Je, Inafaa Mwanamke Kuwa Na Tumbo Kubwa?

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa.

Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi.

Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote.

Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama:

  • Vyakula feki (Junk food)
  • Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi
  • Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
  • Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala
  • Kukaa masaa mengi kwenye kiti
  • Kutokujishughulisha na mazoezi
  • Mfadhaiko (stress)
  • Kula wali kila siku
  • Ugali wa sembe
  • Kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi, maandazi, nk)

Umuhimu wa mwanadamu upo kwenye kujua hali ya AFYA yake ikoje , watalaamu na madaktari wanatushauri ni muhimu kupima na kujua afya yako ikoje lakini wengi wetu tumeshindwa kupima na kujijua kiafya je afya zetu ni mgogoro au ni njema tumebaki na dhana za kukaa bila kupima afya zetu na kujiona tuko sawa tu. ...
Afya njema haina thamani ya kuinunulia. Usione uvivu au taabu kupima afya yako. Sasa unayo fursa nzuri ya kupima afya yako bure kabisa itumie fursa hii usichelewe bado ipo 
Kupima afya si lazimia uwe mgonjwa au unaumwa la hasha, tunaweza kujiona tuko kamili au fit kabisa na tuko ngangari kumbe afya zetu ni mgogoro vijiamaaradhi vinatunyemelea bila hata kujijua wenyewe mana twajiona fit kila wakati.

Njia rahisi ya kujua afya zetu na kujiona tuko fresh ni kupima mara kwa mara kitaalamu.

Je, Unapaswa kufanya nini ili kuzuia tumbo lisiwe kubwa? Jibu ni hili, jitahidi sana kuacha kutumia vyakula feki, kama vile, kukaa magengeneni na kula,

  • miguu ya kuku,
  • vichwa vya kuku,
  • utumbo wa kuku,
  • filigisi au maini ya kuku,
  • chips kavu,
  • ice cream,
  • chokleti,
  • vitu vilivyokobolewa au kusindikwa, nk.

Je, Ufanyeje Ili Kuondoa Tatizo La Tumbo Kubwa?

Ushauri: Jitahidi kunywa maji vuguvugu glasi 1 kila siku asubuhi unapoamka, pia fanya mfungo kwa kuacha kutumia vyakula vilivyopikwa, tumia juisi hasa ya nanasi, au tango.

Kwakufanya hivyo itakusaidia kupunguza tumbo na uzito wa mwili.

Neno La Faraja: Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia. Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako. (Angalia Ayubu 22:21).

Mwisho: Kwa ushauri, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa