibofu cha nyongo kitaalamu tunaita, “cholecystitis”. Hali hii inaweza kuwa ya muda mfupi au ikawa ya muda mrefu. Uvimbe wa muda mrefu huwa ni matokeo ya mashambulio ya uvimbe wa kujirudiarudia. Uvimbe hatimaye unaweza kuharibu kibofu cha nyongo, na kukifanya kipoteze uwezo wake wa kufanya kazi kama kinavyotakiwa.
2. Mawe: Mawe huwa ni madogo madogo, matabaka magumu ambayo hujengeka kwenye kibofu cha nyongo. Matabaka haya yanaweza kuendelea kukua kwa miaka kadhaa bila kugundulika.
Kusema kweli watu wengi wana mawe ya figo na huwa hawajali kabisa. Baadaye huwa wanasababisha matatizo wenyewe, hasa maambukizi, uvimbe na maumivu. Mawe ya figo husababisha kibofu cha nyongo kuvimba.
Mawe mara nyingi huwa ni madogo sana, hayana upana mkubwa sana. Hata hivyo, yanaweza kukua na kuongezeka sentimita kadhaa. Baadhi ya watu wanaweza kuwa na jiwe moja, na wengine wakawa na mawe mengi. Mawe yanaweza kuanza kuziba njia kutoka kwenye kibofu cha nyongo, kadiri mawe yanavyozidi kuongezeka kuwa makubwa.
Mawe mengi hujengeka kutokana na lehemu(cholesterol) inayokuwa kwenye nyongo ya kibofu. Aina nyingine ya jiwe hujengeka kutokana na Calcium bilirubinate. Hii ni kemikali ambayo huzarishwa wakati mwili unapoyeyusha chembe nyekundu za damu. Aina hii yam awe huwa ni adimu.
3. Mawe Kwenye Mrija Wa Nyongo: Wakati mawe yanapojitkeza kwenye mrija wa nyongo, kitaalamu hufahamika kama, “choledocholithiasis.” Nyongo hutolewa kwenye kibofu cha nyongo, hupita kwenye mirija midogo, na kuingizwa kwenye mrija wa nyongo. Baadaye huingia kwenye utumbo mwembamba.
Kwa upande mwingine, mawe ya nyongo yanayokuwa kwenye mrija wa nyongo huwa ni mawe ambayo huendelea kwenye kibofu cha nyongo na baadaye hupitishwa kwenye mrija wa nyongo. Aina hii ya mawe inaitwa, “ Secondary Stone.”
Wakati mwingine mawe hujengeka kwenye mrija wa nyongo wenyewe. Mawe haya huitwa, “Primary stones.” Aina hii yam awe huwa ni nadra sana lakini inaweza kusababisha maambukizi kuliko aina ile ya Secondary stone.
4. Ugonjwa Wa Kibofu Cha Nyongo Bila Mawe: Mawe hayasababishi kila aina ya tatizo la kibofu cha nyongo. Ugonjwa wa kibofu cha nyongo bila mawe pia hujulikana kama, “acalculous”, unaweza kutokea. Katika tatizo hili, unaweza ukaona dalili zinazoambatana mawe bila kuwa na mawe.
5. Maambukizi Katika Mrija Wa Nyongo: Maambukizi yanaweza kuendelea ikiwa kama mrija wa nyongo unaziba. Matibabu ya hali hii yanapatikana ikiwa kama maambukizi yatagundulika mapema. Kama hayatagundulika, basi maambukizi yanaweza kuenea na kuwa hatari.
6. Kibofu Cha Nyongo Kujaa Usaha: Asilimia chache ya watu wenye tatizo la mawe kwenye kibofu wanaweza pia kuwa na tatizo la usaha kwenye kibofu cha nyongo. Hali hii kitaalamu tunaita, “ empyema.” Usaha huwa ni mchanganyiko wa chembe nyeupe za damu, bakteria pamoja na tishu zilizokufa. Kuwepo kwa usaha, pia hufahamika kama jipu, husababisha maumivu makali sana ya tumbo. Kama tatizo la mkusanyiko wa usaha halitafanyiwa uchunguzi na kutibiwa, yaweza kuwa tishio la uhai wako kadiri maambukizi yatakavyozidi kuenea katika maeneo mengine ya mwili wako.
7. Jiwe La Nyongo Kuziba Utumbo Mkubwa Au Mdogo: Jiwe la nyongo linaweza kuingia kwenye utumbo na kuziba. Hali hii, inayojulikana kama gallstone ileus, ni nadra lakini inaweza kusababisha kifo. Huwatokea zaidi watu walio na umri zaidi ya miaka 65.
8. Kibofu Cha Nyongo Kilichotoboka: Ukisubiri kwa muda mrefu kutafuta matibabu, mawe kwenye nyongo yanaweza kusababisha kibofu cha nyongo kutoboka. Hii ni hali ya kutishia maisha. Ikiwa hali hii haijagunduliwa, maambukizo hatari, yanaweza kuendelea kuenea tumboni.
9. Ukuta Wa Ndani Wa Kibofu Cha Nyongo Kuwa Mgumu: Mfuko wa nyongo wenye afya una kuta zenye misuli migumu. Baada ya muda, machicha ya kalsiamu yanaweza kufanya kuta za kibofu cha nyongo kuwa ngumu, na kuzifanya kuwa imara. Hali hii inaitwa porcelain gallbladder. Ikiwa una hali hii, uko na hatari kubwa ya kuendeleza ugonjwa wa saratani ya kibofu cha nyongo.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa za asili zenye uwezo kmkubwa wa kuondoa magonjwa kwenye kibofu cha nyongo. Unahitaji huduma au ushauri, basi tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment