Mambo 6 Yanayomfanya Mwanamke Kuhisi Maumivu Ya Tumbo Wakati Wa Hedhi Au Baada Ya Kutoka Hedhini

Wanawake wengi huhisi maumivu ya tumbo kabla au wanapokuwa hedhini. Lakini inaweza pia mwanamke akahisi maumivu ya tumbo anapokuwa hedhini. Maumivu haya mara nyingi huwa sio makali sana. Hata hivyo, ni muhimu kwamba unayafuatilia, hasa ikiwa kama yanakaa kwa muda mrefu. Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi inaweza kuwa ni dalili ya magonjwa mbalimbali.

Endelea kusoma Makala hii ujifunze dalili, visababishi, Pamoja na matibabu ya kukosa hedhi au kutokwa na damu ya hedhi nyingi kwa muda mrefu.

Je, Nini Visababishi Vyake?

Wakati mwingine maumivu ya tumbo baada ya hedhi huwa sio makali mno. Lakini kama una maumivu makali endelevu yanayodumu muda mrefu kuliko mzunguko wako wa hedhi, inaweza kuwa ishara kwamba una magonjwa kwenye tumbo lako la uzazi(uterus).

Hapa nitakuelekeza visababishi vya maumivu ya tumbo unapotoka hedhini:

1. Endometriosis

Endometriosis ni ugonjwa ambao hutokea pale seli zinazofanana na ukuta laini wa mji wa mimba (uterus) zinapoota nje ya mji wa mimba. Ugonjwa huu unaweza kusababisha maumivu makali kabla au wakati wa hedhi au baada ya hedhi.

Maumivu yanaweza kuambatana na uvimbe Pamoja na maumivu ya nyonga. Maumivu yanaweza kuwa makali na yanaweza kutokea wakati unaposhiriki tendo la ndoa au unapotoa haja kubwa au unapokojoa. Maumivu haya endelevu unaweza kuyahisi kiunoni mwako.

Dalili za ugonjwa wa endometriosis ni Pamoja na:

  • Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa
  • Maumivu kwenye njia ya haja kubwa wakati unapojisaidia au kukojoa
  • Kutokwa na damu nyingi  wakati wa hedhi au katikati ya hedhi
  • Kushindwa kupata ujauzito(ugumba)
  • Kuhisi uchovu
  • Kuhara au kukosa choo
  • Tumbo kuunguruma
  • Kuhisi kichefuchefu
  • Kuhisi maumivu kabla ya hedhi au wakati wa hedhi au baada ya hedhi huku yakiambatana na maumivu ya kiuno na tumbo la chini.

2. Adenomyosis

Adenomyosis ni ugonjwa unaosababishwa na kuota kwa tishu zisizokuwa za kawaida. Badala ya kujengeka kwenye ukuta wat umbo la uzazi, hizi tishu huota kwenye ukuta wa msuli wat umbo la uzazi(uterus). Dalili zake huwa ni Pamoja na:

  • Kutokwa na damu nyingi ya hedhi tena kwa muda mrefu
  • Kuhisi maumivu makali sana wakati unapokuwa hedhini
  • Kuhisi maumivu makali wakati unaposhiriki tendo la ndoa
  • Damu kuwa na mabonge unapokuwa hedhini
  • Kuhisi maumivu makali maeneo ya tumbo la chini 

3. Maambukizi Katika Via Vya Uzazi Au PID

Maambukizi katika via viungo vya uzazi au PID husababishwa na bakteria katika mfumo wa viungo vya uzazi wa mwanamke. Bakteria hawa wanaweza kusambaa kutoka kwenye uke wako mpaka kwenye tumbo la uzazi, mirija ya uzazi au vifuko vya mayai.

PID inaweza isisababishe dalili au wakati mwingine inaweza kuonyesha dalili kidogo tu. Dalili hizi ni Pamoja na:

  • Maumivu maeneo ya tumbo la chini au kwenye nyonga
  • Kutokwa na uchafu mwingi ukeni wenye harufu na rangi mbaya
  • Kutokwa na damu ukeni nisiyo ya kawaida mfano, yenye utelezi
  • Kuhisi homa au mafua
  • Kuhisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa
  • Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
  • Kuhisi vibaya wakati unapoenda haja kubwa. 

NUKUU: PID inatibiwa na dawa za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa magonjwa ya zinaa. Kwakuwa PID husababishwa na magonjwa ya zinaa, basi kila mwenye maambukizi haya anapaswa apate vipimo kwanza ili aweze kupata dawa za kuondoa maambukizi hayo.

4. Uvimbe Wa Fibroid

Uvimbe wa fibroid sio saratani kwani huota na kujengeka kwenye mfuko wa uzazi(uterus). Wanawake wenye uvimbe wa fibroid mara nyingi huwa hawahisi dalili yoyote.

Dalili za uvimbe wa fibroid hutokana na eneo, ukubwa na idadi ya vivimbe vya fibroid. Dalili zinapojitokeza, zinaweza kuwa Pamoja na:

  • Maumivu ya tumbo yenye kuchoma
  • Mzunguko wa hedhi kubadirika
  • Kutokwa na damu ya hedhi kwa muda mrefu
  • Kuhisi kukojoa mara kwa mara au kushindwa kukojoa
  • Kuhisi mgandamizo au maumivu
  • Kuhisi kukosa choo
  • Kukosa ujauzito(ugumba)
  • Mgongo au miguu kuuma. 

Kumbuka uvimbe wa fibroid unatibiwa na dawa zetu za asili kwa urahisi mno na unapata ujauzito.

5. Vivimbe Kwenye Vifuko Vya Mayai (Ovarian Cysts)

Vivimbe ambavyo hujengekea ndani ya vifuko vya mayai vinaweza kusababisha kutokwa na damu ya hedhi kidogo na tumbo kuuma sana. Vivimbe vingi kwenye vifuko vya mayai hupotea vyenyewe bila matibabu. Hata hivyo, vivimbe vikubwa kwenye vifuko vya mayai vinaweza kusababisha maumivu ya nyonga kwenye maneo ya tumbo la chini.

Tumbo lako linaweza kujaa, ukahisi kama umeshiba au muda mwingine kuunguruma mara kwa mara na kujamba. Kwahi fika hospitali haraka sana ikiwa kama unahisi maumivu makali ya ghafla au homa au kutapika.

Vivimbe kwenye vifuko vya mayai hutibiwa kwa dawa za asili na kuondoa vyanzo vyake.

6. Mimba Kutunga Nje Ya Kizazi

Mimba kutunga nje ya kizazi hutokea wakati yai lililorutubishwa linapojipachika lenyewe nje ya mji wa mimba.

Dalili za mimba kutunga nje ya kizazi zinaweza kuanza kama mimba ya kawaida kabisa. Hata hivyo, unaweza kuendelea kupata dalili zifuatazo:

  • Kutokwa na damu isiyo ya kawaida
  • Kuhisi maumivu kwenye tumbo la chini au nyonga
  • Maumivu kupita kama kisu kinachoma
  • Maumivu begani

NUKUU: Damu nyingi huja kuanza kutoka kama mrija wa uzazi ukipasuka. Hali hii inaweza kuambatana na damu nyepesi, kukosa pumuzi na mshituko wa moyo. Unapoona hivyo wahi kupata matibabu haraka.

Je, Tiba Yake Inakuwaje?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa maambukizi yanayosababisha matatizo kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke na mwanaume pia, pamoja na vivimbe kwenye kizazi. 

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP tukakuunganisha na darasa letu uzidi kujifunza zaidi. Unahitaji huduma, basi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana.

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa