Fahamu Dalili Za Ugonjwa Wa Thyphoid

Je, Homa Ya Matumbo(Typhoid) Ni Nini?

Homa ya matumbo (Typhoid) kwa kawaida husababishwa na bakteria anayeitwa Salmonella Typhoid

Ugonjwa huu huambukizwa kwa mtu kwa kula au kunywa chakula au maji yalio na kinyesi cha mtu aliyambukizwa. Bakteria hawa hutoboa na kunyonya chakula kwenye matumbo ya binadamu.

Je,  Dalili Zake Ni  Zinakuwaje?

Kwa kawaida dalili ya ugonjwa huu huwa ni nyingi sana, nazo huwa kama hivi ifuatavyo:

  • Homa kali
  • Kutoka kwa majasho mengi
  • Kuharisha (bila ya kutoa damu)
  • Mara nyingine, vitone vyekundu huonekana kwenye mwili.

NUKUU: Kwa kawaida, homa ya matumbo isipotibiwa hugawanyika katika hatua nne, kila hatua ikichukua takriban wiki moja.

Je, Katika Wiki Ya Kwanza Inakuwaje?

Kwa kawaida mgonjwa hupatwa na dalili nyingi mbalimbali kama nilivyosema mwanzo, nazo zipo hivi kama zifuatazo:

  • Joto la mwili huongezeka
  • Kichwa huuma
  • Kukohoa
  • Damu kutoka kwa pua, ingawa tukio hili huwa ni nadra kutokea.
  • Maumivu ya tumbo pia huweza kutokea

Je, Katika Wiki Ya Pili Inakuwaje?

Katika wiki ya pili mgonjwa pia hupatwa dalili zingine ambazo humfanya kuwa na masumbufu sana, nazo huwa kama hizi:

  • Homa huongezeka
  • Mgonjwa huanza kupagawa, kama mwenda wazimu
  • Vitone vyekundu huanza kutokea kwenye kifua
  • Mgonjwa huharisha, takriban mara sita au nane kwa siku.
  • Kutapika kwa mgonjwa
  • Ini la mgonjwa huvimba
  • Homa ya mgonjwa huongezeka katika wakati wa alasiri kwenye wiki ya kwanza na ya pili.

Je, Wiki Ya Tatu Inakuwaje?

Wiki ya tatu hali huzidi kuwa mbaya sana na kumfanya mgonjwa kujisikia vibaya kiasi kwamba hupatwa na dalili kama hizi zifuatazo;

  • Matumbo hutoa damu.
  • Matumbo hutoboka

Wiki ya tatu ikishamalizika, basi hali ya homa ndipo huanza kutulia. Hivyo hali hii huendelea hadi wiki ya nne.

Kumbuka: Homa ya matumbo haiuwi binadamu. Ila wakati unapoona ya dalili zilizoainishwa hapo juu ni vema ukawahi vipimo na kinga  sahihi za kitaalamu katika kituo cha afya kilicho karibu na wewe.

 Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tuna dawa za asili zenye uwezo wa kuondoa tatizo hili la vimelea wa  maambukizi haya ya typhoid. Unahitaji huduma, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana! 

Comments

Popular posts from this blog

Aina 9 Ya Vyakula Unavyopaswa Kuviepuka Unapokuwa Na Tatizo La Figo

Fahamu Mambo Yanayosababisha Uke Kulegea

Mambo 6 Yanayopelekea Mwanamke Kuhisi Maumivu Makali Anaposhiriki Tendo La Ndoa