Fahamu Vyanzo Na Dalili Za Uric Acid
Je, Nini Maana Ya Uric Acid?
Uric acid ni uchafu au taka iliyobaki kutokana na michakato ya kawaida ya kemikali katika mwili, nayo hupatikana kwenye mkojo na damu. Mkusanyiko usio wa kawaida wa uric acid mwilini unaweza kusababisha ugonjwa unaoitwa gout. Kuongezeka kwa viwango vya uric acid kwenye damu na mkojo inaweza kuwa athari.
Kiwango cha juu cha uric acid kwenye mkojo huwa ni uric acid nyingi kwenye damu. Uric acid hutengenezwa wakati wa kumeng’enywa kwa chembechembe ngumu. Chembechembe ngumu hupatikana katika vyakula fulani na huundwa na mwili.
Damu hupeleka uric acid kwenye figo. Figo hupitisha uric acid nyingi kwenye mkojo, ambayo baadaye hutoka mwilini.
Kiwango cha juu cha uric acid kinaweza kusababishwa na gout au mawe kwenye figo. Lakini watu wengi walio na viwango vya juu vya uric acid hawana dalili za mojawapo ya hali hizi au matatizo yanayohusiana tatizo hili.
Je, Nini Chanzo Chake?
Kiwango cha juu cha uric acid kinaweza kuwa matokeo ya mwili kutengeneza asidi nyingi, bila kuiondoa mwilini. Sababu za kuongezeka kwa uric acid kwenye damu ni pamoja na:
- Unywaji wa pombe sana
- Ulaji wa nyama nyekundu hasa za mbuzi au supu
- Unywaji wa soda sana,au ulaji wa vyakula vingi sana vyenye sukari
- Ugonjwa wa presha ya kupanda
- Madawa ya kuongeza kinga mwilini
- Matatizo ya figo
- Upungufu wa damu mwilini
- Upungufu wa vitamini B3
- Unene
- Ugonjwa wa ngozi unaosababisha harara kwenye jointi za viwiko au magoti
- Vyakula vyenye chembechembe ngumu kama vile maini, nyama pori, nk
Je, Ni Wakati Gani Inakupasa Ufike Kwenye Kituo Cha Afya?
Kiwango cha juu cha uric acid sio ugonjwa. Sio kila wakati husababisha dalili. Lakini mhudumu wa afya anaweza kuangalia viwango vya asidi ya mkojo kwa watu walio na shambulio la gout au aina fulani ya mawe kwenye figo.
Ikiwa unafikiri mojawapo ya dawa zako inaweza kusababisha kiwango chako cha juu cha uric acid, basi zungumza na mtoa huduma wako.
Je, Dalili Zinakuwaje?
Uric acid kwa kawaida huwa haisababishi dalili. Watu wengi huwa hawajui kuwa wanayo hadi pale viwango vyao vya uric acid vinapokuwa juu sana na kusababisha gout au mawe kwenye figo.
Dalili za shambulio la gout katika moja wapo ya viungo vyako ni pamoja na:
- Maumivu makali
- Rangi nyekundu maeneo yanayovimba
- Mwili kuvimba
- Kuumia hata unapoguswa na shuka unapojifunika
- Unyevunyevu au kuhisi kama vile jointi zipo kwenye moto
Dalili za mawe kwenye figo nazo huwa kama hizi zifuatazo:
- Maumivu ya kiuno
- Kichefuchefu au kutapika kunakosababishwa na maumivu
- Kuhisi homa
- Damu kwenye mkojo
- Kuhisi maumivu pale unapokojoa
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara
- Mkojo kutoa harufu au kuwa na rangi ya ukijivu.
Je, Nini Suluhisho Lake?
James Herbal Clinic tunazo dawa za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa vyanzo vya uric acid. Unahitaji huduma,wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu Sana!
Comments
Post a Comment