Fahamu Matatizo Yanayomfanya Mwanamke Kurudia Kupata Hedhi Mara 2 Kwa Mwezi Mmoja.

Kiwango cha kawaida cha siku za mzunguko wa hedhi huwa ni siku 28, lakini zinaweza kutofautiana kutoka siku 24 hadi 38. Kama mzunguko wa hedhi ni mfupi, basi mtu anaweza akapata hedhi zaidi ya mara moja kwa mwezi.

 

NUKUU: Ingawa mabadiriko kwenye mzunguko wa hedhi huwa sio jambo la kawaida, basi mara nyingi hali ya kupata hedhi mara 2 kwa mwezi inaweza kuwa ishara au dalili za matatizo huko mbeleni.

Je, Unavijua Visababishi 6 Vya Tatizo Hili?

Visababishi vinavyomfanya mwanamke kupata hedhi mara 2 kwa mwezi huwa kama ifuatavyo:

 1. Muda Usioeleweka

Mtu anaweza kuwa na kipindi kifupi cha mzunguko wa hedhi ambao unaweza kuwa na vipindi 2 vya hedhi ndani ya mwezi mmoja. Kwa kufuata hali hiyo, vipindi vyao vinaweza kubadirika na kuwa katika hali ya mzunguko usiobadirika.  

Mabadiriko ya mara kwa mara ndio huwafanya madaktari waweze kutafuta vigezo kamili vinavyoonyesha kutokwa na damu mfululizo kabla ya kupata matibabu ispokuwa tu kuna maambukizi au matatizo mengine.

2. Umri Mdogo

Mzunguko wa hedhi wenye kubadirika huwa ni hali ya kawaida kwa mabinti ambao tayari wameanza kuingia hedhini. Mabinti huonyesha kuwa na mzunguko wa hedhi mfupi au mrefu wakati wa kuvunja ungo, hali ambayo inaweza kusababisha kuwa na vipingi viwili vya hedhi ndani ya mwezi mmoja.

 3. Endometriosis

Endometriosis huwa ni hali ambapo tishu zinazofanana na tishu za ukuta wa mfuko wa uzazi ambazo huota katika eneo jingine la mwili wako. Endometriosis inaweza kusababisha maumivu ya tumbo la chini, tumbo kuunguruma, na kukosa vipindi vya hedhi. Wakati mwingine, damu ya hedhi inaweza kuwa nyingi sana na kuonekana kama hedhi ndio inaanza hata kama inaelekea kuishiria.

NUKUU: Daktari anaweza wakati mwingine kupima tatizo hili kwa kutumia kipimo cha Ultrasound au Pelvic Exam. Hata hivyo, upasuaji mdogo unaojulikana kama, “laparoscopy” huwa ni njia nzuri katika kupima hali hii.

 4. Kipindi Cha Kuelekea Kukoma Hedhi

Muda unapowadia mwanamke kukoma hedhi, mfumo wa homoni huanza kubadirika. Hali ya kuonyesha kama hedhi imekoma inaweza ikadumu mpaka miaka 10. Katika kipindi hicho, watu mara nyingi hupatwa na hali ya hedhi kubadirika au vipindi vya hedhi kuruka, au kutokwa na damu ya hedhi nyingi sana au kidogo tu, au kutokwa na damu nzito ya hedhi au nyepesi.

Kama mtu hakuweza kupata hedhi kwa muda wa miezi 12, basi tayari atakuwa ameshakoma hedhi.

 5. Matatizo Ya Tezi Ya Thyroid

Tezi ya thyroid huwa ina kazi ya kurekebisha kazi ya mfumo wa homoni mwilini mwako. Tezi hii ndogo yenye umbo kama la kipepeo huwa inakaa chini ya koromeo kwa mbele, na huendesha utendaji kazi nyingi kama vile joto la mwili, nk.

Mzunguko wa hedhi kubadirika au kukosa hedhi huwa ni dalili zinazoambatana na matatizo ya tezi ya thyroid.  Dalili za tezi ya thyroid kuwa na uwezo mdogo wa kufanya kazi huwa ni kama ifuatavyo:

  • Kuhisi baridi mara kwa mara
  • Kukosa choo
  • Kujihisi uchovu muda wote
  • Kutokwa na damu nyingi ya hedhi
  • Ngozi kuwa nyeupe
  • Uso kukunjamana 
  • Kiwango kidogo cha mapigo ya moyo
  • Kuongezeka uzito

Dalili za tezi ya thyroid kufanya kazi kupita kiasi huwa ni kama ifuatavyo:

  • Kuhisi joto mara kwa mara
  • Macho kuwasha
  • Kuhisi kuhara
  • Kukosa usingizi
  • Mapigo ya moyo kwenda mbio
  • Uzito kupungua

NUKUU: Matatizo haya yote mawili yanatibika, hivyo unapaswa kufika hospitalini na kufanya vipimo.

 6. Uvimbe Wa Fibroid

Uvimbe wa fibroid huota ndani ya mfuko wa kizazi. Mara nyingi uvimbe huu huwa sio saratani bali unaweza kusababisha kutokwa na damu hasa damu nyingi ya hedhi. Dalili za nyonyeza za uvimbe wa fibroid zinaweza kuwa kama ifuatavyo:

  • Kuhisi sehemu za nyonga kujaa
  • Kukojoa mara kwa mara
  • Maumivu ya kiuno
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

 Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

Je, unasumbuliwa na tatizo a kupata hedhi mara 2 ndani ya mwezi mmoja? James Herbal Clinic tuna dawa nzuri kabisa zenye uwezo wa kuondoa tatizo hili kwa muda mfupi tu. Unahitaji huduma, basi tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana! 

Comments

Popular posts from this blog

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa