Fahamu Kazi Ya Homoni Ya Prolactin Mwilini Mwako
Na ieleweke kuwa, tezi hii husaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa mwanamke pamoja na uzarishaji wa manii au mbegu kwa mwanaume.
Kwa kawaida prolactin inayozarishwa na tezi ya pituitary ambayo iko kichwani kwenye ubongo. Uzarishaji wake huuongozwa na homoni zingine kitaalam tunaita, “Prolactin-Inhibiting Factors” ambayo inajumuisha dopamine. Wanaume na wanawake huonekana kuwa wana kiwango kidogo cha prolactin katika damu zao. Kwa upande wa wanaume, homoni ya prolactin huchochea uzarishaji wa mbegu za mwanaume ili kurutubisha yai la mwanamke.
NUKUU: Kwa upande wa wanawake, homoni ya prolactin husaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi na kuyafanya matiti yaweze kuota na kukua.
Wakati mwanamke anapokuwa mjamzito, kiwango chake cha homoni ya prolactin huongezeka na kupanda juu. Mtoto anapozaliwa kiwango cha homoni ya prolactin kilichopo ndicho husababisha uzarishaji wa maziwa kwenye matiti kwa ajili ya kunyonyesha mtoto.
Je, Hyperprolactinemia Ni Nini?
Na ieleweke kuwa ikiwa mwanamke au mwanaume ana kiwango cha juu cha homoni ya prolactin kwenye damu, mara nyingi hupatwa na hali inayoitwa, “Hyperprolactinemia.” Bila shaka ukifika hospitali na ukapata vipimo ukakutwa na hali kama hii, basi utaona kwenye cheti chako wataandika neno kama hilo.
Wanawake wenye tatizo la hyperprolactinemia wanaweza kuendelea kutumia vidonge vya uzazi wa mpango ili kuzuia ujauzito ama kurekebisha mzunguko wao wa hedhi. Kiwango kikubwa cha prolactin kinaweza kuingiliana na uzarishaji wa kawaida wa homoni, kama vile estrogen na progesterone.
Baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na kiwango kikubwa cha prolactin, lakini wasionyeshe dalili zozote, wengine wanaweza kuonyesha dalili kama hizi:
- Kutokupata ujauzito
- Kutokwa na maziwa, japokuwa hawanyonyeshi
- Hedhi kubadirikabadirika au kukosa hedhi ndani ya miezi 2-3, nk.
- Mabadiriko au kushindwa kabisa mayai kupevushwa kutokana na mabadiriko katika uzarishaji wa homoni za estrogen na progesterone
Kwa upande wa wanaume, kiwango cha juu cha homon ya prolactine kinaweza kusababisha mambo yafuatayo:
- Kutokwa na majimaji kama maziwa kwenye chuchu
- Kushindwa kudindisha au uume kutosimama
- Kukosa hamu ya tendo la ndoa
- Ugumba
- Kushindwa kufika kileleni au kufika kileleni na kutoa mbegu kidogo tu.
NUKUU: Ikiwa kama utakuwa na dalili kama nilizozitaja hapo juu, basi daktari wako afanyapo vipimo anapaswa aangalie kiwango cha prolactin kwa kupima damu yako.
Kiwango cha juu cha homoni ya prolactin kinaweza pia kuashiria hali zifuatazo:
- Matatizo ya kifua
- Magonjwa ya figo
- Kuvimba kwa tezi ya pituitary(hali hii huwapata wanawake wenye umri chini ya miaka 50)
Je, Unawezaje Kutibu Kiwango Cha Prolactin?
James & Ferdinand Herbal Clinic tunapenda kukushauri kuwa,
- Ikiwa kama una tatizo hili, basi fika hospitali yoyote ya wilaya au mkoa uweze kupata vipimo ili kujua mapungufu ama kiwango cha juu cha homoni ya prolactin.
- Ikiwa kama daktari wako hataweza kugundua chanzo cha kubadirika kwa kiwango cha homoni ya prolactin, au ikiwa kama kiwango cha juu cha homoni ya prolactin kimetokana na uvimbe mdogo katika tezi ya pituitary, lakini bado kuna hali nzuri ya kupata homoni ya estrogen, basi James Herbal Clinic tuna dawa nzuri aina ya CARD HERB, VITAMAKA na REDEEMER unazopaswa kutumia kuondoa tatizo lako.
- Ikiwa kama una uvimbe mkubwa katika tezi ya pituitary ambao unasababisha kiwango chako cha homoni ya prolactin kupanda juu na inaonyesha kuwa njia ya tiba kupitia madawa imeshindikana kuondoa tatizo hilo, basi daktari wako anayekufanyia uchunguzi anaweza kupendekeza kuwa inafaa tatizo hilo liondolewe kwa oparesheni.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa vyanzo vya tatizo la homoni ya prolactin. Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment