Haya Ndio Mambo 6 Yanayofanya Mirija Ya Uzazi Kuziba
Hali ya kujaa maji kwa mirija ya uzazi ya wanawake huitwa kitaalamu, “hydrosalpinx”. Ni tatizo ambalo hujitokeza kwa wanawake kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo yamekaa muda mrefu bila kutibiwa, kama vile kisonono, pangusa, malengelenge, nk, ambayo kwa ujumla tunaweza kuita maambukizi katika via vya uzazi yaani PID (pelvic inflammatory disease), bila shaka tutayazungumzia baadaye katika makala zinazofuata kwa kuchanganua ugonjwa mmoja baada ya mwingine na tutaona madhara yake na dalili zake pia. Mara nyingi matatizo haya husababisha tatizo la ugumba na maumivu ya kiuno.
NUKUU: Mirija ya uzazi hujishikiza upande wa kulia na kushoto mwa tumbo la uzazi, nayo hupitisha mayai kila mwezi kutoka kwenye ovari ama kifuko cha yai, kwenda kwenye mji wa uzazi. Urutubishaji wa yai la uzazi hutokea katika mirija hii.
Je, Nini Chanzo Cha Mirija Ya Mayai Kuziba?
Mara nyingi mirija ya uzazi kuziba hutokana na magonjwa mengi nayo huwa kama ifuatayo ;
- Maambukizi katika via vya uzazi au PID(Pelvic inflammatory disease)
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
- Utoaji mimba(abortion)
- Upasuaji maeneo ya kiunoni (pelvic surgery)
- Uvimbe mkusanyiko wa majimaji au usaha ambao huonyesha uvimbe mwishoni mwa mrija wa uzazi(hydrosalpinx).
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo yamekaa muda mrefu bila kutibiwa kama vile kisonono na klamidia au pangusa.
NUKUU: Hali zote hizo zinaweza kuathiri moja kwa moja mirija ya uzazi au eneo hilo la mwili wako. Vile vile hali hizi zinaweza kusababisha michubuko au jeraha ambazo zinaweza kuziba mirija ya uzazi.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Wanawake wengi wanaweza wasiwe na dalili zozote, isipokuwa kupata matatizo katika kupata mtoto. Dalili zinazojitokeza mara nyingi huwa ni;
- Uchafu kutoka sehemu za siri.
- Kuhisi maumivu katika nyonga au tumbo
- Kutokushika ujauzito
- Maumivu ya kiuno, nayo hujitokeza mara kwa mara hasa siku chache kabla au baada ya kuingia kwenye hedhi.
NUKUU: Wakati mwingine mrija ulioziba unaweza kusababisha yai lililorutubishwa lishindwe kusafiri. Hali hii hujulikana kama mimba iliyotunga nje ya kizazi.
Lakini mimba iliyotunga nje ya kizazi inaweza isionyeshe dalili na mara nyingi hupimwa kwa kupiga mionzi. Hata hivyo, baadhi ya wanawake wanaweza kupata dalili za ujauzito, kama vile tumbo kuuma maeneo ambapo mimba imetunga, au kutokwa damu ukeni. Mwanamke yeyote anayehisi kuwa ana tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi anapaswa kutafuta huduma ya tiba haraka.
Je, Unawezaje Kuligundua Tatizo Hili?
Kuna vipimo kadhaa vya kuwezesha kujua kama mirija yako ya uzazi imeziba na kujaa maji, nayo ni;
1. Hysterosalpingogram(HSG)
Hii ni aina maalumu ya X-ray ya kiuno, ambayo kimiminika maalumu huingizwa ndani ya mji wa uzazi kwa kupitia shingo ya uzazi. Kama mirija haijaziba, kimiminika huweza kupita mpaka ndani ya kiuno na kama imeziba, kimiminika hicho hushindwa kupita. Hii itaonekana kwenye hiyo hysterosalpingogram.
2. Ultrasound Ya Kiunoni (Pelvic Ultrasound)
Ultrasound itaweza kuonesha kama mirija yako imeziba na kujaa, na ukubwa wake. Pia itaweza kuonesha kama kuna matatizo mengine kwenye via vya uzazi vya ndani.
3. Upasuaji wa Tumbo(Laparoscopy):
Upasuaji huu hufanyika kwa kutumia mirija maalumu yenye kamera ili kutazama mirija hiyo. Matundu mawili hutobolewa tumboni ili kupitisha mirija hii.
Tatizo Hili Likitibiwa, Je, Mama Anaweza Kupata Ujauzito?
NUKUU: Na ieleweke kuwa, tatizo hili likitibiwa unaweza ukapata ujauzito. Lakini pale mirija inapokuwa imeharibika sana uwezekano wa kupata ujauzito huwa ni mdogo kwa mwanamke.
James Herbal Clinic tuna dawa za asili zenye uwezo wa kuondoa tatizo hili bila kufanya upasuaji kwani zina uwezo wa kunyonya majimaji yanayosababisha mirija kutuna, pia vimelea wote wanaosababisha tatizo hilo, nazo ni MULTI-CURE POWDER, CARD HERB na VITAMAKA.
Je, Nini Madhara Ya Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi?
Mfumo wa uzazi wa mwanamke una vifuko vya mayai(ovaries), mfuko wa uzazi(uterus), pamoja na mirija ya uzazi(fallopian tubes). Ikiwa kama tiba yoyote itaharibu maeneo haya matatu, inaweza kusababisha ikawa vigumu kushika mimba.
Kumbuka kila kifuko cha yai kimeshikamana na mfuko wa uzazi(uterus) kupitia mrija wa uzazi. Vifuko vya mayai huhifadhi mayai na kuyaachilia pale yanapopevuka. Ni utaratibu wa mfumo wa mwili kwamba kifuko kimoja cha yai huachilia yai kila. Kwa mfano, kifuko cha kulia kinaweza kuachilia yai kwa muda wa miezi mitatu mfululizo, na baadaye mfuko wa kushoto ukaanza kuachia yai mwezi unaofuata.
NUKUU: Kama mrija mmoja wa uzazi utaziba, kunaweza kukawa bado na uwezekano wa yai kurutubishwa, lakini kama mirija yote itaziba, kutakuwa na changamoto kubwa mno katika urutubishaji wa mayai.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tuna dawa za asili zenye uwezo wa kuondoa tatizo hili bila kufanya upasuaji kwani zina uwezo wa kunyonya majimaji yanayosababisha mirija kutuna, pia vimelea wote wanaosababisha tatizo hili.
Je, Unatahitaji Huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626. Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ukajiunga na darasa letu la masomo ya afya.
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment