Je, Vidonda Vya Tumbo Vinaweza Kusababisha Damu Kuvuja Tumboni?

 Neno "ulcers" linamaanisha kidonda kisichopona haraka. Ikiwa kidonda kinaendelea kwenye maeneo ya mshipa wa damu, basi inaweza kusababisha damu kutoka. Kutokwa na damu nyingi kwenye kidonda cha tumbo inapaswa kufanyiwa huduma ya dharura haraka kwani inaweza kusababisha upotezaji wa damu na hatimaye kifo.

Mara nyingi, watu wanapotaja kidonda, wanamaanisha vidonda vya tumbo, vinavyoendelea katika njia ya utumbo. Neno "peptic" linamaanisha kuwa inahusiana na asidi.

Vidonda vya tumbo vinaweza kutokea kwenye tumbo, utumbo mwembamba chini ya tumbo, au umio (koo la chakula) juu ya tumbo.

Wakati mwingine, vidonda vya tumbo vinaweza kutokwa na damu. Madaktari hutaja haya kama vidonda vya tumbo vinavyotoa damu. Kutokwa na damu nyingi, kunaweza kutishia uhai wa mgonjwa. Kutokwa na damu kidogo kwenye kidonda kwa kawaida sio vibaya na inaweza kutibika hali hiyo bila kuhangaika.

Baadhi ya mambo muhimu kuhusu vidonda vya tumbo vinavyotoa damu  ni pamoja na:

  • Dalili hutofautiana kwa zaidi. Hasa, kuna maumivu katika tumbo la juu au tumbo la chakula
  • Maambukizi na baadhi ya madawa yanaweza kusababisha vidonda vya damu, kwa mfano madawa ya kupunguza maumivu kama asprin, declophenac, panadol, nk
  • Kwa kutumia matibabu sahihi, hasa tiba za asili madaktari wanaweza kuponya vidonda vya damu.
  • Utambuzi na matibabu ya vidonda vya tumbo vinavyotoa damu kawaida huhusisha kipimo cha endoscopy.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Vidonda vya tumbo vinaweza kuwa vigumu kuvitambua kwa sababu baadhi ya watu huwa hawaonyeshi dalili. Wale ambao hupata dalili mara nyingi huziona kabisa. Dalili hizi ni pamoja na: 

  • Maumibu makali amaeneo ya tumbo la juu, ambayo yanweza kuwa mabaya zaidi baada ya kula au wakati tumbo linapkuwa tupu
  • Kuhisi kichefuchefu, kutapika
  • Kuhisi kushiba au tumbo kujaa

Ikiwa vidonda vya tumbo vikianza kutokwa na damu, mtu anaweza kugundua:

  • Kinyesi cheusi chenye utelezi
  • Kinyesi cheusi na chenye damu
  • Matapishi yenye rangi kama ya kahawa ambayo yana damu ndani yake
  • Kuzimia au kichwa kuuma sana.

Mtu aliye na mojawapo ya dalili hizi anapaswa kutafuta huduma ya matibabu ya dharura. Kidonda kikali kinachovuja damu kikiachwa bila kutibiwa kinaweza kusababisha upungufu wa damu haraka na hata kifo.

Je, Chanzo Chake Ni Nini?

Tumbo hutoa asidi yenye nguvu ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya umeng’enyaji chakula. Asidi hii kwa kawaida haiharibu njia ya usagaji chakula kwa sababu ya utando wake unaokuwa kwenye ukuta wa mfuko wa chakula.

Hata hivyo, katika baadhi ya matukio, mwili hutoa asidi nyingi ya tumbo, na hiyvo, utando au uteute unaokuwa kwenye ukuta wa mfuko wa chakula (stomach) huharibika. Hali hii inapotokea, asidi inaweza kuharibu utando wa njia ya utumbo na kusababisha kidonda (ulcers). 

Vidonda vingi vya tumbo vina visababishi mbalimbali vinavyokuwa wazi, kama vile;

  • ulaji wa vyakula vilivyokobolewa,
  • ugali wa sembe,
  • chapati, maandazi,
  • mikate myeupe,
  • chips na soda mara kwa mara,
  • pilau kila siku, 
  • kuchelewa kula, 
  • kutumia pilipili sana, nk

Sababu fulani zinaweza kuongeza hatari ya mtu ya kuendeleza ugonjwa huu.

Je, Madhara Yake Ni Nini?

Kutibu haraka vidonda vya tumbo, hasa vinavyotoa damu, ni njia bora ya kuepuka madhara baadaye katika mwili wako. Ikiwa mtu hatafuti matibabu ya vidonda, hali fulani zinaweza kutokea, kama vile:

  • Damu kuvujia tumboni
  • Tumbo kuvimba
  • Chakula kutokumeng’enywa tumboni, hii ni hatari sana

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa zenye uwezo wa kuotokomeza vidonda vya tumbo na madhara yake. Ukiwa unahitaji huduma na ushauri basi, tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Dalili 3 Za Ugonjwa Wa Chembe Ya Moyo (Angina Pectoris)

Jinsi ya Kuondoa Sumu Kwenye Kongosho Lako Kwa Njia Ya Asili Kwa Kutumia Aina Tatu Tu Za Juisi!

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea