Haya Ndio Mambo 7 Yanayosababisha Kutokwa Na Damu Katika Njia Ya Haja Kubwa (Rectal Bleeding)

Hali ya kutokwa na damu katika njia ya haja kubwa mara nyingi hujionyesha yenyewe mara unapokuwa chooni baada ya kujipangusa na tishu (toilet paper), ama wakati kinyesi kinapotumbukia kwenye sink na kuyafanya maji kubadirika na kuwa mekundu. Wakati mwingine hali hii inaweza kujidhihirisha kwenye kinyesi baada ya kukiona kuwa na rangi nyekundu sana.

Rangi ya damu inaweza kuonyesha mahali damu inakotokea:

  • Damu nyekundu yenye kung’aa huonyesha damu inayovuka kwenye utumbo mpana au njia ya haja kubwa
  • Damu yenye rangi ya weusi mara nyingi huvuja kutoka kwenye utumbo mwembamba au mpana
  • Damu yenye rangi ya weusi ulioiva sana huvuja kutoka kwenye tumbo la chakula, kama vile kwenye vidonda vya tumbo

Sio kwamba matatizo yote ya kuvuja kwa damu kwenye njia ya haja kubwa huonekana kwa macho. Wakati mwingine kutokwa na damu katika njia ya haja kubwa huonekana kwa kuangalia kinyesi kupitia darubini. Pia kuna vipimo vijulikanavyo ‘Hemoccult’ ambavyo hutumiwa na madaktari.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Dalili za tatizo hili mara nyingi huwa kama ifuatavyo:

  • Maumivu sehemu ya njia ya haja kubwa
  • Damu kwenye kinyesi yenye kung’aa sana
  • Kinyesi kigumu
  • Kuhisi uchovu
  • Kizunguzungu

Je, Nini Visababishi Vyake?

Kutokwa na damu damu katika njia ya haja kubwa inaweza kutokea kutokana na sababu nyingi mbalimbali. Vyanzo vya kawaida vya tatizo hili ni pamaoja na:

  • Mpasuko ama kidonda katika njia ya haja kuwa
  • Kukosa choo muda mrefu
  • Kupata kinyesi kugumu
  • Bawasiri
  • Saratani ya utumbo mpana
  • Uvimbe kwenye njia ya haja kubwa
  • Kuvimba kwa utumbo mpana kutokana na maambukizi

 Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa matatizo ya kutokwa na damu katika njia ya haja kubwa pamoja na madhara yanatosababisha kutokwa na damu kama vile baawasiri, nk. 

Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa