Je, Vyakula Visivyokuwa Na Faida Mwilini Vinaweza Kuwa Vyanzo Vya Magonjwa Katika Mwili Wako?

Kamwe ugonjwa haupatikani bila sababu. Kwa kuzivunja kanuni za afya, ugonjwa hupata njia na kukaribishwa. Watu wengi huugua kutokana na makosa ya wazazi wao…Walakini, watu wengi zaidi huwa wagonjwa kwasababu ya matokeo mabaya yao wenyewe. Wanazivunja kanuni zinazohusu afya njema kwa desturi zao za kula, kunywa, kuvaa mavazi ya kubana, na kufanya kazi nyingi kupita kiasi. Uhalifu wao wa kawaida wa maisha huleta matokeo halisi, na wakishikwa na ugonjwa, wengi hawakubari ya kwamba wao ndio wamejiletea madhara, bali humunung’unikia Mungu kwa ajili ya maumivu yao.

 

Watu wengi wana mazoea ya kula vitu vingi ambavyo huwa sio vizuri kwa afya zao. Bila shaka hili limekuwa wazi kabisa kuanzia katika familia zetu, mpaka shuleni, na vyuoni. Baadhi ya watu wanashindwa kufikiri kabisa kuwa huenda vyakula wanavyokula ni vizuri na vinafaa kwa afya zao au vinaweza kusababisha madhara baadaye katika miili yao. Wakati mwingine tumekuwa tukila vyakula pasipokujua kuwa vina madhara gani katika afya zetu.


Sasa yafaa sana kila mmoja wetu ajifunze  ili kujua vyakula gani vinafaa na vyakula gani vinapaswa kuepukwa, na baadaye tuwe waangalifu kabisa ili kujiepusha na ulaji wa vitu ambavyo vinaweza kutupatia madhara katika miili yetu.

 

NUKUU: Tatizo la kukosa choo linazidi kushamili sana katika jamii ya watu. “Mara nyingi utovu wa kiasi umekuwa ukianzia nyumbani. Ulaji wa vyakula vilivyokolezwa sana na viungo au mafuta mengi kama vile pilau, nyama rosti, chips mayai, au ugali wa sembe, mkate mweupe, chapatti, maandazi, nk, kamwe havifai kwa afya kwani hudhoofisha viungo vya mwili vinavyohusika na uyeyushaji wa chakula tumboni, na hivyo kumfanya mtumiaji kuwa na tatizo la kukosa choo, na baadaye kukaribisha magonjwa mabaya kama vile bawasiri, kisukari pamoja na magonjwa ya moyo.

 

Mama wana kazi ya kuwasaidia watoto wao kuwa na mazoea mema na kukipenda chakula kisafi. Kwa habari ya vyakula na vinywaji vya viwandani kama vile juisi, biskuti, chokoleti na ice-cream, njia salama ni kutovigusa, kutovionja, na kutovitumia kabisa. Nafikiri kina mama wanaolea familia zao mumenielewa ninachokieongea hapa.

Danieli hakuweza kuyashinda majaribu mpaka kuwa mtu wa Mungu kama asingefuata mafundisho aliyofunzwa na mama yake nyumbani mwao. Mama yake Danieli alikuwa mtu anayempenda Mungu sana, na hivyo alishika maagizo yote na akafuata kanuni na sheria za Mungu. Pia alijifunza sana hata unabii, na ndio maana mara nyingi alikuwa akimuelekeza mtoto wake.

Danieli alipoingia utumwani, hakusumbuka hata kidogo maana alijua yupo na Mungu. Isitoshe hakutamani vyakula vibaya, vya asana kama tunavyopena leo mitaani, mashuleni na hata nyumbani. Danieli na wenzake hata alipoandaliwa chakula cha mfalme, wao hawakuwa tiyari kukipokea na kukitumia, bali walisema maneno haya tu; Tafadhali utujaribu sisi watumishi wako muda wa siku kumi; na watupe mboga za majani tule, na maji tunywe. Danieli 1:12. Najua kuna watu wanafahamu ni neno mtama, mkitaka nikueleweshe, wewe nitafute tu kwa meseji nitakuelekeza utaelewa.


Je, Dalili Za Ugonjwa Zinapoanza Kuonekana Unapaswa Ufanyeje?

Tendo moja ambalo ni chanzo cha magonjwa mengi na madhara mengi, ni kutumia namna za dawa zenye sumu bila kiasi. Kuna watu wengine ambao wakishikwa na ugonjwa fulani, hawajisumbui kupeleleza chanzo au asili ya ugonjwa. Kwa kutumia dawa zenye sumu, wengine hujiletea magonjwa ya maisha, na watu wengi hufa ambao wangeliendelea kuishi kama wangetumia njia ya tiba za asili kwa ajili ya kuponya magonjwa yao kama vile kukosa choo kwa muda mrefu.


Matatizo ya uyeyushaji chakula tumboni yanaweza kuathiri ubora wa maisha yako. Hali ya tumbo kushindwa kuyeyusha chakula inaweza kusababisha kiungulia, matatizo ya majipu, tumbo kujaa gesi au kujamba jamba, kuharisha, kukosa choo, tumbo kuuma, au kupatwa na vichomi.

Mwisho wake kabisa, huwa ni kupatwa na magonjwa mabaya kama vile matatizo ya moyo na kisukari.

Mungu akubariki sana ndugu msomaji, nakaribisha maoni kutoka kwako, na maswali juu ya afya.

Kwa mawasiliano, tupigie; 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Comments

Popular posts from this blog

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa