Haya Ndio Mambo 6 Yanayomfanya Mwanamke Kutokwa Na Damu Nyingi Bila Mpangilio.

Ndugu msomaji na ieleweke kuwa, tatizo hili huwasumbua wanawake wengi walio katika umri wa kuzaa na baadhi ya wanawake ambao tayari wameshafikia ukomo wa kuzaa. Kwa mwanamke aliyekwishafunga kupata hedhi kuendelea kupata damu ya hedhi au kutokwa na damu ukeni bila ya mpangilio siyo hali ya kawaida.

Mwanamke anaanza kuvunja ungo kuanzia umri wa miaka 12 na hufikia ukomo kuanzia umri wa miaka 45. Kupatwa na damu ukeni chini ya umri wa miaka 40 kuna vyanzo vingi kama tutakavyoona.

Je, Nini Chanzo Chake?

Na ieleweke kuwa, kwa kawaida tatizo hili husababishwa na mambo yafuatayo:

  • Mabadiliko katika uwiano wa homoni(Hormonal Imbalance)
  • Uwepo wa uvimbe katika tumbo la uzazi
  • Matumizi ya dawa za homoni mfano sindano au vipandikizi
  • Kuweka kitanzi katika kizazi
  • Mshtuko wa mwili au hali ya mabadiliko ya mazingira.
  • Kuharibika kwa mimba

Mwanamke mwenye umri wa zaidi ya miaka 45 kupata damu ukeni bila ya mpangilio ni vema kuchunguza kwa undani kwani wana uwezekano mkubwa wa kuwa na saratani ya kizazi au shingo ya uzazi.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Mwanamke anapokuwa na tatizo hili hupatwa na dalili zifuatazo:

  • Kuona siku za hedhi zaidi kuliko kawaida yake, au kuona katikati ya mzunguko yaani aliona, ikaacha sasa inaanza tena.
  • Damu inaweza kuwa nyingi na mwanamke akabadilisha pedi mara nyingi kuliko kawaida  yake au akapata matone kidogokidogo lakini kwa muda mrefu.
  • Damu inaweza kuwa nyepesi au nyeusi au nzito yenye mabonge.
  • Hutoa harufu isiyo ya kawaida endapo ata-bleed kwa muda mrefu
  • Maumivu makali ikiwa damu inatoka na mabonge
  • Mgonjwa huchukua muda mrefu hata zaidi ya majuma mawili akiwa anatokwa na damu,
  • Kuumwa tumbo chini ya kitovu ikiwa ni dalili za kupatwa na maambukizi ya PID kwa kuwa bakteria hupenda sana mazingira ya damu.

Hali inapoendelea mwanamke hupoteza uwezo wa kushika mimba na huathiri uzazi kwani hushindwa kufanya tendo la ndoa, homoni zinavurugika na maambukizi ya kizazi huathiri mirija ya mayai.

Uvimbe wa Fibroid ukiwa ndani ya kizazi husababisha damu zitoke bila ya mpangilio na kuzuia mimba kukua na hata ikiingia inaweza isiendelee. James Herbal Clinic huwa tunapenda kuwashauri sana wagonjwa wenye tatizo hili kuwa ni vyema ukafika hospitali za wilaya au Mkoa ili kufanya vipimo vya Ultrasound, na upatapo majibu, basi unaweza kufika James Herbal Clinic ukapata matibabu ya dawa za asili ambazo zina uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya uvimbe katika kizazi ama ugumba kwa wanawake.

 Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya uvimbe katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Pata huduma huduma hii, pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP tunakuunganisha na darasa letu ili uweze kupata masomo kila siku ya afya.

Je, unahitaji huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Dalili 3 Za Ugonjwa Wa Chembe Ya Moyo (Angina Pectoris)

Jinsi ya Kuondoa Sumu Kwenye Kongosho Lako Kwa Njia Ya Asili Kwa Kutumia Aina Tatu Tu Za Juisi!

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea