Jinsi Ya Kuandaa Chapati Ya Brown Ya Kusukuma.

Chapati ya brown ni chapati inayoandaliwa kwa kutumia unga wa ngano ambayo haijakoborewa kama unavyoona kwenye picha hapo chini.

Je, Unaandaaje Chapati Hii?


 MAHITAJI

  • Unga wa ngano kilo 1
  • Mafuta ya kupikia au siagi vijiko vya chakula (tablespoon) 10
  • Sukari au asali kijiko 1 cha chakula
  • Chumvi kijiko cha chai 1
  • Tui la nazi vikombe 3 na nusu
  • Mafuta ya kukaangia nusu lita

FaNUKUU: Ili kuifanya chapati iwe laini, chukua unga wa ngano ambayo haijakobolewa nusu kilo na unga wa ngano mweupe nusu kilo ili upate kilo 1. 

HATUA ZA KUFUATA

  •  Pima unga wa ngano na uchekeche vizuri
  • Weka chumvi, sukari au asali, tui la nazi na mafuta uchanganye vizuri,
  • Kanda unga kwa tui la nazi kwa dakika 8-10 au mpaka ulainike kabisa.
  • Kata madonge ya duara kwa kukadiria au pima gramu 120 kwa kila chapati.
  • Sukuma umbo duara kwa donge, paka mafuta kijiko kimoja cha chakula, kunja. Fanya hivyo kwa madonge yote.
  • Funika ziache kwa dakika 7
  • Weka kikaangomotoni na sukuma chapati duara la saizi ya kati.
  • Weka chapati kikaangoni, iache iive upande mmoja geuza upande wa pili bila kuweka mafuta kwenye kikaango,
  • Weka mafuta kijiko kimoja cha chakula kwa kila upande,
  • Kaanga mpaka ipate rangi ya hudhurungi (brown) toa weka kwenye sahani au bakuli pana
  • Fanya hivyo kwa chapati zote zilizobakia.

 




Mungu awabariki sana wapendwa na muwe na afya njema.

 

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa