Fahamu Mambo Yanayosababisha Koo La Hewa Kuvimba.

Kuvimba kwa koo la sauti hutokana na muwasho au maambukizi. Ndani ya koo lako huwa kuna kiboksi cha sauti, ngozi mbili laini zenye utelezi wa membreni zinazofunika msuli pamoja na mfupa laini. Kwa kawaida, koo la sauti hufunguka na kujifunga kwa ulaini kabisa, huku likitengeneza sauti kupitia mtetemeko wake.

Lakini unapokuwa na tatizo hili, kamba za sauti(vocal cords) huvimba au kuwasha. Hali hii ya kuvimba husababisha masumbufu katika sauti inayotolewa na hewa inayopita kwenye kamba za sauti. Matokeo yake ni kwamba, mlio wa sauti husikika kwa kukwaruza. Kutokana na hali ya uvimbe, basi sauti yako inaweza kuwa yenye kukoroma.

NUKUU: Hali ya koo kuvimba inaweza kuwa ya muda mfupi au ikawa sugu. Matatizo ya kuvimba kwa koo mara nyingi husababishwa na maambukizi na sio kwamba ni makubwa mno. Mwendelezo wa sauti kukwaruza wakati mwingine inaweza kuwa ishara ya matatizo ya msingi ya kiafya.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Hivyo basi, dalili za koo kuvimba huonekana sio chini ya wiki mbili na husababishwa na kitu kikubwa, kama vile virusi. Dalili za kuvimba kwa koo zinaweza kuwa kama ifuatavyo;

  • Kukwaruza
  • Sauti kupotea au kuwa ndogo
  • Maumivu ya koo
  • Koo kukauka
  • Kikohozi kigumu

Nakushauri upate matibabu haraka ikiwa kama;

  • Una matatizo ya kupumua
  • Unakohoa damu
  • Una homa ambayo haiondoki
  • Unakuwa na maumivu makali
  • Unashindwa kumeza vizuri

Ishara na dalili hizi zinaweza kuonyesha uvimbe kwenye koo la chakula na njia ya hewa chini yake. Ingawa uvimbe unaweza kutibiwa nyumbani, lakini bado dalili mbaya zinahitaji matibabu kwa wataalamu. Dalili hizi pia zinaweza kuonyesha kuvimba kwa tishu zinazofanya kazi kama kifuniko (epiglottis) ili kufunika koo la hewa bomba la upepo, hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya watoto na watu wazima.

Je, Nini Husababisha Tatizo Hili?

1Hali Mbaya Ya Kuvimba Kwa Koo

Matatizo mengi ya kuvimba kwa koo huwa ni ya muda na hupona baada ya sababu za msingi kutoweka. Visababishi vya uvimbe mbaya wa koo huwa ni;

  • Maambukizi ya virusi sawa nay ale yanayosababisha homa
  • Sauti kukwama
  • Maambukizi ya bakteria kama vile, diphtheria, japokuwa hii huwa ni mara chache sana.
222. Uvimbe Sugu Wa Koo

Uvimbe wa koo ambao hudumu kwa muda wa wiki tatu hujulikana kama uvimbe sugu. Aina hii ya uvimbe kwa kawaida husababishwa na kuvuta vitu vichafu kama vile hewa yenye vumbi, nk kwa muda mrefu. Uvimbe sugu wa koo unaweza kusababishwa na kamba za sauti kuvimba pamoja na majeraha. Majeraha haya yanaweza kusababishwa na;

  • Kuvuta hewa yenye vitu vyenye kemikali, au moshi mbaya
  • Kuota nyama puani kwa muda mrefu
  • Utumiaji wa pombe muda mrefu
  • Kuimba kwa sauti kubwa sana kupita kiasi
  • Uvutaji sigara
  • Maambukizi ya fangasi au bakteria
  • Maambukizi ya vimelea Fulani

Je, Unawezaje Kujiepusha Na Tatizi Hili?

Ili kuepukana na tatizo hili unapaswa uepukane na mambo kama haya;

  • Kuepukana na maambukizi ya mapafu
  • Epuka kutumia sauti kwa nguvu sana.
  • Epukana na vitu vibaya kama moshi wa sigara, ulevi wa pombe, sehemu za kazi zenye wingi wa kemikali, nk.

Je, Nini Madhara Yake?

Baadhi ya matatizo ya kuvimba kwa koo yaliyosababishwa na maambukizi, maambukizi yanaweza kuenea kwenye maeneo mengine ya koo la hewa.

Thahadhari!

Ili kuzuia hali ya ukavu kwenye koo au muwasho kwenye kamba za sauti, basi fanya hivi vitu vifuatavyo;

  • Epuka unywaji pomba pamoja na kahawa
  • Kunywa maji mengi kila siku
  • Epuka kula vyakula vyenye viungo vingi kama vile pilau, nk
  • Tumia matunda kwa wingi pamoja na mbogamboga
  • Epuka kusugua koo lako mara kwa mara
  • Usivute sigara, na epuka moshi wa sigara kutoka kwa mtu mwingine. Kumbuka moshi wa sigara hukausha koo lako na husababisha kamba za sauti kuwasha.

 Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa matatizo ya uvimbe kwenye koo. Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda.

Karibu sana!

 


 

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Dalili 3 Za Ugonjwa Wa Chembe Ya Moyo (Angina Pectoris)

Jinsi ya Kuondoa Sumu Kwenye Kongosho Lako Kwa Njia Ya Asili Kwa Kutumia Aina Tatu Tu Za Juisi!

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea