Hizi Ndizo Sababu Kuu 10 Zinazomfanya Mwanamke Kushindwa Kupata Mimba.

Ndugu msomaji katika makala hii, wanaume wenzangu napenda niwajuze tu hivi, unapoona mkeo hapati ujauzito, tafadhali usipende kulaumu wala kuchukia wala kuamsha ugomvi ndani ya ndoa. Jitahidi kuwa mvumilivu tu maana hii huwa ni hali ya kawaida ambayo ikitibiwa inaweza ikaondoaka haraka tu. Tiba za mimea ya asili ni njia pekee zinazotatua matatizo makubwa ya afya. Kaka Sephu bila shaka umenielewa hapo ulipo!

Je, Ugumba Ni Nini?

Hii ni hali ya wapenzi au mke na mume kutopata ujauzito baada ya kushiriki tendo la ndoa kwa muda wa mwaka mmoja mfululizo. Ugumba unaweza kuwa mtu hajawahi kubeba mimba kabisa (primary infertility) tangu azaliwe au mtu ambaye amewahi kuzaa lakini kwa sasa ameshindwa kubeba ujauzito (secondary infertility).

NUKUU: Kwa kawaida hali hii imekua ikiongezeka kadri miaka inavyosonga mbele kwa sababu mbalimbali kama mionzi ya mawasiliano yaani wi-fi , magonjwa mapya ya binadamu na kadhalika. Kwa wanawake utafiti mpya unasema uwezo wao wa kubeba mimba unaanza kupungua baada ya miaka 30 ya umri kutokana na kuanza kuishiwa nguvu kwa viungo vya uzazi. Ugumba leo unaonyesha kuwa na vyanzo vingi sana ambavyo vingine havifahamiki mpaka leo  lakini hebu tuone vyanzo muhimu vya ugumba.

1. Utoaji Mimba (Abortion

Huenda hichi ndio kitakua chanzo kikuu cha ugumba miaka ijayo kwani siku hizi karibia kila mwanamke ana sababu za kutoa mimba hasa wanafunzi walioko vyuoni. Utoaji wa mimba una hatari nyingi ambazo huweza kuleta ugumba kama kuoza au kuharibika kwa kizazi baada ya kushambuliwa na bakteria, au kuwa na makovu yanayoletwa na vifaa vinavyotumika kutoa mimba kwenye mfuko wa uzazi na mlango wa uzazi huweza kusababisha ugumba usiotibika.

2. Matatizo Ya Vizarishaji Vya Mayai (Ovary)

Ovari ni kiungo ambacho kinatoa yai moja kila mwezi ili liweze kurutubishwa na mbegu za mwanaume. Lakini inaonyesha kuwa kuna magonjwa mengi hivi sasa kama vile maambukizi katika via vya uzazi au PID ambayo yanaweza kusababisha ovari hiyo ikaugua na kushindwa kutoa mayai.  Mwanamke ana ovari mbili lakini moja ikiuugua tu na nyingine haifanyi kazi mfano ugonjwa wa vivimbe kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts). 

3. Matatizo Ya Mirija Ya Uzazi

Ovari zimeunganishwa kwenye  mirija ambayo hupitisha mayai kwenda kwenye mfuko wa uzazi. Wakati mwingine mirija hiyo huziba kwa sababu mbalimbali kama vile maambukizi kama niliyoyataja hapo juu, hivyo mayai hushindwa kupita na kusababisha ugumba. mfano ugonjwa wa endometriosis, upasuaji na peritonitis.

 4. Matatizo Ya Kizazi

Kizazi ndio sehemu kuu ambayo mtoto hutunzwa na kuishi kwa miezi yote tisa, tatizo lolote linaloshambulia kizazi huleta ugumba, mfano; makovu ndani ya kizazi, uvimbe ndani ya kizazi, kugeuka kwa kizazi na magonjwa ya zinaa kama kaswende na kadhalika. 

5. Saratani

Kansa ya kizazi huzuia yai la mama lililorutubishwa kushindwa kujipachika kwenye kizazi ili kukua, hivyo huchangia sana mimba kuharibika au kutotungwa kabisa. 

6. Matatizo Ya Mlango Wa Uzazi

Oparesheni za kizazi, utoaji wa mimba na magonjwa ya zinaa huweza kusababisha kuziba kwa mlango wa uzazi, hivyo mbegu za kiume kushindwa kabisa kupita kwenye mlango wa uzazi na kusababisha ugumba.

7. Magonjwa Mengine Ya Mwili

Magonjwa yeyote ya binadamu  ambayo huingilia mfumo wa homoni za uzazi huleta ugumba mfano magonjwa ya ini, kisukari, hyperthyrodism, na kadhalika. 

8. Matumizi Sigara Na Pombe

Unywaji wa pombe sana na uvutaji wa bangi huzuia yai kutoka kwenye ovari, lakini pia uvutaji wa sigara hupunguza uwezo wa yai kutembea kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mfuko wa uzazi na wakati mwingine husababisha mimba kutunga nje ya kizazi.

9. Msongo Mkubwa Wa Mawazo

Ukiwa unatafuta mtoto tayari ukiwa umepaniki kwamba huenda usimpate husababisha mwili kutoa homoni kitaalamu kama cortisol ambazo huzuia kazi za homoni za uzazi kitaalamu kama (gonadotropin releasing hormone) hivyo hali huzidi kua mbaya. 

10. Uzito Uliopitiliza

Mwili mkubwa unaingilia mfumo wa utengenezaji homoni za uzazi, hivyo huweza kuleta ugumba katika umri mdogo sana, hivyo kupunguza uzito ni moja ya njia bora kabisa ya kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuzuia ugumba. Unahitaji kupunguza uzito, pata NEOTONIC na PRE-ENERGY POWDER.  

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tuna dawa za asili zenye uwezo wa kuondoa tatizo hili bila kufanya upasuaji kwani zina uwezo wa kuua vimelea wote wanaosababisha tatizo hilo. 

Unataka huduma, basi tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Comments

Popular posts from this blog

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa