Je, Kutoa Mimba Ni Haki Mbele Za Mungu?

 Leo tunajadili umuhimu wa tumbo la mama kama mahali pekee ambapo Mungu alipachagua kuwa makazi ya muda ya mtoto mchanga kabla hajazaliwa. James Herbal Clinic tunataka kutafakari leo na kuwauliza akina mama wa leo, je, matumbo yao yamekuwa mahali salama kwa makazi ya watoto? Lakini tunatafakari pia jinsi Mungu alivyomtayarisha kila mtoto kwa huduma, utumishi au madaraka katika uhai wake baada ya kuzaliwa na kukua. Lakini tunataka kuwatoa wasiwasi wanawake wote kuwa hicho kilichomo ndani ya tumbo lako, au hicho kinachoitwa mimba ni binadamu mdogo, mwenye akili na mwenye kujimudu katika hatua yake ya kukua.

Kwa hiyo kitendo chochote cha kumwua mtoto aliyemo ndani ya tumbo la mama katika kile kinachoitwa utoaji mimba, ni mauaji ya binadamu mdogo ambaye anakuwa na kwamba baada ya kumwua hakuna binadamu mwigine anayechukua mbadala wake, anakuwa amepotea moja kwa moja na hatutamwona tena kwa macho, tukamshika, tukambembeleza.

Mungu hutumia tumbo la mwanamke kuleta uhai au kiumbe kipya duniani; wito wa kuheshimu na kutunza mimba; kila binadamu ni wa pekee na kila binadamu analetwa duniani kutimiza matakwa fulani ya Mungu; hakuna binadamu aliyeumbwa na Mungu asiyekuwa na faida, naongea lakini ninaumia moyoni mwangu kwa kitendo hiki.


Mafundisho kutokana na sehemu mbalimbali za maandiko

  • Kila mama mjamzito hubeba uhai wa binadamu kamili tumboni mwake
  • Kila mtoto katika tumbo la mama ni wa  pekee na asiyeweza kujirudia
  • Kila mama anabeba Baraka ya Mungu kwa kuwa mshiriki wa uumbaji pamoja na Mungu; hivyo kila mama mjamzito ni MBARIKIWA WA MUNGU
  • Kila binadamu amepangiwa na Mungu majukumu yake hapa duniani tangu akiwa tumboni mwa mama yake
  • Ni wajibu wa kila mama kuitunza mimba yake na kuilinda dhidi ya mashambulio yoyote yale
  • Ni Mungu pekee mwenye kumjua kila binadamu kwa undani jinsi alivyo kutokana na tendo lake la uumbaji  [soma Zab. 8:5-6]
  • Tendo lolote la kutoa mimba ni tendo la kuua mtoto anayekua tumboni mwa mama na aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na aliyeshirikisha pande tatu: Mungu, mwanaume na mwanamke
  • Kila mwanamke anayetoa mimba anamuua mtoto wake mwenyewe, anaiua sehemu ya nafsi yake na anabeba laana na kuondoa ubarikio wa Mungu
  • Kila binadamu na amshukuru Mungu kwa kuumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha
  • Kila binadamu ni tunda la fikra ya Mungu [soma Mwa. 1:26] na hivyo kila binadamu anashiriki u-takatifu wa Kimungu kwa njia ya pumzi hai ya Mungu isiyokufa, ndiyo roho yake.

Mungu awabariki sana, na napenda niishie hapa.

Kwa ushauri au huduma, basi unaweza kuwasiliana kwa namba zetu hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Kwa maoni na ushauri, acha ujumbe katika barua pepe yetu: samkusundwa@gmail.com 

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!     

Comments

Popular posts from this blog

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa